Maalim seif: Tume zingatieni maoni ya kweli

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,483
[h=1][/h]Written by Elbattawi // 06/04/2013 // Habari // 4 Comments

maalim-seif-564x272.jpg

KATIBU mkuu wa Chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amemshangaa Mwenyekiti wa Tume ya kuratibu Katiba mpya nchini Tanzania, Jaji Joseph Warioba kuhusu aina ya mapendekezo yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba mpya.
Amesema anamshangaa Mwenyekiti wa Tume hiyo kwa kuja na mapendekezo yake, na anawaona Wazanzibari kuwa na akili za kitoto, jambo ambalo wameshang’amua.
Maalim Seif alisema: “Tunamshangaa sana Jaji Warioba kwa kutugeuza Wazanzibari ‘danganya toto’ anatufanya sisi tuna-akili za kitoto…hizo serikali tatu ni nani hao waliyozitaka,” alihoji Maalim Seif.
Alisema maoni ya wananchi na viongozi wa Zanzibar, waliyoko madarakani na waliyostaafu (aliwataja kwa majina) yanatosha kuzingatiwa na Tume kuhusu aina gani ya mfumo wa Muungano wanaouhitaji Wazanzibari.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamo wa kwanza wa rais wa Zanzibar, alisema asilimia kubwa ya Wazanzibari, pamoja na viongozi wanaoitakia kheri Zanzibar, walitoa maoni ya kutaka Zanzibar, iwe na MAMLAKA yake kamili ya ndani na kimataifa.
Akionekana kuzumza kwa kukereka katika mkutano wa hadhara uliyofanyika leo jioni Mkwajuni, Kaskazini Unguja. Maalim Seif, alimueleza Warioba kuwa Zanzibar serikali tatu wala nne hawazitaki na kinachotakiwa ni kuzingatia maoni ya kweli yalitolewa na Wazanzibari na sio ‘danganya-toto’:
“Mhe Jaji Warioba…tunakwambia bila Zanzibar yenye MAMLAKA yake kamili ndani na kimataifa hatutakubali…kwa hivyo rudia maoni ya Wazanzibari,” alisisitiza Maalim Seif..
 
Mimi nasema yote hio ni heri tu ,maana kila wakifanya hivyo ndipo wanapoibua zaidi hasira kwa wananchi wa Zanzibar kwa hio sizani kuwa Warioba na tume yake ya Dodoma watakuwa na urafiki na wananchi wa Zanzibar nikuwachonga ukali na kujikoroga zaidi kwa kujionyesha ukoloni wao zidi ya Zanzibar.

Hakuna historia hata ya taifa moja nguvu ya wananchi kushinwa kwa kuwatumia ubabe bila ridhaa yao, kwa hio wacha ccm itawale na kuwapuza Wazanzibar wajuwe ikiondoka tu hata miaka mia basi wananchi wa Zanzibar hapo ndipo patakapokuwa patamu na hakuna urafiki tena.

Maana hivi sasa huo Muungano ni wakichama tu, baina ya ccm Bara na ccm Zanzibar ndio udugu wa Muungano lakini mbele ya Wazanzibar Muungano nisawa na maradhi ya ukoma au uharo wa Bata, hawautaki hata kuona wanataka ufe leo na hilo sio siri mbele ya Tanzania yote ndio ukaona kinacho fanywa ni Tanganyika ijitayo Tanzania inaikalia kibabe Zanzibar.
 
Kama muundo wa serikali tatu utakuwa ni matakwa ya wanzazibar basi maamuzi yao yataheshimiwa na si maamuzi ya watu wachache. Pia kama viongozi walioko madarakani na wale wastaafu wanahitaji Zanzibar yenye mamlaka kamili si wapitishe azimio la kujitenga sasa kinachowafanya kulalamika ni nii? Kama hiyo haitisho juzi walikuja kupokea vitambulisho vya taifa dsm, leo wanaanza kutoa maneno mengi wakati maamuzi ya Zanzibar huru wanayowao wenyewe.
 
jamuhuri ya watu wa zanzibar kwanza, jamuhuri ya tanganyika kwanza, muungano baadae na katiba yake.
 
Jamhuri ya watu wa z'br kwanza longolongo baadae.

Nurdin,

..mimi ni Mtanganyika na ninamuunga mkono Maalim Seif.

..tofauti yangu na Maalim ni pale anapotaka "muungano wa mkataba."

