Zanzibar 2020 Maalim Seif: Mimi ni muumini wa Muungano

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
6,276
12,336
Amesema hayo wakati akihojiwa na BBC Swahili amesema "Mimi Ni muumini kabisa wa Muungano ila uwe wa haki"

======

Akizungumza na BBC idhaa ya Kiswahili, Mgombea wa Urais visiwani Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, ameanisha baadhi ya mambo anayoyapa kipaumbele katika sera zake ikiwa ni pamoja na kuondoa umasikini miongoni mwa Wazanzibari pamoja na kuondoa tatizo la kutokuwa na ajira.

Maalim Seif pia amesema moja katika mambo ambayo anapanga kuwafanyia Wazanzibari ni kudumisha umoja, kwamba atawaunganisha kwa kuhakikisha wanaepuka ubaguzi wa aina yoyote ile.

Akizungumzia kuhusu suala la Muungano, Seif amesema:

"Mimi ni muumini mkubwa wa Muungano. Mimi nataka Muungano wa Haki; Muungano wa Usawa."

"Mambo yote yanaamuliwa Dodoma. Hata yale mambo ambayo ni ya Zanzibar peke yeke, haiwezi kuamua."
 
Hizi ni fikra zako. Una haki ya maoni ila aliyoyasema ndio anayoyaamini. Tatizo wapinzani wake wanampa sifa mbaya ili aonekane haupendi muungano. Haupendi mfumo wa sasa wa muungano unaoikandamiza Zanzibar. Hiyo ndio hali halisi.

Maalim sio muumini wa Muungano ; he has never been such;

Ukichagua Maaalim jua Umevunja Muungano.

Ukichagua Lisu jua umeleta mabeberu.
 
Amesema hayo wakati akihojiwa na BBC Swahili amesema "Mimi Ni muumini kabisa wa Muungano ila uwe wa haki"

======

Akizungumza na BBC idhaa ya Kiswahili, Mgombea wa Urais visiwani Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, ameanisha baadhi ya mambo anayoyapa kipaumbele katika sera zake ikiwa ni pamoja na kuondoa umasikini miongoni mwa Wazanzibari pamoja na kuondoa tatizo la kutokuwa na ajira.

Maalim Seif pia amesema moja katika mambo ambayo anapanga kuwafanyia Wazanzibari ni kudumisha umoja, kwamba atawaunganisha kwa kuhakikisha wanaepuka ubaguzi wa aina yoyote ile.

Akizungumzia kuhusu suala la Muungano, Seif amesema:

"Mimi ni muumini mkubwa wa Muungano. Mimi nataka Muungano wa Haki; Muungano wa Usawa."

"Mambo yote yanaamuliwa Dodoma. Hata yale mambo ambayo ni ya Zanzibar peke yeke, haiwezi kuamua."
Mpaka sasa Maalim na Tundu Antiphas Lissu wameshashinda.

Hoja kuu ya Ccm kuwa Maalim na Lissu watavunja Muungano imezikwa rasmi.

Hongereni sana Chadema na ACT.

Dj leta manenoooooooo!!!!
 
Maalim sio muumini wa Muungano ; he has never been such;

Ukichagua Maaalim jua Umevunja Muungano.

Ukichagua Lisu jua umeleta mabeberu.
Binafsi nawakaribisha mabeberu kwa mikono yote miwili, hivi huu upuuzi wenu wakukosa hoja na kushikilia kisentensi kimoja tu kisicho na mashiko yoyote hamuoni kama kinawaaibisha nyie na mgombea wenu,? Shame on you.
 
Maaalim nae ni pimbi...kuna mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano...

Kuna mambo znz wanayaamua wenyewe maana si ya Muungano... Sasa akija kusema kila kitu kinaamuliwa Dodoma anakua anajitekenya mwenyewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom