Maalim Seif Aitisha Mgomo Baridi Unguja

Maalim Seif Aitisha Mgomo Baridi Unguja

sanif

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2016
Posts
480
Reaction score
324

SIKU moja tu baada ya kuhojiwa na Polisi kwa saa tatu visiwani hapa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema njia pekee ya kumwondoa Rais Dk. Ali Mohamed Shein madarakani, ni kuendeleza mgomo baridi.

Maalim Seif alisema hayo jana alipozungumza na wafuasi wa chama hicho, Kilimahewa Wilaya ya Mjini Unguja, katika ziara zake za kuimarisha CUF katika kila wilaya za Zanzibar.

Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Salum Msangi, aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa jeshi lake lilimhoji Maalim Seif kwa saa tatu.

Ingawa Msangi hakusema walimhoji katika masuala gani, Wakili wa Maalim Seif, Awadh Ali Said, alisema juzi kuwa mteja wake aliwekwa kati na maafisa 12 wa polisi, ambao walitaka kujua pamoja na mambo mengine, ni kwa nini hawakatazi wafuasi wake kumwita Rais.

Akizungumza jana, Maalim Seif alisema mataifa ya nje hayawezi kumwondoa Dk. Shein madarani lakini kama wananchi na wafuasi wa CUF wataungana kufanya mgomo baridi, haitafika miezi mitatu kabla hajaachia madarakara.

“Wala msidhani kwamba atakuja Mmarekani kumwondoa Dk. Sheni,"alisema Maalim Seif na kuongeza kuwa: "Hii ni nchi, taifa lingine haliwezi kuingilia."

Katibu mkuu huyo alisema anachoweza kufanya Mmarekani ni kuzuia misaada na wameshalianza hilo.

"Sasa hawa wezetu mataifa ya nje wanatubeba na anayebebwa hujikaza. Tukikaza uzi huyu bwana miezi mitatu hafiki kwa sababu hana fedha, ataweza vipi kuiongoza Serikali wakati baadhi ya mataifa yameshazuia misaada yao?"alihoji.

CUF imegoma kuitambua serikali ya Dk. Shein kwa madai kuwa uchaguzi mkuu wa marudio wa Machi 20, mwaka huu, uliomwingiza madarakani ni batili.

CUF inadai kutambuliwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, ambao ilielekea kushinda na ambao matokeo yake yalifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanizbar (ZEC), Jecha Salum Jecha, kwa madai ya kuwapo kwa kasoro nyingi.

ZEC ilifuta matokeo hayo licha ya waangalizi wa ndani na wa kimataifa, wakiwemo kutoka Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Ulaya (EU) na Marekani kuutangaza kuwa huru na haki.

Akizungumza katika kikao hicho jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui, alisema Maalim Seif ndiye mkombozi wa Wazanzibari kama alivyokuwa Nelson Mandela wa Afrika Kusini.

Alisema wana imani kuwa Maalim Seif ndiye Rais wa Zanzibar na wataendelea kumwita Rais na hakuna wa kuwazuia kwa sababu yeye ndiye aliyeshinda katika uchaguzi wa Oktoba 25.

Alisema kitendo cha wafuasi wa CUF kuwatenga wafuasi wa CCM na viongozi wa Serikali walioko madarakani ni halali na kuwataka wafuasi hao kuendelea na mgomo huo.

“Hakuna cha kuogopa, endeleeni kuwagomea,"alisema Mazrui na kuwataka wasiende katika shughuli zao, mazishi na wanaouza maduka wasiwauzie bidhaa mpaka haki yao irejee.
 
naamini tunafichwa taarifa juu ya hali halisi inayoendelea zenji.kazi IPO huu mwaka.
 
Maisha Unguja yanenda kama kawaida, hiyo matamko yao kila siku hayawazuwii watu kufanya kazi zao...Na wasije wakafanya upuuzi wao huo unguja wanajua nini kitafuata
 
Kwani maduka yote zanzibar ni cuf tu. Ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya kuandaa maroli ya kushughulikia mazishi ya wanaccm huko pemba.
Kwaeli cuf wapumbavu. Ngoja tuone mafanikio yake
 
Huyu mzee ana lake analolitafuta na atalipata tu wewe muache amesahau kuwa kila mchuma janga huangaika na nnduguze, arudishe kwanza familia yake iliyopo arabuni halafu ndio aendelee choko choko zake.
 
Shein hana hamu n usanii wa ccm bara! Anatawala kama zombie tu hawezi kwenda ulaya au marekani mwisho wake ataenda arabuni ambapo hata hawaelewi demokrasia, siku akija kwenda nchi zinazojitambua nadhani ataanguka kwa pressure! Sio rais halali wa Zbar! Ameiba na amebaka demokrasia!!!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Maalim anahiji utawala gani ambao hauzingatii sheria???
Kuliko kutaabisha watu ni bora aende mahakamani.hii njia itamgarimu kwasababu msumali unapoingilia ndipo utakapotokea.Ajifunze kwa MOHAMED MURSI.
 
Kwani maduka yote zanzibar ni cuf tu. Ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya kuandaa maroli ya kushughulikia mazishi ya wanaccm huko pemba.
Kwaeli cuf wapumbavu. Ngoja tuone mafanikio yake
I wish hao wanao goma wafutiwe leseni.
 
Maalim Seif ni shujaa ! Mtu uko buguruni unajifanya uko unguja , unataka kumdanganya nani ?
Mimi wacha buguruni hata zipo Tanzania... lakini nakuambia maisha ya unguja yanaenda kama kawaida..Seif sharif hana ushujaa ni mtu ambae ameshaanza kuchanganyikiwa na akili imeshamtoka kwa uchu wa madaraka... na inaonyesha hata unguja huuijui
 
Ngoja nisubiri komenti zaidi ntarudi

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom