Maalm Seif adaiwa kuwatelekeza wafuasi wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalm Seif adaiwa kuwatelekeza wafuasi wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Jan 2, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amedaiwa kuwatelekeza wananchama wa chama hicho ambao waliathirika katika maandamano yaliyotokea mwaka 2001 kutokana na kumuunga mkono katika kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000. wanachama zaidi ya 30 walipoteza maisha na wengine walijeruhiwa na kubaki na ulemavu wa maisha ambapo inadaiwa chama ndicho kilipaswa kuwasaidia kupata haki zao. Wanachama wengine zaidi ya 2000 walikimbilia nje ya nchi kuomba hifadhi.

  Waathirika hao wa maandamano hususan waliopata ulemavu wa kudumu wametelekezwa ambapo sasa chama chini ya maalim seif kimeyaweka kando madai yake ya kutaka wanachama wake wafidiwe na serikali ya mapinduzi.

  pia imeelezwa kwamba kiongozi wengine wa CUF wanaojaribu kufuatilia na kukumbushia hoja ya kulipwa fidia waathirika hao wamekuwa wakipigwa vita kwa kuzushiwa tuhuma za kuchochea ubaguzi kati ya wananchi wa pemba na wale wa unguja.

  chanzo. Gazeti la Dira ya mtanzania leo Januari 2, 2012.

  Tujadili.
   
Loading...