Maalim Seif: Mimi ndio Rais wenu

Maalim Seif: Mimi ndio Rais wenu

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Posts
16,697
Reaction score
9,589
KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad amewaasa wananchi wa Unguja na Pemba kutambua kuwa chama hicho ndicho kilichopata ushindi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 na wasihadaike na propaganda za viongozi wa CCM. Anaandika Jabir Idrissa, Zanzibar (endelea).

Maalim Seif ambaye ndiye aliyegombea urais kupitia CUF amesema kwamba yeye ndiye anayestahili kutangazwa mshindi na atatangazwa wakati wowote mgogoro ukishamalizika.

Alitoa kauli hiyo leo alipokuwa akihutubia viongozi wa chama hicho ambao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na kamati tendaji za wilaya za Unguja kwenye ukumbi wa Majid Store, Mombasa mjini hapa.

Amesema mazungumzo yake na Jakaya Kikwete kabla ya kuondoka madarakani yalikuwa mazuri na yaliyokuwa ya kina na kufikiwa makubaliano huku akimuachi kuamilisha kazi iliyobakia rais mpya, Dk. John Magufuli.

Amesema kwamba dunia nzima inajua ukweli wa kwamba Maalim Seif Shariff Hamad wa Chama cha Wananchi ameshinda uchaguzi mkuu wa Zanzibar isipokuwa CCM ikaamua kupindua ukweli huo kwa maslahi binafsi ya kung?ang?ania madaraka.

Maalim Seif amesema wana CUF na Wzanzibari wote bila ya kujali tofauti zao za kisiasa na nyinginezo watulie wakiamini kuwa watatangaziwa rais wao halali na si mwingine baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kukamilisha uhakiki wa matokeo ya mwisho ya majimbo 23 yaliyobakia wakati Mwenyekiti wa tume hiyo, Jecha Salim Jecha ?alipokurupuka na kutangaza peke yake kuyafuta matokeo ya uchaguzi wote.?

Mimi sina wasiwasi ninajihesabu kama Rais wa Zanzibar ninayesubiri kuitwa na kuapishwa, na sasa nimo katika matayarisho ya kuunda serikali ili nikiapishwa tu nisipoteze tena muda wa kufikiria kuunda serikali,? amesema katika kikao cha kwanza na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho.

Amesema Tume wanachokifanya ni kuchelewesh tu utaratibu wa kukamilisha kazi yao ya wajibu kwa mujibu wa Katiba ya Zanibar, 1984, lakini akasema, nina uhakika, wataikamilisha na kutangaza matokeo yaliyo halali kwa sababu kila mtu anayajua kwa sasa.?

Wakati akisema hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi inayofanya kazi za Mwenyekiti wa chama hicho baada ya kujiuzulu kwa Profesa Ibrahim Lipumba, amesema CUF haina fikra hata chembe za kuwepo uchaguzi mpya kwa Zanzibar baada ya ule wa Oktoba 25 ambao Wazanibari walishuhudiwa wakimpa ridhaa Maalim Seif Shariff Hmad ya kuongoza nchi yao.

Twaha Taslima ambaye ni mwanasheria na wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania amesema Baraza Kuu la Uongozi la Taifa (BKUT) la CUF limeridhia kwamba chama hicho kimeshinda uchaguzi na limelaani njama za kumtangaza mtu asiyechaguliwa na wananchi.

Taslima amesema njama hizo zimeongozwa na Mwenyekiti Jecha akitumiwa na wanasiasa wahafidhina wa Chama Cha Mapinduzi wanaoshindwa kuheshimu misingi ya demokrasia kwa kutaka kung'ang'ania madaraka.

Bado alisema Baraza lina imani kuwa Tume itakamilisha kazi ya kuhakiki matokeo ya majimbo 23 yaliyobakia na kumtangaza mshindi wa uchaguzi huo aliyechaguliwa kihalali ambaye atakuwa ni Maalim Seif Shariff Hamad.

