Maalim Seif: Tunataka kiti cha Zanzibar UN kirudishwe

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar akihutubia wafuasi wa CUF visiwani Zanzibar kasema anapendekeza na kutaka pia kiti cha Zanzibar Katika umoja wa mataifa UN kirudishwe.

Kwa usemi huu ni dhahiri Zanzibar inataka kuwa dola huru na muungano kwisha habari yake.
Na Mwinyi Sadallah | 14th August 2012

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuna haja kwa Zanzibar kurejeshewa kiti chake katika Umoja wa Mataifa (UN).

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na viongozi wa wilaya na majimbo wa Chama cha Wananchi (CUF) katika ukumbi wa Benjamin Mkapa, kisiwani Pemba jana.

Alisema Zanzibar kabla ya Muungano ilikuwa nchi huru iliyokuwa na kiti chake UN na kuelezea haja ya kuwepo kwa mamlaka kamili ya Zanzibar ili iweze kurejesha kiti chake kwenye umoja huo.

Maalim Seif alisema hoja kubwa ambayo Wazanzibari wanatakiwa kujadili katika mchakato wa maoni ya Katiba mpya ni muundo na mfumo wa Muungano.

"Zanzibar tunayo Katiba yetu ya mwaka 1984 ambayo imejitosheleza kwa mambo yetu ya Zanzibar, lakini suala kubwa kwenye mabadiliko hayo kwetu sisi litakuwa ni la Muungano na hili haliwezi kuepukwa," alisema Maalim Seif.

Maalim Seif aliwataka wananchi kuangalia maslahi ya nchi yao kwanza katika mchakato wa kukusanya maoni ya mabadiliko ya katiba na kuacha tabia ya kutetea misimamo ya vyama badala ya maslahi ya nchi na wananchi wake.

"Katiba ya nchi ni mali ya wananchi siyo ya chama chochote, lakini najua kila chama kina katiba yake na hiyo ndiyo itabakia kuwa katiba na mwongozo wa chama husika, kwa hivyo ndugu zangu naomba tulifahamu hili na tuangalie maslahi ya nchi yetu kwanza," alisema Maalim na kupigiwa makofi na wanachama.

"Mimi najua wapo wanaotaka serikali moja, wengine mbili, tatu, nne, na muungano wa mkataba, lakini wengine wanataka waachiwe wapumue…Yote hayo ni maoni na kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake bila ya kulazimishwa, kwa hivyo wakati wenu ukifika nendeni mkatoe maoni hayo kwa uwazi," alisema Maalim Seif.

"Wakati wenu ukifika nendeni mkatoe maoni yenu kwa uwazi bila ya hofu hiyo ni haki yenu ya kikatiba," aliongeza.

Alisema serikali ya Tanzania tayari imepanga ifikapo Aprili 2014, Tanzania iwe na katiba mpya ambayo inatokana na matakwa ya wananchi wake wa pande mbili za Muungano huo.

Ingawa Maalim Seif hakufafanua kauli yake ya Zanzibar kuwa na kiti chake katika UN, lakini anamaanisha kwamba Zanzibar inapaswa kuwa na mamlaka yake kamili.

Kwa maana hiyo ikiwa Zanzibar itarejeshewa kiti chake katika UN hapatakuwepo na Muungano tena kwa kuwa itakuwa ni nchi kamili ambayo inatambuliwa na UN na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.

Tangu Tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya kuanza kazi hiyo, kumeibuka kikundi kinachofanya kampeni misikitini (Uamsho) kutaka Zanzibar kujitenga katika Muungano huku wengine wakitetea kuwepo kwa Muungano wa mkataba.

Vile vile, baadhi ya Wazanzibari wakiwemo mawaziri na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamesema kuwa kuna haja ya kuwa na Muungano wa mkataba kwa lengo la kumaliza kero zinazolalamikiwa.

Baadhi ya makada wa CCM waliotaka Muungano wa mkataba ni Waziri asiye na Wizara Maalum, Mansour Yusuf Himid na mmoja wa waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Nassoro Moyo.

Hata hivyo, baadhi ya makada wamewashambulia na kuwatisha wanachama wa chama hicho wanaotoa maoni tofauti na sera ya CCM ambayo ni muundo na mfumo wa serikali mbili.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, wiki iliyopita wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Jimbo lake la Kitope, alisema wanaopingana na sera ya CCM kuhusu muungano warejeshe kadi zao za uanachama badala ya kusubiri kufukuzwa.

Naye Mbunge wa Uzini (CCM), Dk. Mohammed Seif Khatib, Alhamisi iliyopita akizungumza na waaandishi wa habari mjini Dodoma akiwa na wabunge zaidi ya 30 kutoka Zanzibar alieleza kushangazwa na wanachama wanaotoa maoni ya kuvunja Muungano.

