‘Maamuzi ya CCM yanarudisha imani kwa wananchi’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

‘Maamuzi ya CCM yanarudisha imani kwa wananchi’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kibunda, Aug 6, 2011.

 1. k

  kibunda JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mwana JF,

  Nape amezidi kusasibu kuwa zoezi la kujivua gamba linarudisha imani ya wananchi kwa CCM.

  [h=2]‘Maamuzi ya CCM yanarudisha imani kwa wananchi’[/h]Thursday, 04 August 2011 19:55 newsroom
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  NA BASHIR NKOROMO
  HATUA ya kuwataka watuhumiwa wa ufisadi wapime na kuchukua uamuzi wa kuondoka katika vikao vya maamuzi ya CCM, kutakifanya Chama kuaminiwa zaidi na wananchi. Hayo yalisemwa jana mjini Dar es Salaam na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipokuwa akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Africa Media Group, inayomiliki vyombo kadhaa vya habari, kikiwemo kituo cha Televisheni cha Chanel Ten. Alisema, maamuzi ya CCM yanalenga zaidi maslahi ya nchi na wananchi wake na si maslahi ya mtu mmoja mmoja. Alisema, kutokana na misingi iliyowekwa na waasisi wake, CCM bado ina kila sababu ya kuendelea kuongoza nchi kwa kutekeleza yale yote ambayo yamo ndani ya Ilani ya Chama hicho.
  Nape alisema, mazingira yaliyokuwapo ndani ya Chama hivi sasa, yamekilazimu kufanya mabadiliko ili kukabiliana na changamoto mbali mbali. Alisema, mabadiliko hayo ambayo yalipitisha maamuzi zaidi ya 20, ni miongoni mwa mengi ambayo CCM imekuwa ikiyafanya tangu wakati wa TANU na hivyo watu wasichukue muda mwingi kuyashangaa bali washiriki katika kuyaenzi kwa kufanya utekelezaji. Hata hivyo, alikiri kuwa mabadiliko hayo yanaweza kuwaathiri baadhi ya watu, lakini hilo halitakuwa jambo la ajabu kwa sababu mabadiliko yoyote yanapotokea, wapo watakaoathirika katika kipindi kifupi, lakini wakafaidika kwa muda mrefu. "Siwezi kusema hakuna watakaoathiriwa na mabadiliko haya, wale waliokuwa wananufaika na mfumo holela uliokuwa unawapa mwanya kufanya mambo kwa manufaa yao hata kama yanaathiri taifa, lazima wataguna na kujaribu kufanya sarakasi za kupinga mabadiliko haya," alisema Nape. Alisema kutokana na sababu hizo, ndio maana zimetokea changamoto za hapa na pale katika mapokeo ya mabadiliko yaliyofanywa na CCM, ikiwemo baadhi kujaribu kujitokeza na kusema hadharani kwamba mabadiliko haya hayana maana.
  Nape aliwataka Watanzania na hasa vyombo vya habari, kuacha kuyafanyia kazi maneno ya mitaani, hasa yanayokihusu Chama cha Mapinduzi. Alisema CCM inaendeshwa kwa vikao na hata wanahabari wanapaswa kuripoti kile kilichozungumzwa ndani ya vikao.
  Alisema milango ipo wazi kwa kila mwenye hoja mbadala inayohusu maamuzi yanayofanyika hivi sasa. Ziara hiyo ya kutembelea vyombo vya habari, ni mwendelezo wa ziara za Mwenezi huyo alizoanza kuzifanya mwezi uliopita.
  Source: Uhuru Newspaper 4/8/2011
   
 2. afroPianist

  afroPianist Member

  #2
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "HATUA ya kuwataka watuhumiwa wa ufisadi wapime na kuchukua uamuzi wa kuondoka katika vikao vya maamuzi ya CCM, kutakifanya Chama kuaminiwa zaidi na wananchi."...
  Hivi Nape na mabosi wako waliolewa dozi kubwa za madaraka, mnatafakari kabla ya kupika hizo propaganda zenu kweli? Kusema "hatua ya kuwataka watuhumiwa wa ufisadi wapime", kimsingi sio maamuzi bali ni pendekezo, uamuzi ni kuchukua hatua na si kuiongelea. Na tena, ni wananchi gani hao ambao wamerudisha imani yao kwa CCM kwa "maamuzi" hayo? Na kwanini? Hii ni hoja butu kama kisu cha plastiki.

  Huwa ninakerwa sana na siasa za kipuuzi za CCM lakini zaidi huwa nahisi kutukanwa kama Mtanzania, hasa hawa jamaa wanavyothibitisha kila siku ni jinsi gani wanawachukulia watanzania kutokuwa na akili ya kupambanua mambo kiasi hicho!!!

  Imani na wananchi kwa CCM itarudi pale watoto wao masikini watapata uhakika wa elimu bora inayowawezesha kuishi katika ulimwengu wa kisasa wenye changamoto lukuki, huduma bora za afya hasa vijijini, uwezeshwaji katika kilimo na masoko bora yenye maslahi kwa wakulima, ajira kwa vijana walio wengi, mafao bora kwa wastaafu (rejea malalamiko ya wazee wastaafu EAC na Gen.Sarukikya) na hatimaye uwezo wa serikali ya CCM kuhakikisha upatikanaji endelevu wa nishati ya umeme, uthabiti wa vyombo vya ulinzi na usalama na ulindwaji mahsusi wa rasilimali za taifa kwa faida na manufaa ya watanzania wote.

  KAMA CCM MNADHANI WATANZANIA WOTE HAWANA AKILI BASI NYIE NDIO HASA MLIO WAPUMBAVU WA KUTUPWA!
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kama maneno yangekuwa utajiri Nape angekuwa bilionea.
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ni Vizuri Kujipa moyo maana kila Mtanzania anatambua CCM inawaogopa wezi ndio maana inawaomba wajitoe ha ha ha
   
 5. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ikifika 2015 ndio watajua kama watanzania imani wanayo au hawana,
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kumbe wananchi wenyewe ni uhuru na mzalendo, hapo sawa.
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nape na CCM waonekana kuzika vichwa vyao kwenye mchanga na hivyo kuanza kujiridhisha ya kwamba wamejificha vilivyo na kwamba hakuna hata mwananchi mmoja anayekumbuka madhambi yao ya ufisadi tena.

  Hilo nalo ni santuri nzuri pia ya mtu kujipa moyo mwenyewe kama mwizi gizani; wenzetu endeleeni hivo hivo huenda mkono wa binadamu ukadondoka nanyi mkauokota ifikapo 2015.
   
 8. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunasubiri Nape aende Arusha akafanye mkutano wa hadhara kisha akabidhiwe kadi za madiwani waliomaliza muda wao, kisha awape kadi za CCM.
   
 9. Nyota Ndogo

  Nyota Ndogo Senior Member

  #9
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  siyo kweli kwamba wananchi wote ni majuha.
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  hahahaaaaaaaumensaidia kuisogeza saum yangu
   
Loading...