Maalim Seif: Tunataka kiti cha Zanzibar UN kirudishwe

Kila siku Wazenj wanaleta hadithi mpya, ni heri moongano uishe waendelee na mambo yao.
 
Pasco, kama ZnZ wanajaribu kupatana na walioungana nao(Tanganyika) na wanakataa miaka nenda miaka rudi je unataka waanze vurugu kwenye kujiondoa au kukimbilia mataifa makubwa/wafadhili?? Ipi njia sahihi apo? Hicho unachoongea wewe ni nadharia na sio practically hata miaka 500 watadai na wenzao bara haitafanikiwa. Mi nadhani yupo sahihi Maalim baada ya ZnZ kuzinguliwa kwa muda sasa.
Sikujua kuwa Maalim Seif naye pia ni mtu wa kujifurahisha!. Kabla Zanzibar haijaomba hicho kiti chake kule UN, "first it has to exist"!. Katika medani za kimataifa, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar!, Zanzibar doesn't exist anymore so does Tanganyika!. Kimataifa nchi ni moja tuu Tanzania, na Zanzibar ni sehemu ya hiyo Tanzania!.

Ili Zanzibar iweze ku reclaim its lost glory, hatua ya kwanza sio kukimbilia kwa big brother na kuomba utambuliwe, bali ni kumwambia partner wako kuwa umemchoka, mvunje kwanza hiyo parneship yenu ya muungano, uwe huru, uwe una exist tena kama zamani, then unabisha hodi UN kwenyewe na sio kwa host wa UN!.

Hivyo ili kukipata kiti chenu, hatua ya kwanza ni kuuvunja muungano na kuirejesha jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Kama alivyoshauri Mzee Mwanakijiji pale juu, tumieni BLW, mamlaka hayo mnayo kupitia ile sheria yenu ya kura ya maoni!. Hamna haja ya kuiliza bara lolote, pigine kura ya maoni kuwauliza Wazanzibari kama wanautaka muungano kwa yes or no, watakaojibu no na kama no ndio itashinda, then BLW wanapitisha azimio na taratibu za kuuvunja muungano zinafuatia ikiwemo namna ya kugawana mali!.

Maalim ana bahati sana sasa hivi ni enzi za Dhaifu, ingekuwa ni enzi ya Mwalimu, na ni kweli ameuwasilisha huo huko wa kwanza kushughulikiwa ni Shein, angeulizwa tuu, "jee unataarifa kuhusu waraka huo?, jee ulitoa baraka zako?, kama jibu ni ndiyo, then Shein angetiwa kizuizini (nyumbani) kama Jumbe!, na Maalim angeambiwa ambaki huko huko, na kama hana tujisenti twa Uswiss twa kumsetiri,yule half brother wake Sultani wa Brunei, angaokoa jahazi kumsetiri kama wanavyoifadhili CUF and that would have been the end of the story!.
 
Mkuu mnyanyaswaji, kama ni kweli huu ndio mtazamo wa Zanzibar ndani ya muungano, inamaanisha Zanzibar inajiona kama jina lalo, yaani ni mnyanyaswaji!, ukishajua unanyanyaswa, husemi kuwa unananyaswa, uwezo wa kupinga kunyanyaswa huku unao lakini huutumii, then huo ni uthibitisho kuwa umeshakubali kunyanyasika na umeridhika na manyanyaso hayo ndio maana hufanyi kitu kuyazuia!, sasa hili la kwenda kumwambia jirani kuwa "usinione hivi, mwenzio
nanyanyasika", haikusaidii lolote zaidi ya kujifurahisha na kujifariji kuwa "hata majirani wanajua nanyanyaswa"!.