Wakati huohuo, mwanasheria gwiji nchini aliyeongoza timu iliyoandika Katiba ya Zanzibar mwaka 1980, Aboubakar Khamis Bakary ametangaza rasmi kuwa mawaziri wote katika serikali ya Dk. Ali Mohamed Shein wanaotoka CUF wameshakabidhi ofisi na gari serikalini.

Aboubakar ambaye alikuwa akiongoza wizara ya Katiba na Sheria, amesema wametekeleza hatua hiyo ya kisheria baada ya uongozi wa serikali ya Dk. Shein kumaliza muda wake rasmi ilipofika Novemba 2 mwaka huu.

Alisema kwa mujibu wa Kif. 28 cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Rais Dk. Shein alikamilisha muhula wa miaka mitano tarehe hiyo na mtu yeyote anayetafsiri vinginevyo katiba, anafaa kuitwa ?mbumbumbu wa sheria.

Mimi ni mwanasheria na mtaalamu hasa wa masuala ya katiba na hakuna wa kunidanganya. Wanaosema rais Dk. Shein anaongoza kihalali eti kwa kuzingatia kifungu cha 28, hawajui wanachokifanya, au wanapotosha makusudi ukweli ili kukidhi matakwa yao binafsi, amesema Aboubakar.

Amemsihi Dk. Shein azingatie katiba badala ya kusikiliza viongozi wa CCM ambao alisema wanatafuta njia ya kutengeneza mgogoro mwingine wa kisiasa Zanzibar baada ya kushindwa uchaguzi.

Lazima tufike mahali tuithamini demokrasia tuliyoamua kuijenga. Haikubaliki kuwasumbua wananchi wa Zanzibar kwa uchaguzi ambao baadhi yetu wanasiasa hatuko tayari kupoteza madaraka, hii si sahihi hata kidogo, amesema gwiji huyo wa sheria aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya Zanzibar baada ya Zanzibar kupata katiba yake ya kwanza tangu ile iliyovunjwa na Mzee Abeid Amani Karume mwaka 1964 yalipofanyika mapinduzi.

Oktoba 28 mchana, ndipo Mwenyekiti wa ZEC, Jecha alitangaza kwenye eneo ambalo halijaelezwa vizuri ni wapi, kuufuta uchaguzi wote wakati mwenyewe alishatangaza matokeo ya urais katika majimbo 31, kati ya 54 ya Zanzibar. Wakati huo tayari fomu za matokeo yote zilikuwa zimebandikwa kwenye kuta za vituo vya uchaguzi nchini kote.

Alichukua hatua hiyo inayoelezwa kama ya shinikizo kutoka uongozi wa juu wa CCM, siku mbili baada ya Maalim Seif kutangazia ulimwengu kuwa alikuwa na kura asilimi 52.87 dhidi ya 47.13 za Dk. Shein, na kutaka Tume isicheleweshe matokeo.

Pia alimsihi Dk. Shein kukubali matokeo hayo na kutoa ushirikiano kama alivyokubali yeye katika uchaguzi mkuu wa 2010. Alisema atashirikiana na CCM kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kama Katiba inavyoelekeza.


Chanzo:
Mzalendo net.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wananchi kisiwani Pemba watembee kifua mbele kwa sababu ni suala la muda tu kabla hajatangazwa kuwa mshindi wa Urais wa Zanzibar na kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya nane.

Maalim Seif alisema hayo alipokuwa akihutubia katika mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya viongozi wa Wilaya, Majimbo na Matawi kisiwani Pemba uliofanyika katika ofisi za uchaguzi za CUF Pemba zilizopo Ngoma Hazingwa, Chakechake.

Alisema wanachofanya viongozi wa CCM hivi sasa ni kuchelewesha muda tu, lakini kwa kuwa wananchi wa Zanzibar wamemchagua yeye kuwa Rais na Dunia nzima inafahamu hilo, hatimaye watamwita wenyewe na kumuapisha kuwa Rais wa Zanzibar.

