Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Tokea Maalim Seif alipofunguka na kuanza kutembelea , mikoa yote ya Zanzibar Kichama, amewafanya viongozi wa SMZ kuacha kabisa shughuli za kuendesha nchi na kuanza kumjadili yeye tu. Hali hii imetapakaa kwenye mikutano ya ndani ya CCM, semina na hivi majuzi kuhamia hata kwenye baraza la wawakilishi.
Katika jambo lisilio la kawaida Baraza la Wawakilishi, liliacha shughuli zake za kujadili bajeti na kuanza kumjadili Maalim Seif. Maneno yasiokuwa na staha wala heshima kusemwa kwenye baraza, tena ya kutamkwa na watoto wadogo wa kike yalifanyika, kanuni zote ziliwekwa kando.
Mwakilishi Ali Salim Haji, aliotoa hoja hiyo binafsi na kuungwa mkono na baraza lote, alisema " Seif Sharif ni Rais wa CUF, Rais wa Daraja Bovu na Garagara na Rais wa watu wasio na akili Zanzibar, Seif ni Rais wa wendawazimu, Seif Shariff ni mwendawazimu na anaowaongoza pia ni wendawazimu.” Baraza lilizizima kwa makofi na mayowe kumshangilia mtoa hoja. Kama hayo hayatoshi, Wawakilishi waliendelea kusema kuwa Maalim Seif hana mda mrefu atakufa na wanawaonea huruma vijana wanaomtegemea!
Mbali na kurushwa "live",Shirika la utangazaji wa ZBC lilitengeneza kipindi maalum na kurejea majadiliano hayo mara kadhaa, bila kujali athari zake.
Maazimio yaliotokana na hoja hiyo binafsi ni kutoa maagizo yakufanyiwa kazi haraka, baadhi yao ni:-
1. Aagizwe Msajili wa vyama vya siasa, akifute chama cha CUF mara moja kama vile alivyowahi kufanya kwa chama cha PONA
2.Asiwe na msafara wa aina yoyote zaidi ya gari ya ulinzi anaopewa na Polisi
3.Asifanye mkutano wowote wa chama hata wa ndani
4. Anapopita watu wasikusanyike wala kumshangilia, watu hao watakuwa wamevunja sheria na hatua stahiki zitachukuliwa
Swali, ni mpkaka lini Baraza letu litakapokusanya akili na kuanza kujadili maendeleo ya nchi yetu na kupanga vipi tutavyoweza kuivusha Zanzibar kutoka mkwamo huu wa kisiasa?
Ni lini Baraza litaacha kudahili kiumbe mmojammoja?. Maalim Seif hana "Kifaru wala Rocket launcher" sasa hiki kifafa cha siasa kinatoka wapi?