Maambukizi mapya ya VVU yazidi kupungua nchini

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imesema maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) yamepungua kutoka watu 110,000 mwaka 2016/17 hadi kufikia 54,000 mwaka 2020/2021.

Hayo yamesema Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk Leonard Maboko, Jumanne Novemba 14, 2022 wakati akizungumzia maadhimisho ya siku ya Ukimwi yanayofanyika Desemba Mosi kila mwaka.

Dk Maboko amesema idadi ya vifo pia imepungua kutoka vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi 64,000 mwaka 2016/17 hadi kufikia vifo 29,000 mwaka 2020/21.

“Ndani ya wiki hiyo tutakuwa na eneo maalum tunaliita kijiji cha vijana. Kule tutakuwa na kijiji maalum kwa ajili kuendelea kupata taarifa na huduma kwa ajili ya vijana,”amesema.

Awali Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene amesema maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika mkoani Lindi katika uwanja wa michezo wa Ilulu mkoani humo.

Simbachawene amesema maadhimishio hayo yataanza Novemba 24, 2022 hadi Desemba Mosi mwaka huu, ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali zitakazofanyika ikiwemo maonyesho na huduma ya upimaji wa magonjwa mbali mbali.

Amesema kauli mbiu ya maonyesho hayo ni imarisha haki.

MWANANCHI
 
Kwa data za kupika. Ila hili Taifa!!!
Una uhakika hizi data ni za kupika? Unaujua mfumo wa kuchukua taarifa kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma vinavyofanya kazi? Watanzania lini mtaamini kazi za wataalamu wenu nyie? Kila kitu ni kukitoa kasoro tu. Haya basi leta wewe data zako zisizo za kupika.
 
Zanzibar hakuna na chin San kimaambukizi less than 3 %

Mbona wengi huko wanafirana
 
Unauhakika hizi data ni za kupika?Unaujua mfumo wa kuchukua taarifa kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma vinavyofanya kazi?Watanzania lini mtaamini kazi za wataalamu wenu nyie?Kila kitu ni kukitoa kasoro tu. Haya basi leta wewe data zako zisizo za kupika.
Acha janja janja mkuu !!!!
 
Back
Top Bottom