Mhe Hamad Rashid amewaowa hao wabara kwa hiyo wasimtukane sana. Hivi huu mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa (GNU), imeanzia Zanzibar tu? Na hii si serikali ya mseto kama waandishi wa habari wa bara wanavyoandika. Hivi kule Nairobi kuna serikali ya aina gani vile? Hivi kule Nairobi watu walipambana mauwa ikisha wakaunda serikali yao mpya na baadaye katiba mpya au kwanza walitwangwana magumu na kuuwana? Hivi kule Harare kuna serikali ya aina gani vile? Hata leo iwe dhambi kwa Zanzibar. Sisi kama kuna uwezkano wa kuunda mfumo ambao utatusaidia kufanya mambo yetu na kuifaidika nayo, basi tupo tayari haya mavyama ya siasa yakafutwa.
Maalim Seif hajalewa wine yeye ni Muislamu wa kweli, ungesema kalewa kahawa na haluwa ya malindi hapo tungekuelewa. Nyinyi chadema mukipewa serikali mutalewa supu ya utumbo kwa ndizi choma ha ha ha!
Wanasema ipigwapo Zanzibar basi zile dharuba zake.... jaza wewe. Baada ya miaka mitatu ya serikali yetu, nyinyi mutakuja kusoma kwetu kama mulivyo soma ile miaka ya 1984 tulipo uwa azimio la Arusha, tukakufundisheni biashara huko bara baada ya kupanda maboti na huku bahari munaogopa, hebu vunjeni Muungano mupate kufaidi majumba waliyo jenga Dar na kuufanya mji leo hii. Baada ya hapo mumalizane kwa udini na umajimbo wewe mchaga, mmakonde, mmasai...