MWIBA WA KATANI
Member
- Feb 26, 2012
- 39
- 42
leo kulikuwa na press Conference CUF na haya ndiyo yaliyojiri
MAAZIMIO YA KIKAO CHA BARAZA KUU LA UONGOZI
LA TAIFA KILICHOFANYIKA SHABAN HAMIS MLOO
MJINI DAR ES SALAAM TAREHE 14-15 Julai, 2012.
MAAZIMIO YA KIKAO CHA BARAZA KUU LA UONGOZI
LA TAIFA KILICHOFANYIKA SHABAN HAMIS MLOO
MJINI DAR ES SALAAM TAREHE 14-15 Julai, 2012.
S/N | JINA | NAFASI |
1 | Katani A.Katani | M/kiti |
2 | Yusuph K. Makame | M/Mwenyekiti |
3 | Khalifa A. Ali | Katibu |
4 | Thomas D.C. Malima | Naibu Katibu |
5 | Sonia Magongo | Mjumbe |
6 | Bonifasia Mapunda | Mjumbe |
7 | Kuruthumu Mchuchuli | Mjumbe |
8 | Said Maulid | Mjumbe |
9 | Ashura Mustapha | Mjumbe |
10 | Hamidu Bobali | Mjumbe |
11 | Ahmed Mudhihir | Mjumbe |
12 | Shomvi R Issa | Mjumbe |
13 | Faustin Khalfan | Mjumbe |
14 | Suleiman S. Abdallah | Mjumbe |
15 | Biubwa M. Mselem | Mjumbe |
14 | Pavu J. Abdallah | Mjumbe |
15 | Gora J. Hamis | Mjumbe |
16 | Hafidh A. Hafidh | Mjumbe |
17 | Ayoub Y. Khamis | Mjumbe |
15. Sera za kukusanya mapato zimejikita katika kodi za vinywaji na sigara. Sentensi moja inaniudhi kuisikia katika bajeti kila mwaka nayo ni Ushuru wa Cigar unabaki kuwa asilimia 30. Hivi cigar ngapi zinazovutwa Tanzania mpaka zistahiki kuwa ndani ya hotuba ya bajeti kila mwaka! Bajeti haizungumzii kabisa hatua zinazochukuliwa kuhakikisha sekta ya madini inachangia vya kutosha mapato ya serikali. 16. Katika kukabiliana na upungufu wa umeme serikali iliahidi kuchukua hatua kadhaa za kukabiliana na upungufu huu, ikiwemo kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 100 Dar es Salaam na ule wa megawati 60 Mwanza. Katika bajeti ya mwaka huu bado inaeleza Serikali ilisaini Mkataba wa mkopo wa Euro milioni 61 na Benki ya HSBC. Mkopo huu umeelekezwa kugharamia ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa megawati 60 Nyakato Mwanza. Bajeti tano mfululizo zimekuwa zinaeleza utekelezaji wa mradi huu. Mpaka sasa haujakamilika. Fedha zinazotengwa kila mwaka kukamilisha ufuaji wa umeme, Nyakato Mwanza zinakwenda wapi? Hali ya umeme bado ni tatizo kubwa nchini mbali na mwaka 2008 kutengwa 1.7 trilioni kama mfuko wa kichocheo cha kufufua uchumi (stimulus package) utekelezaji wake hauelezwi uliyeyukia wapi na fedha hizo zilizotengwa zimekwenda wapi! Serikali ya CCM, imeshindwa kutatua tatizo hili na kuisababishia nchi kupata hasara kubwa kwa kudhoofisha uchumi wa nchi. Hali hiyo imezorotesha uzalishaji viwandani na bidhaa zimepanda bei na kusababisha ukali wa maisha kwa watanzania, huduma za mahospitalini, katika sekta ya elimu, upatikanaji wa maji, KUPOROMOKA KWA SHILINGI na mengi mengineyo. CUF tunaamini bila ya umeme wa uhakika nchi haiwezi kupata maendeleo. 17. Serikali pia iliahidi kuweka mazingira mazuri ya kuongezeka kwa ajira. Mpaka sasa tatizo la ukosefu wa ajira ni kubwa mno na halielekei kutatuliwa. Katika nchi yenye nguvukazi ya zaidi ya watu milioni 22, walioajiriwa katika sekta rasmi ya viwanda ni watu 115000 tu. 18. Tatizo kubwa la bajeti yetu ni kuwa matumizi ya serikali hayatekelezi bajeti ya maendeleo iliyopitishwa na bunge. Matumizi ya miradi ya maendeleo ya mwaka wa fedha 2011/12 yatakuwa chini kwa shilingi bilioni 600 ukilinganisha na bajeti iliyopitishwa na Bunge. Baadhi ya sekta, matumizi halisi ya maendeleo ni chini ya asilimia 50 ya fedha zilizoidhinishwa. 