Maalim Seif bado mgonjwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim Seif bado mgonjwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilimasera, May 9, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MAKAMU wa Rais wa Zanzibar, Seif Shariff Hamad, amejibu malalamiko mbalimbali ya wananchi dhidi yake, viongozi na Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuhusu kupanda kwa maisha na kutokuwapo kwa serikali ya kitaifa ngazi za chini.

  Akihutubia Mkutano Mkuu wa CUF Wilaya ya Mjini jana, Maalim Seif baadhi ya wabunge na wawakilishi wa CUF hawaonekani kwenye majimbo yao tangu walipochaguliwa mwaka jana.

  “Nimesikia malalamiko kwamba sionekani na kwamba, viongozi tumekaa kimya kuhusu operesheni ya Darajani ambako wafanyabishara waliondolewa. Nafikiri ni vuzuri nyie viongozi mkafanya utafiti kabla ya kutulaumu,” alisema Maalim Seif.

  Katika kujibu malalamiko hayo, Maalim Seif alisema aliahidi kupunguza bei ya bidhaa hasa chakula iwapo angechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar.“Mimi siyo rais, ni makamu na mshauri tu wa rais. Hata hivyo, sisi viongozi tunafanya kazi ili kuleta unafuu kwa wananchi,” alisema.

  Kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa, Maalim Seif alisema siyo Zanzibar pekee, bali nchi mbalimbali hali ya maisha inazidi kuwa ngumu na kwamba, limesababishwa na kupungua kwa uzalishaji duniani na uharamia wa Wasomali.

  Maalim Seif alitaja baadhi ya mikakati ya kupambana na hali ngumu ya maisha kuwa, ni kushawishi wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza Zanzibar, kuimarisha kilimo hasa cha mpunga wa umwagiliaji.

  Pia, Maalim Seif alisema miongoni mwa mambo mazuri ambayo Serikali ya Umoja wa Kitaifa inaadaa, ni kuzingatia suala la kubinafsisha soko la Karafuu ili wakulima wawe huru kuuza wanapotaka.Kuhusu muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alisema katiba imeelekeza kuwa mgawanyo wa nafasi ni ngazi ya mawaziri na naibu mawaziri.

  “Nafasi nyengine zote zipo chini ya rais kwa mujibu wa katiba. GNU katika kugawana nafasi imeishia juu tu na ndivyo katiba inavyosema,” alisema.

  Alisema amepunguza kazi na amekuwa haonekani hadharani kwa sababu bado anaumwa, huku akiwataka viongozi wengine wakiwamo wabunge na wawakilishi kuimarisha chama na kuwatumikia wananchi.

  “Nasikitika, ni kweli viongozi tumelala, sioni harakati ndani ya chama. Vijana na wanawake mmekaa kimya, afadhali ya wanawake. Lazima kazi ya kuimarisha chama iendelee ngazi zote,” alisema.

  Alisema baadhi ya wabunge na wawakilishi wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika majimbo yao, lakini amewaonya ambao bado hawajaonyesha juhudi za kuwatumikia wananchi na kwamba, atawabana wamweleze walichofanya.
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Kwani anaposema yeye sio Rais ni makamu ana maana gani??hajijui kwamba he is in top position??so he cant do anything regarding his people??Halafu haya maisha magumu kutolea mifano ya nchi nyingine mi inanikera sana..hapa inaonesha kabisa viongozi wetu sio wabunifu...oh nchi mbalimbali maisha ni magumu...so what??

  Halafu Kilimasera, huyu bwana anaumwa nini hasa??huo ugonjwa wake aliujua kipindi anagombea??kama aliujua kwanini aligombea ilhali yeye hayuko sawa na hataweza kuwatumikia watu wake??this is shame!! ugonjwa wake usiwe excuse kwa kutowatumikia wazanzibar, na wala kwenda huko majimboni hajaenda!! Shame Maalim!!unafikiri uongozi ni mchezo wa kiduku..!!
   
 3. O

  Omr JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zamu ya Slaa inakuja, apewe uwaziri ndio ajue ugumu wake kama huyu mpemba.
   
 4. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Muungano wa CUF na CCM ulikwisha tiliwa mashaka,hicho ndicho walichotaka sasa wacha waone cha moto wataendelea kushika mikoba ya CCM tu.

  Kuna serikali za ummoja lakini sio na CCM ,hawa jamaa hawataki kuona wengine wakitawala,Leo Maalimu anatoa majibu ya kihuni kwa waliomtetea kwa kura ni aibu kubwa.
   