?Wananchi wa Pemba kuleni mshibe, laleni bila ya hofu na tembeeni kifua mbele, hawana njia lazima watakubali maamuzi ya wananchi wa Zanzibar walionichagua niwe Rais wao?, alisema Maalim Seif.

Hata hivyo, Maalim Seif alisema jambo la muhimu kwa wananchi wa Pemba na Wazanzibari wote wasikubali kuchokozeka baada ya hali iliyojitokeza, kwa sababu kuna watu lazima watafanya vitimbi kwa tama ya kuvuruga amani ya nchi.

Alieleza kuwa Chama cha Wananchi CUF kupitia Baraza Kuu la Uongozi tayari kimeamua kwamba hakuna suala la uchaguzi wa Zanzibar kurejewa kwa sababu wananchi wameshafanya maamuzi ya kidemokrasia katika uchaguzi uliokuwa wa huru na haki.

Alisema hakuna haja ya kupoteza muda na kuendeleza propaganda zisizokuwa na msingi kinachopaswa kufanyika hivi sasa ni Tume ya Uchaguzi Zanzibar kumalizia kazi yake na kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 25.
?Wache wapoteze muda wataniapisha tu, na wajue muda wangu wa Urais utaanza siku nitakapo apishwa kwa mujibu wa Katiba?, alisema.

Katibu Mkuu huyo wa CUF ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alisema jambo linalowatia kiwewe CCM na kutoa visingizio kuhusiana na kura za Pemba ni kutokana na fedha nyingi walizotumia kwa tamaa ya kupata majimbo kadhaa.

Alisema kwamba CCM wamesahau kuwa miaka yote hawapati majimbo kisiwani Pemba na hivyo si ajabu katika uchaguzi wa mwaka huu kukosa viti vyote vya Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.

Maalim Seif alisema hata huyo mgombea Urais wa Zanzibar kupitia ADC, Hamad Rashid Mohammed ambaye alitegemewa na CCM kupunguza kura za Maalim Seif kisiwani Pemba hakufua dafu na yeye mwenyewe (Hamad Rashid) aliambulia kura 495 tu.

?Viongozi wa CCM maskini walimdanganya sana Dk. Shein kuwa watapata viti Pemba na kura za kutosha za Rais, wametumia fedha nyingi katika uchaguzi huu, lakini walisahau hali halisi ya Pemba na sasa wanahangaika?, alisema Katibu Mkuu wa CUF.

Alieleza kuwa zipo taarifa kuwa kiasi cha shilingi milioni 70 zilitumiwa na CCM katika jimbo moja tu la Mtambwe, jimbo ambalo katika chaguzi zote zilizofanyika chama hicho hakijawahi kupata kura zaidi ya asilimia tano.

Maalim Seif aliwapongeza mawakala wa CUF katika majimbo yote 54 ya Zanzibar kwa namna walivyo jidhatiti kulinda kura za chama chao na hatimaye kukiwezesha kupata ushindi mkubwa ambao haujapata kutokea Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazuri alisema uchaguzi mkuu uliofanyika kisiwani Pemba mwaka huu ni mfano mzuri wa uchaguzi uliokuwa huru na wa haki katika nchi nzima.

Alisema kuwa wale wanaodai kuwa kura zimezidi kisiwani humo ni waongo wanaotapa tapa kwasababu kuna watu waliojiandikishwa zaidi ya 20, 000 hawakupiga kura na waliojitokeza kwenda kupiga kura ni 119,000.

Mazrui alisema CCM wamepatwa na maumivu makubwa kisiwani Pemba kutokana na matumizi makubwa ya fedha waliyoyafanya kwa tamaa ya kupata majimbo manne, lakini wananchi wa Pemba hawakuona sababu ya kukichagua chama hicho.
 
Zanzibar. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema yuko tayari kukamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka, kama kitendo chake cha kujitangazia ushindi ni kosa.

Maalim Seif alikuwa akizungumza na viongozi wa majimbo, makatibu wa matawi, wajumbe wa mkutano mkuu, wajumbe wa kamati za utendaji za ngazi zote na watendaji wa chama hicho.