19. Bajeti ya Maendeleo ya 2012/13 ni ndogo. Matumizi yote ya serikali yameongezeka toka shilingi trilioni 13.1 na kufikia shilingi trilioni 15.1 bajeti ya maendeleo imepunguzwa toka shilingi trilioni 4.9 mwaka 2011/12 na kufikia shilingi trilioni 4.5 mwaka 2012/13. Bajeti ya Maendeleo mwaka 2011/12 ilikuwa asilimia 36.4 ya matumizi yote ya serikali. Matumizi halisi ya bajeti ya maendeleo katika mwaka 2011/12 yatakuwa asilimia 33.3. Mwaka 2012/13 Bajeti ya Maendeleo ni asilimia 30 ya bajeti yote. Matumizi ya kawaida yameongezwa kwa asilimia 23.2 na bajeti ya maendeleo imepunguzwa kwa asilimia 8.1. Ukizingatia mfumko wa bei matumizi halisi ya bajeti ya maendeleo yatapungua mwaka 2012/13 ukilinganisha na mwaka 2011/12. Ili kuweka msukumo katika ukuaji wa uchumi bajeti ya maendeleo iwe alau asilimia 40. 20. Matumizi ya kawaida yanakua kwa kasi kubwa kwa sababu ya kuongeza gharama za utawala kama vile kuanzisha wilaya na mikoa mipya, safari nyingi za nje za Rais na viongozi wengine wa serikali, ukubwa wa Baraza la Mawaziri, posho za semina na makongamano. Hatua za maksudi zinahitajiwa kuchukuliwa kubana matumizi ya utawala. 21. Baraza kuu limeshtushwa na hali ya MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA UMMA kama ilivyoainishwa na taarifa iliotolewa na Msimamizi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Serikali Kuu, halmashauri mbalimbali nchini na mashirika ya umma, mabilioni ya shilingi ya fedha za walipa kodi wanyonge wa Tanzania zimetafunwa na watendaji wachache bila hatua stahiki kuchukuliwa dhidi yao. Baraza Kuu linaitaka Serikali ya CCM na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kuchukua hatua za kuwakamata wahusika wote waliotajwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Matumizi ya Rasilimali za mafuta, gesi, madini 22. Kuhusu matumizi ya Rasilimali za mafuta, gesi, madini ya uranium na madini mengine nchini, Baraza kuu linaitaka serikali kuweka utaratibu mzuri wa mchakato wa matumizi ya rasilimali hizi ili ziweze kuwanufaisha watanzania wenyewe kwani uzoefu inaonyesha kuwa nchi nyingi dunia zimeingia katika matatizo makubwa kutokana na ufisadi mkubwa wa watu wachache waliohodhi rasilimali hizo kwa maslahi yao. 23. Baraza Kuu la linatoa wito kwa Watanzania wote, pale Tume ya Kukusanya Maoni itapopita kwenye Wilaya zao, kutoa Maoni juu ya sehemu ya Mapato yanayopatikana toka kwenye mauzo ya Mali ya Asili kama vile gesi, dhahabu na madini mengine yagawiwe kwa Wananchi moja kwa moja ili yaweze kupunguza makali ya maisha na kuleta ulinzi shirikishi wa Rasilimali za Nchi na mali ya Asili ya Nchi yetu katika kukuza na kuimarisha dhana ya Utawala Bora. Mpasuko wa kisiasa ndani ya serikali ya CCM 24. Kuhusu mpasuko wa kisiasa ndani ya serikali ya CCM unaathiri na kuiyumbisha nchi na ustawi wa maisha ya watanzania kwa kiasi kikubwa kutokana na makundi makubwa ya nani awe mgombea urais kupitia chama hicho mwaka 2015. Jukumu la msingi la chama kinachounda serikali inayounda kufahamu kuwa nchi yetu inahitaji mabadiliko. Baraza Kuu linatoa wito kwa Watanzania kuzinduka na kufahamu kuwa nchi yetu inahitaji mabadiliko. CUF na viongozi wake wako tayari kuwaongoza Watanzania kuelekea katika mabadiliko wanayoyataka. CCM imeshindwa kuiongoza Tanzania. Na tujiandae kuishughulikia kikamilifu mwaka 2014/15 ili CUF iweze kuunda serikali makini itakayoweza kuweka mipango thabiti ya kiuchumi na maendeleo ya Taifa yetu. Kuhusu suala la Vitambulisho vya Mnzanzibar Mkaazi ZAIN ID 25. Baraza Kuu la Uongozi Taifa linaipongeza Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar juu ya maamuzi yaliyofanywa na Baraza la Wawakilishi kuhusu kushghulikia suala la Vitambulisho vya mzanzibari mkaazi ZAN-ID. Baraza Kuu linawaomba Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuona haja ya kutatua tatizo hili la Vitambulisho vya Mzanzibar Mkazi ili kuendeleza Ummoja uliopatikana kwa siku za