Khatib ambaye ni Mwenyekiti wa wabunge wa CCM Zanzibar, alisema chama hicho kinapaswa kuwachukulia hatua kwa maelezo kuwa walipata nyadhifa zao kwa kutumia ilani ya CCM inayoeleza wazi kuwa sera yake ni ya Muungano wa serikali mbili.

CHANZO: NIPASHE
 
Sura kamili ya Maalim inajidhiri. Safi sana Maalimu Seif kwa kueleza kilicho moyoni.
Kwa mantiki hiyo Maalimu anasema kuwa hoja ya serikali 3 au mkataba haina maana tena.
Afadhali Maalimu amesema wazi tofauti na alivyokuwa anajificha nyuma ya pazia.

Muungano sasa umefikia hatima yake, na tunashukuru kuachana kwa usalama.

LET ZNZ GO!
 
Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar akihutubia wafuasi wa CUF visiwani Zanzibar kasema anapendekeza na kutaka pia kiti cha Zanzibar Katika umoja wa mataifa UN kirudishwe.

Kwa usemi huu ni dhahiri Zanzibar inataka kuwa dola huru na muungano kwisha habari yake.
ROU, sorry I doubt this was said!.
 
Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar akihutubia wafuasi wa CUF visiwani Zanzibar kasema anapendekeza na kutaka pia kiti cha Zanzibar Katika umoja wa mataifa UN kirudishwe.

Kwa usemi huu ni dhahiri Zanzibar inataka kuwa dola huru na muungano kwisha habari yake.

R-O-U,

..kirudishwe na nani?

..SMZ wanapaswa kwenda UN na kudai kiti hicho.

..kama baraza la wawakilishi liliweza kuondoa mafuta ktk masuala ya muungano, sijui kwanini wanashindwa kupiga kura mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa yasiwe masuala ya muungano.
 
Mkuu sura halisi ya huyu Bwana haieleweki maana ni yeye aliyemchomea aliyekuwa Rais wa Zanzibar Aboud Jumbe kwa Mwalimu Nyerere baada ya kushirikiana na Waarabu kutaka kuuvunja Muungano, ndipo Jumbe alipovuliwa madaraka yote aliyokuwa nayo!!!
Sura yake inaeleweka vizuri tu ni ya "kinyonga". Ni mtu mnafiki mwenye uwezo wa kufanya chochote ili kupata Uongozi. Aogopwe kama 'Ukoma"
 
Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar akihutubia wafuasi wa CUF visiwani Zanzibar kasema anapendekeza na kutaka pia kiti cha Zanzibar Katika umoja wa mataifa UN kirudishwe.

Kwa usemi huu ni dhahiri Zanzibar inataka kuwa dola huru na muungano kwisha habari yake.

Mnafiki huyo
 
Wakati mpango huo ukiendelea, tunaomba tujulishwe mpaka wetu kati ya Zanzibar na Tanganyika uko wapi, ili mambo yakiharibika tu, kila nchi inachukua chake kwa amani.
 
Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar akihutubia wafuasi wa CUF visiwani Zanzibar kasema anapendekeza na kutaka pia kiti cha Zanzibar Katika umoja wa mataifa UN kirudishwe.

Kwa usemi huu ni dhahiri Zanzibar inataka kuwa dola huru na muungano kwisha habari yake.

Ngoja ngoja yaumiza matumbo...let them get what they want
 
R-O-U,

..kirudishwe na nani?

..SMZ wanapaswa kwenda UN na kudai kiti hicho.

..kama baraza la wawakilishi liliweza kuondoa mafuta ktk masuala ya muungano, sijui kwanini wanashindwa kupiga kura mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa yasiwe masuala ya muungano.

.

..

Huu muungano ushamfia mtu mkononi.
 
Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar akihutubia wafuasi wa CUF visiwani Zanzibar kasema anapendekeza na kutaka pia kiti cha Zanzibar Katika umoja wa mataifa UN kirudishwe.

Kwa usemi huu ni dhahiri Zanzibar inataka kuwa dola huru na muungano kwisha habari yake.

Kwasababu kunaonekana wazi nyufa kubwa zilizopo kati waunguja na wapemba hata ishia hapo atataka Pemba iwe na kiti chake UN. Huyu mzee ana uchu tu na madaraka ya uraisi anaitaka hiyo nafasi kwa udi na uvumba lakini ataisikia tu!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
napenda maada za kuvunjika kwa muungano yaani ingewezekana ziwe zinawekwa sticky thread nilivyouchoka huu muungano na kelele za wazanzibari kuonewa.. tuwaache waende kwa amani tumemakamilika kila kitu mbona tulipata uhuru bila wao ..
 
Nilisema tangu mwanzo kundi la Uamusho ni mkakati wa kwanza wa Maalim Seif sasa kajifunua wazi.
 
Back
Top Bottom