Zanzibar inao uwezo wa kutoka ndani ya muungano kwa heshima kupitia BLW, kama hawautumii uwezo walionao kutoka rasmi kwenye muungano kwa heshima, hili la kuendelea kulalamika na kunung'unikia vipembeni na vichochoroni haiwasaidikii kitu!, na msipoangalia, tutaendelea kuwatawaleni mpaka basi, na mkizidisha chokochoko, msidhanie sisi ndio tutatishika, tutakufunzeni adabu kwa kuwanyang'anya hicho kijiserikali zuga tulichowaachia kwa kuunda muungano thabiti wa serikali moja na kuifanya Zanzibar ni mkoa, hivyo kuifutilia mbali kabisa na wataoleta chokochoko, serikali, kupitia kile kikosi cha FFU cha jeshi lake la polisi kita wamwa...si wale wote watakaoleta fujo au fyoko fyoko ya aina yoyote, akiwemo huyo sharubu!.
 
Kama hata huyo kiongozi mkubwa kabisa hajuwi utaratibu wa kuingia UN, unatarajia nini kwa wananchi wa kawaida walio wengi. Seif hivi sasa ni kati wa wazenji wachache wanaofaidika na muungano huu uliopo hivi sasa. Kama kweli alidhani muungano uliopo haufai asingekubali kunfunga nao ndoa kwa chochote anachokifanya ni kuwa hadaa wazanzibar ambao wanania ya kweli ya kupata haki ndani ya muungano. Seif anajua fika Zazibar ikijitenga na muungano hana nafasi ya kuishi maisha anayoishi sasa kwa kuwa utawala utakuwa tofauti ya ulivyo hivi sasa na ataendelea kuwa mpizani.
 
Mkuu Nguruvi3, Zanzibar kuna vituko vya ajabu!, wengi wanadhani ni Maalim ndie autakaye sana urais wa Zanzibar, hawajui kinachotakiwa sio urais, kinachotakiwa ni kisiwa na kinatakiwa na wenyewe!.

Baadhi tuu ya vituko vya Zanzibar ni kama vifuatavyo!.
  • Kuna mmoja wa marais wao alikuwa ni Mmalawi!, huko Zanzibar alikuwa hana baba, mama, kaka ,dada wala ndugu yoyote, uzuri ni kwamba hakusahau kwao, hivyo wanawe, aliwasomesha kwao Malawi!.
  • Aliyeongoza Mapinduzi ni Mganda!
  • Kuna rais alikuwa na watoto two brothers, mmoja wa watoto akatunukiwa zawadi ya urais kama heshima tuu kumuenzi baba yake!. Kipindi cha miaka kumi ya urais wa kaka mtu kilipotimia, mdogo mtu akaomba urais, huko kwao wakamkemea kuwa wewe umeona rais anayemaliza ni kaka yako, toka ntoke, halafu na wewe unaomba, huu umekuwa usultani?!. Mdogo mtu akajibu kuwa kama kaka ameupata urais kama shukrani ya kumuenzi baba, mwenye atahiki haswa ya urais ule ni yeye, kwa sababu kaka mtu, sii mtoto wa aliyeenziwa, alikuwa ni mtoto tuu wa kufikia, mwanahalisi ni yeye, hivyo sasa ndio apewe yeye ili kumuenzi kihalali!.
  • Kuna Sultani mmoja, alimbaka mjakazi wa mkewe na kumpa ujauzito (kubaka mjakazi sio kosa kama ilivyokuwa kumuua mtumwa), ili kuisetiri aibu ya mwana sultani kwa kijakazi, mjakazi yule akaileshwa ozwa kwa ndoa ya mkeka pahala mpaka alipozaliwa mwana sultani, wengine wote hawamjua kuwa ni mwana sulani, ila kuna wachache wanaijua siri hiyo!, sasa mwana sultani anafanya juhudi za juu chini kuvikomboa viziwa hivyo mikononi mwa ukoloni wa Tanganyika ili avirejeshe kwa sultani!. Huko ndiko zinakotoka fedha za kundi kama Uamsho, wengi wakifikiri ni ukombozi, kumbe Mwarabu anataka kurudi!.
  • Na kuna rais mmoja alioa mpaka chuo cha 5, best wake alikuwa rais wa mchi tajiri ya mafuta, akamsaidia sana huyo rais na alipomaliza tuu term yake ya urais, akamsaidia mpaka mkewe!.
  • Juzi kwenye Shindano Bibi Bomba ya Clouds kulijitokeza Bibi kutoa Zenj, akajitambulisha kuwa yeye ndiye mke wa kwanza wa rais fulani wa Zanzibar na wamezaa nae mtoto wa kiume, mumewe alipopata mke wa Kiarabu, yeye aliachika na kutelekezwa na mwanae mpaka kesho!.
Visa, vijambo na vimambo vya Zenj viko tele, ila kwa leo naomba niishie hapa, Mtoto akililia wembe mpe.. na mkataa pema, pabaya panamwita!, tuharakishe tuwapatia wanachiotaka halafu subirieni hilo tifu!.

