General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,316
- 23,178
Maalim Seif katibu mkuu wa CUF, na mshindi wa urais Zanzibar hatuna imani nawe.
Wazanzibar tumekuamini na kuwa na wewe bega kwa bega lakini leo hii umetuacha, umetudharau, wazanzibar hawana maana tena kwako.
Seif ni wewe ambaye kwa kipindi kirefu umetuaminisha tukuunge mkono, umetuaminisha kuwa utakuwa mkombozi wetu, nasi bila ajizi tukaamini hivyo, tukawa begamoja nawe, tukakupa imani, tukakuunga mkono kwa kila Jambo lakini leo yote umesahau, umetukimbiaa.
Kwa miaka mingi tumekuunga mkono, umekuwa ukishinda kila chaguzi, uchaguzi uliopita ulituapia hutokubali kuchakachuliwa, ukasema safari hii utatuachia tufanye maamuzi wenyewe lakini umekuwa sivyo.
Seif mpaka sasa hujasema lolote kuhusu zanzibar yetu, umejificha na ccm, umekubali ulaghai wa ccm, umetuacha solemba wana wako.
Hakika dhambi hii popote utakappkwenda itakutafuna.
Ulitupa matumaini kwamba vikao vyenu vitaamua na kufanya maamuzi sahihi, maamuzi ambayo ww utakuwa rais wa zanzibar, lakini kila siku ni danadana na sarakasi nyingi, hakika seif umetuuza wana wako, umekimbia mitini, umesaliti harakati za kuikomboa Zanzibar yetu.
Zanzibar itapata mkombozi mwingine lakini sio wewe seif.
Seif wewe ni MSALITI.