..sasa najiuliza kwanini Znz haitaki mamlaka kamili kama majirani zetu wengine, mfano Kenya, Uganda, DRC, au hata Rwanda?

..muungano mwingine wa aina yoyote ile, ikiwemo huo muungano wa mkataba, unahitaji kuwepo kwa hali ya KUAMINIANA kati ya nchi husika.

..sasa tuwe wakweli kwa nafsi zetu. Watanganyika na Wazanzibari hatuaminiani.

..Kwasababu hatuaminiani, ni bora tushirikiane kupitia jumuiya ya AFRIKA MASHARIKI ambapo wanachama wenzetu watatusaidia kupunguza hii minyukano ya moja kwa moja kati ya Watanganyika na Wazanzibari.

cc: Nonda, Mdondoaji, Kibunango, Zitto, Mwigulu Nchemba, Kakke, GHIBUU, Kadogoo
 
Last edited by a moderator:
mkuu njia rahisi ya kuvunja muungano ni kudai muungano wa mkataba. kudai kuvunja muungano ni uhaini

mkuu, mahusiano ya wazanzibar na watanganyika hayakuletwa na muungano yalikuwepo kabla na hata muungano ukivunjika kesho bado mahusiano yao yataendelea kwahiyo wasiwasi ni wako lakini mahusiano kati ya pande hizi ni unique na hata kama tutakuwa pamoja ndani ya east Africa lakini bado uhusiano wa pande hizi mbili utakuwa tofauti kabisa na nchi nyingine za east afrika. kwa kuwa wananchi wengi visiwani wanataka muungano wa mkataba kwenda kinyume nayo ni kuwadharau watu kwani nchi uongozwa kwa ridhaa za wananchi.
 
norbit,

..inategemea unatumia njia gani kuvunja muungano.

..zipo njia za kikatiba kuuvunja muungano, na kuja na aina mpya ya mashirikiano.

..mchakato huu wa katiba unaweza kutumika kuvunja muungano.

politiki,

..YES, mahusiano kati ya wa-Tanganyika na wa-Zanzibar yalikuwepo kabla hata ya muungano.

..naweza kusema kwamba mahusiano hayo yalikuwa mazuri sana.

..mahusiano hayo yanaingia nyongo pale tunapolazimisha muungano wa KIKATIBA.

..zaidi, ukiangalia hoja ya "muungano wa mkataba" utaona kwamba kila wanachokihitaji wa-ZNZ ktk "mkataba", wanaweza kukipata kupitia EAC.

..biashara, ardhi, uhamiaji, sarafu, ulinzi, yote yanapatikana ktk EAC.

..zaidi, EAC itaondosha ile minyukano na mikwaruzano ya moja kwa moja baina ya wa-Tanganyika na wa-Zanzibari. Minyukano hiyo, in the name of kero za muungano, inapoteza muda na rasilimali nyingi kuishughulikia.

..mwanzoni ilionekana kwamba wa-Znz wanataka serikali 3. wameunga mkono muungano wa mkataba baada ya kufanyika juhudi kubwa kuwaelimisha kuhusu faida zake.

..wa-ZNZ ni watu waelewa. tukiwafahamisha kwamba EAC is a lot better than mkataba, hawatashindwa kuelewa.

cc: Kibunango, GHIBUU, Nguruvi3, takashi
 
Nurdin,

..mimi ni Mtanganyika na ninamuunga mkono Maalim Seif.

..tofauti yangu na Maalim ni pale anapotaka "muungano wa mkataba."

..sasa najiuliza kwanini Znz haitaki mamlaka kamili kama majirani zetu wengine, mfano Kenya, Uganda, DRC, au hata Rwanda?

..muungano mwingine wa aina yoyote ile, ikiwemo huo muungano wa mkataba, unahitaji kuwepo kwa hali ya KUAMINIANA kati ya nchi husika.

..sasa tuwe wakweli kwa nafsi zetu. Watanganyika na Wazanzibari hatuaminiani.