Karibuni. Kuhusu suala la Sensa 26. Baraza kuu linaitaka serikali kudhibiti utoaji wa Takwimu ili kuepusha migongano isiyo ya lazima ndani ya Nchi. Baraza kuu linaona kuwa mgogoro uliopo sasa baina ya Waislamu na serikali katika suala la Sensa unatokana na serikali kutodhibiti utoaji wa takwimu za idadi ya watu kwa taasisi zisizohusika. Baraza Kuu limesikitishwa na namna serikali imelishughulikia tatizo ikiwemo vyombo vya serikali kutoa takwimu potovu na kuwa na dodoso la sensa linalohesabu nyumba za ibada bila kuhesabu waumini wa madhehebu husika. Linatoa wito kwa Rais Kikwete kukutana na viongozi wa dini zote kuwasikiliza hoja zao na kutafuta maridhiano kuhusu dodoso la dini katika sensa kwani ikiwa sehemu ya jamii itahamasishwa na kususia sensa, zoezi hili lenye gharama kubwa halitafanikiwa na nchi itakuwa na takwimu zisizo sahihi. Msimamo wa Chama katika mchakato wa kutoa Maoni ya Wananchi kuhusu uandikaji wa Katiba Mpya ya Jamuhuri Muungano 27. Baraza Kuu limewapongeza Viongozi wa Chama kwa jitihada zilizofanyika za kudai Katiba Mpya na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi na kufanikiwa kuishinikiza Serikali kuanzisha mchakato wa kukusanya Maoni ya wananchi juu mabadiliko ya Katiba mpya. Sera ya CUF ni kuwa na Muungano wa Serikali tatu. Sera hiyo imezingatia ukweli kwamba muundo Mpya wa Muungano ndio unaoweza kutoa ufumbuzi wa kudumu kwa changamoto (Kero) za muda mrefu za muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali mbili. Serikali ya Zanzibar iwe na mamlaka kamili ya mambo yake kuhusu Zanzibar. Ikiwemo uamuzi wa mwisho kwa matumizi ya mali asili (Mafuta, gesi na Madini) na matumizi ya kiuchumi ya bahari. 28. Baraza kuu limeona ni vizuri Serikali ya Muungano ihusike na mambo ya jumla ambayo wananchi wa Serikali mbili zinazounda Muungano watakubaliana. Hata hivyo kwa kuwa Muungano sio wa vyama na umekuwepo kabla ya kuungana kwa TANU na ASP1977, na kwa kuheshimu demokrasia ya wananchi wa pande zote mbili (Tanganyika na Zanzibar) waliofanya Muungano uwepo mwaka 1964, CUF- Chama Cha Wananchi kinasisitiza kuwa Tume isikilize na kuyaheshimu maoni ya Wananchi na isiyachakachue. 29. CUF- Chama cha Wananchi tunawahimiza wanachama na wananchi kwa ujumla wao kutoa maoni yao kwa UHURU ili kufanikisha jambo hili kwa mustakabali wa Nchi yetu. Baraza Kuu limesisitiza kusimamia na kuheshimu Sera ya Chama ya kutaka Muundo wa Serikali tatu ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwepo na Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano. Baraza kuu linawaomba Watanzania kushiriki kutoa Maoni yatakayowezesha kuandikwa Katiba Bora ikayotujengea Tanzania Tuitakayo. Kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi 30. Baraza Kuu linaitaka Serikali kuanzisha Mchakato wa kupata Tume Huru ya Uchaguzi sambamba na Mchakato wa ukusanyaji wa Maoni ya Katiba ili Uchaguzi wa 2015 uweze kufanyika chini ya Tume itayokubaliwa na Watanzania wote ili kuipa muda Tume hiyo kuweza kupitia Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Kuhusu suala la Haki ya Kumiliki Ardhi 31. Baraza Kuu la uongozi linatoa wito kwa serikali kuwamilikisha Watanzania ardhi yao hasa ukizingatia mchakato wa soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki na wimbi la kutafuta na kupora ardhi linalofanywa na nchi zenye fedha lakini zinaagiza chakula toka nje. Katiba mpya iwape Watanzania haki ya kumiliki ardhi yao. Mwisho; Baraza Kuu la Uongozi Taifa linawatakia watanzania wote ushiriki mwema katika utoaji wa Maoni yatakayowezesha kupatikana kwa Katiba Mpya. Imetolewa na Prof.Ibrahim Lipumba Mwenyekiti CUF Taifa
HAKI SAWA KWA WOTE