Kunguru wa Manzese
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 12,709
- 18,059
1-huna uhakika na kula na una elfu moja pekee ulionayo unaamua kunywa viroba. 2-huna kitanda na unaamua kuoa hayo pia ni maamuzi magumu. 3-huna uwezo wa kumlisha mkeo na unampa ujauzito ni maamuzi magumu. 4-shule haina walimu unampeleka mwanao pia ni maamuzi magumu. 5-daladala imejaa mpaka mlangoni na unaamua kupanda ni maamuzi magumu. 6-unalipwa laki 2 unamuhonga binti laki moja hayo ni maamuzi magumu. 7-kama utasoma hapa na ukashindwa kuandika maamuzi magumu unayoyajua utakuwa una maamuzi magumu mno