Ungetaja na majina ndo ingekuwa bomba..
nimewahi sikia kuna mmoja alikuwa sio rizki sijui kama kweli
 
Sikujua kuwa Maalim Seif naye pia ni mtu wa kujifurahisha!. Kabla Zanzibar haijaomba hicho kiti chake kule UN, "first it has to exist"!. Katika medani za kimataifa, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar!, Zanzibar doesn't exist anymore so does Tanganyika!. Kimataifa nchi ni moja tuu Tanzania, na Zanzibar ni sehemu ya hiyo Tanzania!.

Ili Zanzibar iweze ku reclaim its lost glory, hatua ya kwanza sio kukimbilia kwa big brother na kuomba utambuliwe, bali ni kumwambia partner wako kuwa umemchoka, mvunje kwanza hiyo parneship yenu ya muungano, uwe huru, uwe una exist tena kama zamani, then unabisha hodi UN kwenyewe na sio kwa host wa UN!.

Hivyo ili kukipata kiti chenu, hatua ya kwanza ni kuuvunja muungano na kuirejesha jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Kama alivyoshauri Mzee Mwanakijiji pale juu, tumieni BLW, mamlaka hayo mnayo kupitia ile sheria yenu ya kura ya maoni!. Hamna haja ya kuiliza bara lolote, pigine kura ya maoni kuwauliza Wazanzibari kama wanautaka muungano kwa yes or no, watakaojibu no na kama no ndio itashinda, then BLW wanapitisha azimio na taratibu za kuuvunja muungano zinafuatia ikiwemo namna ya kugawana mali!.

Maalim ana bahati sana sasa hivi ni enzi za Dhaifu, ingekuwa ni enzi ya Mwalimu, na ni kweli ameuwasilisha huo huko wa kwanza kushughulikiwa ni Shein, angeulizwa tuu, "jee unataarifa kuhusu waraka huo?, jee ulitoa baraka zako?, kama jibu ni ndiyo, then Shein angetiwa kizuizini (nyumbani) kama Jumbe!, na Maalim angeambiwa ambaki huko huko, na kama hana tujisenti twa Uswiss twa kumsetiri,yule half brother wake Sultani wa Brunei, angaokoa jahazi kumsetiri kama wanavyoifadhili CUF and that would have been the end of the story!.

Bado mmelela na mawazo yenu ya kidikteta... Yule Dikteta Nyerere angalikua hai hadi sasa, kwa taarifa yako angekuwa tayari amesalimu amri...Yameshinda Mubarak ,Gadhafi na wengineo ijekuwa yeye masikini wa Mungu.
 
Ungetaja na majina ndo ingekuwa bomba..
nimewahi sikia kuna mmoja alikuwa sio rizki sijui kama kweli
Mkuu The Boss, kwa vile hizi ni hearsay, kutaja majina ni kuwachafulia tuu watu majina yao!.
Hili la "si rizki" sikupata kulisikia, ila nilichopata kusikia, kuna mmoja alikuwa na ile tabia ya michezo ya "kizanzibari"!.
 
