johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,961
- 141,956
Katika awamu iliyopita ilijengeka dhana kwamba kwa kitendo cha kujiuzulu uwaziri mkuu Lowassa alikuwa amefanya maamuzi magumu. Wapo waliodai kuwa Lowassa ni Waziri Mkuu wa kwanza kujiuzulu kwa hiyari hivyo wakamwita Mzee wa maamuzi magumu. Mimi binafsi niliuchukulia uamuzi ule kama jambo la kawaida kabisa katika kuonyesha uwajibikaji. Ila niwe mkweli katika awamu hii ya 5 chini ya Rais Magufuli nayashuhudia maamuzi magumu yakifikiwa na kutekelezwa na lililonifurahisha zaidi ni yale maandamano yaliyoratibiwa ughaibuni yalivyosambaratishwa. Nilimsikia Rais akiliambia taifa kuwa maandamano yale ni haramu na ole wake atakayethubutu kutia miguu yake barabarani kuandamana. Na jana tukashuhudia nchi ikiwa shwari na leo jamii nzima ya watanzania wakiwemo Chadema wamemkana Mange Kimambi. Mange amebakia mpweke akilia na kusaga meno huko America......haamini kilichotokea. Hayo ndio maamuzi magumu ukisema hapana lazima ionekane kuwa ni hapana hakuna kuchekacheka. Ahsante!