MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,268
Waacheni waendelee na longo longo zao huku wakiparuana. Vyura hawawezi kumzuia tembo kunywa maji.
Wao wamebakiwa na cheap politics zinazokolezwa na spinning na siasa zilizopitwa na wakati za kutaka kujua ni nani msagaji au siyo msagaji.
CCM tumedhubutu, tumeweza na sasa tunatenda.
Makada tuko mikoani tunafanya kazi tuliyotumwa na wananchi kupitia kwenye sanduku la kura 2010.
Kwa urafi wa kutaka madaraka, wameshindwa hata kuwa kitu kimoja kwa manufaa ya wananchi.
Wapinzani hawako kwa ajiri ya kuwatumikia wananchi, wako kwa ajiri ya kujinufaisha wao na watu waliokaribu yao.
Hata wabunge wa viti maalum katika vyama vyao wamepatikana kutoka mifukoni mwa viongozi wao.
Nashangaa na mimi kuwa Seif halioni hilo.Waroho wa madaraka walimpiga shoka mtu anayetofautiana nao kiitikadi. Na wanajisifia kwa hili.
Na pia hao hao wanatumia dini kutugawa. Seif haoni.Waroho wa madaraka walimpiga shoka mtu anayetofautiana nao kiitikadi. Na wanajisifia kwa hili.
ULIBERALI aka UKAMERON ni dira ya CUF!! Maalimu Seif hivi wazanzibar wanajua ulivyomsaliti Aboud Jumbe wakati akidai serikali tatu? Hivi siyo weye uliiba ile Rasimu mezani na kumpelekea Nyerere?! na hadi leo Jumbe amepoteza popularity anachekelea sasa unavyodai madaraka/mamlaka kamili hadi ukaanzisha uasi zenj! unaoongoza hadi leo kwa jina la UAMSHO!! Wewe Maalim huna lolote zaidi ya UROHO hebu elezea baada ya kuingizwa "sebuleni"/"Barazani" mwa dola la majizi na kujishindia makombo ya majizi sasa umeufyata!! USHANFAHAMUEH!KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hammad amekirushia kombora Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kile alichodai kinapoteza mwelekeo kutokana na fujo nyingi zinazotokea wakati wa vikao vya Bunge. Alisema fujo hizo, ni wazi zinaonekana kusababishwa na uroho wa madaraka.
Maalim Seif alitoa kauli hiyo juzi jijini hapa, wakati wa kampeni za kumnadi mgombea nafasi ya udiwani wa Kata ya Eralai, John Bayo.
Alisema wakati CUF, ilipofanikiwa kuongoza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni chini ya uongozi wa Hammad Rashid Mohamed, kulikuwa na busara za hali ya juu katika uendeshaji wa vikao vyao.
Alisema kutokana na umoja na uaminifu ambao CUF ilikuwa nao, ndiyo ilimteua Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilbroad Slaa kuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni.
"Wakati CUF inaongoza Kambi ya Upinzani Bungeni, tulikuwa na umoja mno, tulishirikiana na vyama vyote vya upinzani na naibu wetu, alikuwa Dk. Slaa.
"Ila wao Chadema, walipopata wakaanza kusema wao ni wao, ndugu zangu ndio maana leo hii mnaona Bunge limekuwa la fujo utadhani soko, watu wanamwaga matusi kama cherehani, maadili ya Bunge yameachwa," alisema Hammad.
Alisema CUF ni chama chenye dira na kinachoona mbali, kwa sababu kimeundwa kwa lengo la kutetea maslahi ya wananchi wote na dira yao.
Kwa upande wake, Bayo akiomba kura alijikuta akiangua kilio mbele ya wananchi waliokuwa wakimsikiliza.
Bayo, ni moja ya madiwani waliotimuliwa CHADEMA kwa madai ya kupokea rushwa na kukisaliti chama hicho.
"Sijagusa hata senti kwa ajili ya kuwasaliti watu wangu, najua kitendo hicho kinakiuka maadili na kuwasaliti nyinyi mlionichagua.
Kwa hisani ya Mtanzania.
Mkuu hii ya leo kali yani thread umeanzisha wewe pia ukaona haitoshi utoe na comment yako kabisa ili uwe umeibikiri mwenyewe..
Walishasema CUF (ngoja nitype kwa herufi ndogo nisiwavimbishe vichwa hiki chama cha kijinga) cuf ni maalim sefu na maalim sefu ni cuf..cuf ni kampuni ya maalim sefu yaani ni mwenyekiti mtendaji pale kama r.mengi na ippKweli Nyani haioni ....le. Maalim Saif anaweza kumsema mtu au chama chochote kuwa kina uroho wa madaraka! Yeye tangu mfumo wa Vyama vingi ndo anagombea Urais wa Zanzibar na anashindwa lakini hawezi kumwachia mtu mwingine. Tangu CUF imeanzishwa yeye ni Katibu Mkuu mpaka leo. Amefunga ndoa na CCM na kuua chama kisa ni kupenda madaraka. Leo hii anasema CHADEMA ni waroho wa madaraka? Anahitaji maombi aweze
kujitambua.