kiwalanikwagude
Member
- Jun 8, 2011
- 52
- 19
Akizungumza katika mahojiano na Radio Safari ya mjini Mtwara hivi karibuni Nape amesema serikali ya Rais Jakaya Kikwete ndiyo pekee katika nchi hii iliyokwisha kutoa maamuzi magumu kuliko serikali zote zilizopita.
Nape amenukuliwa akisema...." uamuzi mgumu wa kwanza uliotolewa na serikali ya awamu ya nne ni kwa yeye Lowassa kulazimishwa kujiuzulu, kuvunjwa Baraza la Mawaziri, kuwafungulia kesi kina Mramba na Yona, kuivunja kamati kuu ya CCM na sekretarieti, Ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma na Ujenzi wa shule za kata".