Alisema haoni hatua yake ya kuitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imtangaze kuwa mshindi haina matatizo kwa kuwa ana uhakika kuwa ndiye aliyeshinda kwenye uchaguzi.- -----

?Nilichosema ni ZEC initangaze kwa kuwa nilishinda uchaguzi. Je, hapo kuna ubaya gani ati? Nishitakini basi, nasema niko tayari, nishtakini. Nitakuja mahakamani kujitetea, mnamtisha nani! Mnamtisha nani hapa?? alihoji.

Maalim Seif aliwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), akichuana vikali na mgombea wa CCM, Dk Mohamed Shein.

Hadi sasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) haijamtangaza mshindi na badala yake imefuta matokeo ya kura za nafasi hiyo pamoja na za uchaguzi wa wawakilishi, ikisema uchaguzi utarudiwa tena ndani ya siku 30.

Hata hivyo, CUF imepinga ikitaka ZEC imtangaze mshindi kwa madai kuwa chama hicho ndicho kilichoibuka na ushindi.

Jana, Maalim Seif, ambaye ameshagombea urais wa Zanzibar mara tano, alirudia wito wake wa kuitaka ZEC imtangaze kuwa mshindi ili aapishwe na kuanza kazi, ikidai anataka kuanza kuijenga upya Zanzibar. Pia alisisitiza msimamo wake wa kushirikiana na CCM katika utawala wake kwa kuwa Katiba ya Zanzibar inaelekeza chama kinachoshinda kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

?Sijui wenzetu wanachohofia ni nini na mara hii sisi (CUF) tumeshinda viti 27 na wao idadi hiyo hiyo ya viti 27 vya Baraza la Wawakilishi, tutakuwa na idadi sawa kwa sawa ya mawaziri tuongoze nchi pamoja,? alisema Maalim Seif.

Kiongozi huyo wa CUF alihoji sababu za Rais Shein kutokubali kushindwa akihoji anaona ubaya gani kuridhia.

?Tukae pamoja tuunde Serikali akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais au kama hataki CCM wamteue mtu yoyote tuongoze nchi. Mbona mimi niliridhia kuwa Makamu wa Kwanza?? alihoji.

Maalim Seif alisema hakuna namna yoyote ya kupindua uamuzi wa wananchi walioufanya kupitia masanduku ya kura.

Alisema wanachokifanya ZEC ni kuchelewesha kukamilisha uhakiki wa kura kwa majimbo 14 yaliyobakia na kumtangaza mshindi wa urais, na hivyo kuishauri ZEC kukamilisha kazi ili serikali mpya ianze kufanya kazi ya watumikia wananchi.

Alisema tayari dunia nzima wanamfahamu rais aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu uliopita, na kuwataka wanachama wa CUF kuacha kusikiliza kile alichokiita proganda za CCM zinazoeleza kurejewa kwa uchaguzi.

Akizungumzia madai ya ongezeko la kura katika kisiwa cha Pemba, Maalim Seif alisema hayo hayana ukweli kwani hakuna hata ?kituo kimoja kilichozidishwa wapiga kura 350 kama ZEC ilivyopanga, akisema vingine vilikuwa na wapigakura chini ya idadi hiyo.

Mapema akizungumza katika mkutano huo, mkurugenzi wa mipango na uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe alisema chama hicho kimepata ushindi mkubwa kwa nafasi za uwakilishi na udiwani.

Alisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 chama hicho kilipata wawakilishi wanne na madiwani saba kisiwani Unguja, lakini katika uchaguzi wa 2015 kimepata wawakilishi tisa na madiwani 15.

Kiongozi huyo alisema CCM imepoteza kata zote tatu za udiwani katika kisiwa cha Pemba na kukifanya chama hicho kushindwa kupata mjumbe katika Baraza la Wawakilishi, ubunge na udiwani.

Kabla ya mkutano huo, alielezea kauli ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la CUF kilichokutana chini ya mwenyekiti wake, Twaha Taslima, akisema kiliishauri ZEC kutengua uamuzi wa mwenyekiti wake, Jecha Salim Jecha wa kufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar, kwa vile hana mamlaka ya kikatiba na wala Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar hampi nguvu ya kufuta uchaguzi huo.