 5. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Mlevi wa madaraka huyu!
  Kwishneeeeee!!!!!
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Bi mdogo kaanza kulalamikia ndoa mapemaaaa.....hadi 2015 atakuwa keshachapwa talaka.
   
 7. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa wazee wa cuf hamna kitu,huu ni muungano wa wazee wa cuf na ccm wa kula keki ya taifa
   
 8. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  We Omri, Kwa taarifa yako hekaheka alilolianzisha DR SLAA nchini so far ni uthibitisho tosha kwamba
  ni mtu anayeweza kufanya kitu tangible.

  Swala la Maalimu kulalamika ni ishara tosha kwamba ndoa ya ccm na cuf zanzibar haina tija kwa
  wananchi, ila sababu cuf hawakuliona hilo tunaconclude kwa kusema kwamba mapungufu yanaanzia
  kwenye uwezo wa viongozi binafsi, alafu watu wanapokuwa wanazungumzia mambo serious ya maisha
  jitahidi kuzuia hisia zako uchwala za kisiasa.

  watu wanalalamika hali ya maisha imekuwa ngumu, wewe unaanza kutoa list ya watu ambao
  nao wangeshindwa kusababisha unafuu uje, kama unakubali kwamba serikali ya ccm imeshindwa
  kusababisha unafuu wa maisha uwepo katika jamii yetu, kuwa huru na fuata hisia zako za kweli
  kwamba mabadiliko yanahitajika, acha unazi wa kijinga
   
 9. H

  HomeSweetHome Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HICHI NDICHO ALIKUWA ANAKITAFUTA SIKU NYINGI Bwana Maalim Seif- "Nafasi nyengine zote zipo chini ya rais kwa mujibu wa katiba. GNU katika kugawana nafasi imeishia juu tu na ndivyo katiba inavyosema," alisema.

  NAFASI ZIMEISHI JUU TU ILI YEYE NDIO AFAIDIKE, HAPA HAZUNGUMZII NI JINISI GANI NASAFI YAKE INAWASAIDIA WAZANZIBAR, YEYE ANAWAZA NAFASI YA ULAJI, AFU KWA NINI WEWE UWE MSHAURI WA RAIS, WAKATI CUF INA AGENDA YAKE YA KISIASA NA INA ILANI YAKE YA UCHAGUZI? HAPA WANAISAIDIA CCM KUTEKELEZA ILANI YAO.

  MASIKINI WEEE

  SASA AMEPATA ALICHOTAKA (Maalim Seif) KWA NINI ANASHANGAA HALI HII? HAPA? "Nasikitika, ni kweli viongozi tumelala, sioni harakati ndani ya chama. Vijana na wanawake mmekaa kimya, afadhali ya wanawake.

  Lazima kazi ya kuimarisha chama iendelee ngazi zote," alisema. NA HUU NDIO MWISHO WA CHAMA KINACHOITWA CUF huko Zanzibar kwa kuwa wameshatekwa na CHAMA CHA MAGAMBA-CCM
   
 10. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Ndoa ya Cuf na Ccm haya ndio matokeo yake na wasijilaumu kbs na wasiteme waendelee kumeza tu
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  HSH,wakati ule watu wanashangilia ujio wa GNU,nilisema humu kuwa "that was the begining of an end to CUF“. Niliambulia matukano.

  Wana CUF wanashangilia GNU huku nafasi ya makamu kwanza wa rais ni boya tuu with no any executive powers. Mawaziri wa CUF walioko ndani ya GNU wanatekeleza ilani ya
  CCM!.
  Lazima tukubali GNU imeleta amani na utulivu at the expence of CCM having everything to gain and nothing to loose with CUF loosing everything with nothing to gain.
   
 12. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,074
  Likes Received: 15,725
  Trophy Points: 280
  hahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaahahahah:happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy:
   
 13. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hii inathibitisha kwamba serikali za umoja wa kitaifa hazina ufanisi ambao wananchi huwa wanautarajia. Angalia nchi kama Kenya na Zimbabwe mambo bado ni yaleyale. Nchi za kiafrika zifikirie namna nyingine ya kuwasaidia wanananchi siyo kutumia serikali za umoja wa kitaifa ambazo hazina tija.
   
 14. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kiwavi... ebwana kumbe vipo kitambo? Msekwa hakukuona toka 10th Nov.2008!
   
 15. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  Chuki binafsi?
   
 16. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Msaliti wa democrasia. Wana ccm pimeni wenyewe na mchukue hatua mara moja kabla hamjachelwa
   
Loading...