Pasco, I can't agree with you more!Thanks. Please, allow me to chip in senti sumuni.

Kama ni kweli Maalim atakuwa ameshindwa kuelewa jambo dogo sana. Farouk Karim na Ally Salehe wame-champion Zanzibar kujitoa Chama cha mpira FAT nyakati hizo. Jitihada zao za kujiunga na mashirika ya kimataifa kama FIFA zimegonga mwambwa kwa sababu alizoeleza Pasco hata pale TFF ilipowaunga mkono.

Falconer; Security council ina wanachama wa kudumu 5 (USA,Russia, China, France na UK). Halafu kuna 10 non-permanent members. Wenye kura ya turufu (Veto ni 5) sasa kama unachosema ni kweli Maalimu inabidi awaone wengine 4 maana wanaweza kupinga tu. Hoja yako! mhh

Mwanakijiji: Hakuna ugomvi na Zanzibar kwahiyo maalimu anatakiwa apeleke mswada kwanza BLW kutaka kura ya maoni au kukataa muungano kwa short kati kama ile ya katiba ya Zanzibar, kuondoa mafuta na gesi(Ahmed Rajab) n.k.
Lakini pia alitakiwa awatumie wabunge 50 wanaowakilisha Zanzibar Dodoma.
Zaidi ya hapo wapo wabunge kutoka BLW wanaoingia Dodoma.
Kinachoshangaza ni kuwa unaomba vipi kiti UN kabla hujawa na nchi?

Nadhani Ahmed Rajab anapata majibu ya akina nani wenye ajenda hii (Raia mwema) licha ya kuwatetea.

Baada ya serikali 3(Ahmed Rajab) kukosa majibu na mkataba kuonekana hauna majibu,kwanini wazanzibar wanahangaika sana? Kwanini wasivunje muungano kesho ili keshokutwa Maalim apite kwa Ban Kimoon akiwa na document za maombi.

Huwezi kuwa na kiti UN, ukawa na BLW, Rais, Mahakama halafu ukadai mkataba. Uhusu nini tena!
Seif ni mwanasiasa wa ajabu sana, wakati anachukua mafao treasury Dar es Salaam wakati huo huo anaomba kiti UN.

Maalimu Seif rudi Nyumbani uvunje muungano, acha kujificha nyuma ya serikali 3 au mkataba wewe na washirazi wenzako

Ha ha hah...Mnahangaika na mwiba wa roho mbaya...Sasa mashtaka yenu mpelekeeni mama Maria Nyerere labada yeye anaweza kuwasilisha kwa mumuwe.
 
Bado mmelela na mawazo yenu ya kidikteta... Yule Dikteta Nyerere angalikua hai hadi sasa, kwa taarifa yako angekuwa tayari amesalimu amri...Yameshinda Mubarak ,Gadhafi na wengineo ijekuwa yeye masikini wa Mungu.
Ama kweli, shukrani ya punda, mateke!, Nyerere ni mtu wa nyinyi kuthubutu kumuita Dikteta?!. Tena mumshukuru sana Nyerere bila yeye, hata hapo mlipofika, wengine msingefika na hata jiwe tuu la alama ya kaburi isingalikuwapo!.

Hivi huko Zanzibar, wewe unayajua yalipo makaburi ya halaiki ya wahanga wa mapinduzi?.
 
Mkuu Nguruvi3, Zanzibar kuna vituko vya ajabu!, wengi wanadhani ni Maalim ndie autakaye sana urais wa Zanzibar, hawajui kinachotakiwa sio urais, kinachotakiwa ni kisiwa na kinatakiwa na wenyewe!.

