Maamuzi magumu tu

Haiwezi kubaki salama hata kidogo.... Lowassa ana zaidi ya kura millioni 8 mkononi kupitia wale vijana wa 4u na makundi mbalimbali walioenda kumshawishi....
Akhsante Mkuu, hiki ndo nilichotaka kusikia, JE PLAN B NI NNI ENDAPO ATAKATWA JINA?
 
Kuna mambo watu hamuelewi ccm imechokwa swala c nani emepitishwa
 
Yeye gamba limeshika mpaka mifupa, ukilivua unakiua Chama. Ndio maana linawatesa maana wote sio magamba tu bali makongwe gamba mpaka kwenye mifupa ukivua unaua.
 
Hatuwezi kuwa na rais mwenye kashfa chafu hivyo...
 
Mnapo linganisha hali ya siasa ya mwaka 1995 na Mwaka 2015, usisahau miaka hiyo wewe ulikuwa unavaa nepi huku ukijikojolea na Mama yako akikuhangaikia kukusafisha!! kama unaakili vizuri utagundua ninacho manianisha!!! Lowassa hanampinzani!! hivyo awamu hii ni Lowassa
 
Tanzania tunamuhitaji Lowasa kama tunavyohitaji hewa ili tuishi,Lowasa ni Mkombozi wetu
 

Mi nashauri mseme 'Tuamke ccm sio Watanzania..', msiaminishe watu kuwa Lowassa anapendwa na Watanzania, No ni kikundi ndani ya ccm.
 
Haiwezi kubaki salama hata kidogo.... Lowassa ana zaidi ya kura millioni 8 mkononi kupitia wale vijana wa 4u na makundi mbalimbali walioenda kumshawishi....

Hii ni mbinu ya UTEKEKAJI NYARA wa kisiasa. Kama CCM watatoa hiyo ransom basi itakuwa sio utamaduni mzuri wa kisiasa katika mustakabali wa nchi. Fisadi lo lote litatokea liteke nyara na kutishia 'msiponiteua basi naonadoka na milioni nane za vijana". Sio utamaduni mzuri wa kushabikia kama tunataka kujenga taifa la amani leo, kizazi cha kesho na cha keshokutwa, na mtondogoo. Njaa zetu za leo zisituharibie mustakabali wa taifa.
 
uchambuzi yakinifu, big up japo simkubali hata mmoja hapo
Umeona eh!
Hapa magamba yamepatikana, wampe asiye mwadilifu ili kushinda na baadae chama kife au wampe mwadilifu hata wakishindwa lakini chama kibaki imara.
"wengine walipaswa kutangaza nia ya kwenda jela lakini wanatangaza nia kwenda ikulu" - Prof. Lipumba

 
NSSF DAMU

..........mbinu ya kutishiana ili hold 2005, saaiv haiwezi kufanya kazi tena, naamini mfumo upo imara kupambana na huyo anayetishia TANZANIA......
 
Last edited by a moderator:
Hakuna mtu aliyejua kuwa Ben Mkapa angekuwa raisi! Alikuwa hatajwi wala hajulikani. Jaji Augustino ni bora mara elfu ukilinganisha na Lawasa, ingawa safari hii Raisi bora atatoka chama cha upinzani!
 
Mambo ya chama kwanza yamepitwa na wakati,waangalie sisi wananch tunamtaka nani,sasa kama wao vimgozi watakaa chumbani then watuletee mtu wanaotaka wao kweli wajiandae kisaikolojia,kauli ya mbowe na slaa itatimia,
 
Lakini unatakiwa kukumbuka na kuelewa kuwa wananchi hawa unaowaona Leo si wale wa mwaka 2005 mwananchi wa Leo wanaelewa siasa ni nini, wanaelewa mchezo mchafu wa siasa. Hawataki kuchaguliwa rais. LOWASA ndiye chaguo la wananchi kinyume na hapo KILIO kwa CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…