MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Magazeti yanaripoti usiri uliokuwa umetanda kuhusu afya na matibabu anayoendelea kuyapata Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad huko India umefunuliwa.
Maofisa kadhaa wa juu wa CUF walidai kutofahamu lolote kuhusu kinachoendelea nchini India ambapo Maalim alikwenda kwa matibabu wiki iliyopita baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kumuidhinishia kiasi cha Sh. Milioni 350 licha ya madai ya CUF ya kutoitambua serikali ya sasa ya Zanzibar.
Imegundulika kuwa Maalim Seif amelazwa katika hospitali ya Appolo Hyderabad na tayari ameishafanyiwa upasuaji mkubwa wa (uti) mgongo.
Maalim ameshauriwa kupumzika hadi walau baada ya Machi 10 mwaka huu lakini amekataa ushauri huu na anataka kurudi nyumbani mapema zaidi.