..Kwasababu hatuaminiani, ni bora tushirikiane kupitia jumuiya ya AFRIKA MASHARIKI ambapo wanachama wenzetu watatusaidia kupunguza hii minyukano ya moja kwa moja kati ya Watanganyika na Wazanzibari.

cc: Nonda, Mdondoaji, Kibunango, Zitto, Mwigulu Nchemba, Kakke, GHIBUU, Kadogoo

Kwangu mimi ni simple and clear, Warioba aangaliae maoni ya wa znz nini walisema. Muda huu sio tena wa kuburuzana. Taifa hili limeelemewa hisia kali za kidini na sasa anataka kuengeza za u-znz na u-tngk. Nchi hii haitakalika , na watuulize sisi tumeyaona kwa macho huko ughaibuni.

Warioba asilazimishe watu kitu wasichokitaka... Atajuta majuto ya mjukuu.
 
Nurdin,

..mimi ni Mtanganyika na ninamuunga mkono Maalim Seif.

..tofauti yangu na Maalim ni pale anapotaka "muungano wa mkataba."

..sasa najiuliza kwanini Znz haitaki mamlaka kamili kama majirani zetu wengine, mfano Kenya, Uganda, DRC, au hata Rwanda?

..muungano mwingine wa aina yoyote ile, ikiwemo huo muungano wa mkataba, unahitaji kuwepo kwa hali ya KUAMINIANA kati ya nchi husika.

..sasa tuwe wakweli kwa nafsi zetu. Watanganyika na Wazanzibari hatuaminiani.

..Kwasababu hatuaminiani, ni bora tushirikiane kupitia jumuiya ya AFRIKA MASHARIKI ambapo wanachama wenzetu watatusaidia kupunguza hii minyukano ya moja kwa moja kati ya Watanganyika na Wazanzibari.

cc: Nonda, Mdondoaji, Kibunango, Zitto, Mwigulu Nchemba, Kakke, GHIBUU, Kadogoo
Mkuu JokaKuu, huyu maana si ndiye mwasisi wa serikali 3 chini ya CUF, mbona anagoma tena? Anachotaka ni Tanganyika isikilize maoni ya ZNZ na si kinyume chake. Kama anaona hakubaliani basi asahwishi wznz wagome, period.

Leo vuai kawaambi hadharani kuwa hayo mafuta kama yapo heri kama hakuna imekula kwao.
Kasema wanafaidika sana na muungano na yale tunayoyasema kila siku ameyataja.

Hapa ni suala la kupasua mbao hawa watu waende zao. We don't need them. they need us.
 
Vuai yupi unaemzungumzia ? Yule kibaraka, kipenzi chenu?
 
Nurdin,

..mimi ni Mtanganyika na ninamuunga mkono Maalim Seif.

..tofauti yangu na Maalim ni pale anapotaka "muungano wa mkataba."

..sasa najiuliza kwanini Znz haitaki mamlaka kamili kama majirani zetu wengine, mfano Kenya, Uganda, DRC, au hata Rwanda?

..muungano mwingine wa aina yoyote ile, ikiwemo huo muungano wa mkataba, unahitaji kuwepo kwa hali ya KUAMINIANA kati ya nchi husika.

..sasa tuwe wakweli kwa nafsi zetu. Watanganyika na Wazanzibari hatuaminiani.

..Kwasababu hatuaminiani, ni bora tushirikiane kupitia jumuiya ya AFRIKA MASHARIKI ambapo wanachama wenzetu watatusaidia kupunguza hii minyukano ya moja kwa moja kati ya Watanganyika na Wazanzibari.

cc: Nonda, Mdondoaji, Kibunango, Zitto, Mwigulu Nchemba, Kakke, GHIBUU, Kadogoo
Ndugu yangu , hayo ni maoni ya wazanzibari wanataka mkataba, muungango 3,2,1 kwa maslahi ya Zanzibar hayana. so kama wewe mtanganyika unaona kuwa muungano wa mkataba ni kuzunguka mbuyu badala yake tuvunje kabisa, hayo yatakuwa ni maoni yako, ni vyema ungetafuta wenzio ukaungwa mkono hoja yako ili iweze kufika kunako husika kama vile wazanzibari walivyotoa maoni yao. ukiangalia maoni yenu huko Tanganyika hayakuingia sana katika muungano kwa vile nyinyi ndio wafaidikani wakuu wa muungano, munaona kama suala hili haliwagusi. bado wazanzibari wanahitaji kusikilizwa maoni yao kama sharia ya uundaji wa katiba mpya inavyosema, ni muhimu kusikilizwa kama kweli hii katiba ya watanzania wote, kama ni ya ccm katiba hii yatapuuzwa kwani sera ya chama chao serikali mbili.
 
Back
Top Bottom