Jecha amekuwa akidaiwa kufanya uamuzi huo bila ya kushirikisha viongozi wenzake wa ZEC.

Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanatakiwa kutolewa siku tatu baada ya wananchi kupiga kura na yanaweza kucheleweshwa kwa siku tatu zaidi iwapo kutatokea matatizo katika kuhesabu kura.

Chanzo: Mwananchi
 
Maalim amesema yupo tayari kushitakiwa mahakamani kama ametenda kosa la kujitangazia matokeo mapema kabla ya zec.
 
Maalim amesema yupo tayari kushitakiwa mahakamani kama ametenda kosa la kujitangazia matokeo mapema kabla ya zec.
Seif ameitoa kali hiyo wapi?

Kama ni kweli ametoa kauli hiyo, CCM watumie mwanya huo kumfungulia mashitaka ili mkwamo upatiwe suluhisho kwa haraka.
 
Seif ameitoa kali hiyo wapi?

Kama ni kweli ametoa kauli hiyo, CCM watumie mwanya huo kumfungulia mashitaka ili mkwamo upatiwe suluhisho kwa haraka.
Jamaa anajiamini hajafanya kosa, ukitaka chanzo cha kauli yake Mwananchi Facebook page.
 
Last edited by a moderator:

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    20.2 KB · Views: 1,297
Wadau inasikitisha sana ku pretend tukafanya demokrasia wakati Chama tawala na serikali yake vikiwa vinang'ang'ania madaraka na kushindwa dhamini kura za wananchi. Huku ni kuwafanya wananchi wapumbafu na kuwafanyia maigizo ya demokrasia. Jamani kama zanzibar Cuf wameshinda wageni nchi. Hii ndio demokrasia. Msitumie ubabe kukandamiza haki. Hii inaleta hasira na matokeo yake umwagaji damu.
 
Japo wengine walitaka kuliahirisha hili tatizo ili lionekane ni la awamu ya tano lakini historia itasoma wazi palipokuwa na udhaifu!
 
Kukiwa bado kuna sintofahamu juu ya uchaguzi uliofutwa Zanzibar, Mgombea wa urais kupitia CUF Maalim Seif Hamad, amesema amekua akiandaa baraza la mawaziri ili mara tu akiapishwa aanze kuwatumikia wanzazibari.

Seif amesema hayo jana katika ofisi za CUF alipokua anaongea na wanachama wa chama hicho. Seif amesema katika baraza lake la mawaziri atawajumuisha na wana CCM kama ilivyoainishwa katika marekebisho ya katiba ya Zanzibar juu ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Amesema yy ndio mshindi halali na anachosubiri kuapishwa tu, Seif pia amewataka wanachama wake kupuuzia propaganda za wana CCM za marudio ya uchaguzi huo.

Source: The Citizen
 
twabonyeza kizenji,bonyeeee......😀😀
 
Ukawa nao waliishagawana vyeo, Mbowe PM, Mbatia H/Affairs...ndoto za mchana!
 
Japo wengine walitaka kuliahirisha hili tatizo ili lionekane ni la awamu ya tano lakini historia itasoma wazi palipokuwa na udhaifu!
Ili John naye ajitengenezee jina anapaswa kuutatua huu mgogoro haraka iwezekanavyo kwa kuiagiza tume imtangaze Maalim Seif kama ndo mshindi wa huo uchaguzi. Vinginevyo kitamdodea!!
 
Safi sana Seifu sio akina Lowassa na Mbowe wababaishaji tu.
 
Maalim kwa nn aogope kurudia Uchaguzi wakati wapiga kura ni wale wale kama walimpigia kura si watampigia tena? Maalim ni mvunja Muungano kwa Maslahi mapana ya Taifa letu tushirikieni kuilinda Znz kuangukia kwny Mikono ya Adui
 
Back
Top Bottom