Baadhi tuu ya vituko vya Zanzibar ni kama vifuatavyo!.
  • Kuna mmoja wa marais wao alikuwa ni Mmalawi!, huko Zanzibar alikuwa hana baba, mama, kaka ,dada wala ndugu yoyote, uzuri ni kwamba hakusahau kwao, hivyo wanawe, aliwasomesha kwao Malawi!.
  • Aliyeongoza Mapinduzi ni Mganda!
  • Kuna rais alikuwa na watoto two brothers, mmoja wa watoto akatunukiwa zawadi ya urais kama heshima tuu kumuenzi baba yake!. Kipindi cha miaka kumi ya urais wa kaka mtu kilipotimia, mdogo mtu akaomba urais, huko kwao wakamkemea kuwa wewe umeona rais anayemaliza ni kaka yako, toka ntoke, halafu na wewe unaomba, huu umekuwa usultani?!. Mdogo mtu akajibu kuwa kama kaka ameupata urais kama shukrani ya kumuenzi baba, mwenye atahiki haswa ya urais ule ni yeye, kwa sababu kaka mtu, sii mtoto wa aliyeenziwa, alikuwa ni mtoto tuu wa kufikia, mwanahalisi ni yeye, hivyo sasa ndio apewe yeye ili kumuenzi kihalali!.
  • Kuna Sultani mmoja, alimbaka mjakazi wa mkewe na kumpa ujauzito (kubaka mjakazi sio kosa kama ilivyokuwa kumuua mtumwa), ili kuisetiri aibu ya mwana sultani kwa kijakazi, mjakazi yule akaileshwa ozwa kwa ndoa ya mkeka pahala mpaka alipozaliwa mwana sultani, wengine wote hawamjua kuwa ni mwana sulani, ila kuna wachache wanaijua siri hiyo!, sasa mwana sultani anafanya juhudi za juu chini kuvikomboa viziwa hivyo mikononi mwa ukoloni wa Tanganyika ili avirejeshe kwa sultani!. Huko ndiko zinakotoka fedha za kundi kama Uamsho, wengi wakifikiri ni ukombozi, kumbe Mwarabu anataka kurudi!.
  • Na kuna rais mmoja alioa mpaka chuo cha 5, best wake alikuwa rais wa mchi tajiri ya mafuta, akamsaidia sana huyo rais na alipomaliza tuu term yake ya urais, akamsaidia mpaka mkewe!.
  • Juzi kwenye Shindano Bibi Bomba ya Clouds kulijitokeza Bibi kutoa Zenj, akajitambulisha kuwa yeye ndiye mke wa kwanza wa rais fulani wa Zanzibar na wamezaa nae mtoto wa kiume, mumewe alipopata mke wa Kiarabu, yeye aliachika na kutelekezwa na mwanae mpaka kesho!.
Visa, vijambo na vimambo vya Zenj viko tele, ila kwa leo naomba niishie hapa, Mtoto akililia wembe mpe.. na mkataa pema, pabaya panamwita!, tuharakishe tuwapatia wanachiotaka halafu subirieni hilo tifu!.

Hapa tunaambiwa oh, Pasco mwanasheria ohh, Pasco mtaalamu, sasa naona kaishia kuzungumza mambo ya udaku... Kwa taarifa yenu , Zanzibar huru inakuja na mkependa msipinde hiyo juu yenu...Let znz go!
 
Ama kweli, shukrani ya punda, mateke!, Nyerere ni mtu wa nyinyi kuthubutu kumuita Dikteta?!. Tena mumshukuru sana Nyerere bila yeye, hata hapo mlipofika, wengine msingefika na hata jiwe tuu la alama ya kaburi isingalikuwapo!.

Hivi huko Zanzibar, wewe unayajua yalipo makaburi ya halaiki ya wahanga wa mapinduzi?.

Dikteta Nyerere ndio alioifisidi Zanzibar , bali ya yeye na choyo na roho mbaya yake Zanzibar asingalikua fukara . Mimi sijui yalipo makaburi ya wahanga wa Mapinduzi , laba unifahamishe wewe.
 
