Maamuzi ya Serikali kuhamia Dodoma yalitawaliwa na ukurupukaji mkubwa

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
10,489
34,793
Dodoma kuwa makao makuu ilitakiwa kazi ifanyike na itiliwe mkazo kwa ustadi toka awamu ya Kwanza ya utawala, kulazimisha sa hv Kuhamishia kila kitu kwenda Dodoma ni kuumiza rasilimali fedha ya nchi ambayo ipo strictly limited.

✓Dar esalaam ilikuwa imejitosheleza Kwa kila kitu , kuanzia majengo , miundo mbinu n.k unaanzaje kujenga upya sehemu nyingine tena na kitu kile kile , huku ukiwa na uhaba wa mambo mengi ya mhimu.

✓ Sababu nyingi zilizokuwepo za kuhamisha makao makuu toka DSM kwenda Dodoma now ni useless , Dunia sa hv ipo kwenye kiwango cha juu cha ustarabu hakuna purukushani za kivita , pia technolojia inakua Kwa Kasi Sana , no need ya mtu kutoka mbali kuja makao makuu kuhudumiwa , hata interview na maombi ya kazi now yanafanyika online.

✓Mawazo ya mkwere ya kutengeneza zones yalikuwa na maana Sana , zone hzi zingehudumia watu kuepuka ulazima kujazana makao makuu na Kwa kweli miji iliyobeba hadhi ya zone ilikua Kwa Kasi ya kuridhisha kipind cha mkwere e.g Mwanza, Arusha, Mbeya , Mtwara na hat Dodoma yenyewe.

Ninaungana na ndugu Mchungaji msigwa kuwa JPM hakuwa mtu sahihi kuvivaa viatu vya uraisi Kwa sasa , jamaa alikuwa mzalendo aliyepitwa na wakati , the guy was more outdated.

Mpango wake wa kuhamisha ofisi za kiserikali toka DSM kwenda Dodoma kumeathiri sana vitu vingi sana. Arusha imedorora Sana , mikutano yote ilizimwa kule , Mwanza nayo hamna kitu mji kama umesimama kabisa , Mbeya nayo , Mtwara ndo kabisa.

Dar es salaam imeathirika Kwa namna moja ama nyingine japo somehow mji umebaki strong because of its firm foundation Ila jamaa alikuwa anauvunja vunja kabisa mji.

Familia nyingi zimeathirika Sana , ndoa nyingi za wafanyakazi zimevunjika na watu walikuwa kwenye msongo mkubwa wa mawazo sababu ya kutenganishwa Kwa lazima.

Nini kimetokea sasa , Jiwe amekufa huku mji wa Dodoma ukiwa bado haujakamilika na bado unahtaji multibillion USdollar kukamilika. At the same time DSM ina kila kitu kinachohtajika , kiukwel mama Samia yupo kwenye sintofahamu Sana namna ya kufanya resources allocation.

Nini kifanyike , kwa maoni yangu , ofisi zilizopo tayari ziendelee kufanya kazi Dodoma , na ambazo hazipo tayar zibakie DSM, na pia zones ziendelee kupewa nguvu kama mwanzo ili kuboost uchumi wa kikanda ambao ulikuwa kama umekufa kabisa.....
 
Wewe ndiyo una mawazo ya kizamani. Unaongelea mambo ya zones wakati sasa hivi mamlaka yanapelekwa mikoani. Usilolijua ni usiku wa giza. Unasema Dar ilijitosheleza kwa kila kitu. Upo wizara gani wewe??? Au ndo nyie mnasikia vitu bila kuvijua mnaanza kusambaza
 
Hata Lisu alipoambiwa ukweli kwamba anasaliti nchi kwa kututisha tutashitakiwa MIGA alichukia sana.
Kawaida mnufaika hawezi kufurahi kuona maslahi yake yapo shakani,yaweza kuwa aligusa maslahi yako mahali fulani,ama kwakutokutenda haki ama kwa kutaka habari zifike kwa wote,ama kwa kutaka kwake uwepo wa democrasia yakweli na uzalendo halisi na sii ule wa maslahi.
 
Kukurupuka kwa Hayati Magufuli katika azma ya kuhamia Dodoma Ilikuwa sahihi na kimsingi huko nyuma alikosekana kiongozi mkuu wa nchi mwenye utashi thabiti wa kutekeleza mipango iliyokuwa makabatini tangu enzi za Nyerere.

Bila ya Hayati Magufuli kuwakia kwenye gia katika kuhamisha makao makuu, bado wazo la kuhamia Dodoma lisingefanikiwa kwa visingizio vingi tu. Ikumbukwe kuwa CDA ilikuwa ni kichaka tu cha kuchotea pesa za Serikali bila kufanya walichotakiwa kufanya.
 
Kuna haja ya ku define object ya kuhamisha makao makuu kwa mazingira ya sasa na kutazama ile ya zamani. Je ni kweli kuna ulazima kwa sasa kwa kuzingatia gharama yake na kuwa tuna mahitaji muhimu ya kijamii ambayo hatujaweza kufulfil kama shule, zahanati, barabara na vitu vingine vya kuchochea uchumi na ajira kwa wananchi. Si vizuri kulitazama tu kuwa ni uamuzi ulifanyika bali ni vizuri analysis ya kiuchumi na kijamii ikafanyika.
 
Tunafahamu kwamba kuna watu mna chuki ya dhati kabisa naHayati kutokana na sababu mnazozijua nyinyi,lakini hii tabia ya kutaka kulazimisha kila alilofanya lionekane baya mbele ya watu wote,haki ya nani inawawafanya muonekane MATAHIRA !!
 
Unajua ni mwaka gani Serikali ilitangaza kuwa Dodoma ni makao makuu ya nchi?unajua hata kabla ya uamuzi huu tayari ofisi ya Waziri Mkuu na baadhi ya wizara zilishahamia Dodoma?
 
Kuhamia Dodoma kuna faida zake.
Kwa mujibu wa theory ya center peripheral development, kuhamia Dodoma kutaleta impact ya maendeleo kwa mikoa yote ya pembezone. Easy tu, we angalia sehemu yeyote inayoanzishwa Wilaya mpya, jinsi maendeleo yanavyokuja kwa haraka. Kwa hiyo halikadhalika establishment ya Dodoma itapelekea mikoa inayozunguka kupata uambukizo wa maendeleo.

Sababu ya kwamba kuna maendeleo ya sayansi na teknolojia hivyo hamna umuhimu wa watu kuja Dar halina ukweli. Bado kuna sababu nyingi za watu kwenda makao makuu Kama inavyoonekana mpaka sasa. Lakini vilevile viongozi wa serikali wanawajibu wa kutembelea mikoa mingine, Kwa hiyo sasa itakuwa ni rahisi zaidi. Dsm imezidiwa na movement za watu toka Tz nzima, matokeo yake mji ulisimama. Na study zilishafanyika zikaonyesha hasara ya congestation Dsm ni kubwa sana.

Lakini kuna wachumi wanaoamini serikali kuwa na miradi Kama hiyo inasisimua uchumi
 
Back
Top Bottom