Mkuu Takashi, ni kwa kutojua hata makaburi ya wahanga wa mapinduzi, ndio maana nawaambia watu kama nyinyi mumshukuru sana Nyerere angalau mmeweza kuwepo!, vinginevyo hata kaburi la baba yako usingelijua lilipo, seze ungezaliwa?!.
 
Pasco,
Hakuna kitu hicho mzanzibari "kushukuru sana dikteta Nyerere" kwa lipi la maana alowafanyia? Kabla ya Muungano ,Zaanzibar ilikua na akiba yake ya kutosho na haikuwa na deni hata senti moja. Yenye ndio alikuja na huo ulaghai na uwongo wake wa kutaka Muungano. Kwanza alianza kuzitolea macho fedha ya Zanzibar , akataka ahamishiwe Tanganyika.
Alikua ana ajenda zake za kidini za kikatoliki. Lakini alizivisha koti la umoja wa waafrika...Nia yake haikuwa kamwe Muungano bali ni utawala wa kuifanya Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika. Tunamuomba MMungu ampe hukumu anayo stahili kwa madhila aliyo wafanyia na kuwanyima haki zao za msingi wazanzibari.
 
Mkuu The Boss, kwa vile hizi ni hearsay, kutaja majina ni kuwachafulia tuu watu majina yao!.
Hili la "si rizki" sikupata kulisikia, ila nilichopata kusikia, kuna mmoja alikuwa na ile tabia ya michezo ya "kizanzibari"!.

Ndo huyo alieoa saana?
 
Pasco,
Hakuna kitu hicho mzanzibari "kushukuru sana dikteta Nyerere" kwa lipi la maana alowafanyia? Kabla ya Muungano ,Zaanzibar ilikua na akiba yake ya kutosho na haikuwa na deni hata senti moja. Yenye ndio alikuja na huo ulaghai na uwongo wake wa kutaka Muungano. Kwanza alianza kuzitolea macho fedha ya Zanzibar , akataka ahamishiwe Tanganyika.
Alikua ana ajenda zake za kidini za kikatoliki. Lakini alizivisha koti la umoja wa waafrika...Nia yake haikuwa kamwe Muungano bali ni utawala wa kuifanya Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika. Tunamuomba MMungu ampe hukumu anayo stahili kwa madhila aliyo wafanyia na kuwanyima haki zao za msingi wazanzibari.
Mkuu Takashi, usizungumzie fedha za kwenye kijaluba, au hayo mafuta ya kwenye kinibu!, jee wajua baada ya mapinduzi Zanzibar ingekuwaje bila Nyerere?, nimegundua nataka kubishana na mtu anayejidhania ni Mzanzibari akijiaminisha kuna watu wanaitwa Wazanzibari!. Endelezeni tuu hizo choko choko kuuchokoa muungano, hatimaye mtakipata mnacho kitaka na tutakutana humu humu wakati wa majuto ni mjukuu!.
 
Maalim Seif anaweza kutumia kodi ya wananchi kwenda kufanya huu mzaha Marekani?

UN hakuna kiti cha Zanzibar wala kiti cha Tanganyika. Kuna kiti cha Tanzania. Kama Maalim Seif anataka kurudisha kiti cha Zanzibar UN process iko very clear:

1. Amrudishe Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na kutangaza rasmi kuwa Zanzibar haimtambui.

2. Awarudishe mawaziri wote toka Zanzibar walio kwenye baraza la JMT

3. Awaite nyumbani wabunge wa JMT wanaowakilisha Zanzibar

4. Apeleke muswada BLW ili Zanzibar itangaze rasmi kuwa ni dola kamili.

Na haya yote anaweza kufanya bila kupanda ndege na kwenda Marekani.
 
Ngoja nikapitie vifungu vya sheria ya ndoa nione vinasemaje watu wanapochoka ndoa Yao. Ntarudi baadae
 
Back
Top Bottom