TANZIA Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia

DAGAA WA MWANZA

Senior Member
Jan 27, 2019
169
464
Maalim2.jpg

Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Maalim Seif amefariki ktk Hospitali ya Muhimbili. Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ametangaza siku 7 za maombolezo ya Kitaifa

Pia soma > Wasifu/ CV ya Maalim Seif Sharif Hamad, Historia yake kwa Ufupi

Kupitia ukurasa wa Twitter, Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli atoa salamu za rambirambi pamoja na kutangaza siku tatu za maombolezo Kitaifa.

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mwinyi, Familia, Wazanzibari, wanachama wa ACT-Wazalendo na Watanzania wote. Mungu amweke mahali pema peponi,Amina"

Maalim.JPG


1613563766691.png


Pia soma > Zanzibar 2020 - Uchambuzi Urais Zanzibar 2020: Nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad
20210217_132853.jpg

Maalim Seif alizaliwa kutokana na familia ya wakulima wa kijiji cha Mtambwe, nje kidogo ya mji wa Wete, Pemba, katika Oktoba 22, 1943, Maalim Seif alivuka bahari ya mkondo wa Pemba kuja Zanzibar kuendelea na masomo ya sekondari kutoka 1958 hadi 1963.

Hakuweza kuendelea na masomo ya chuo kikuu pale alipotakiwa aende kusomesha katika shule za sekondari ili kujaza mapengo yaliowachwa na walimu wengi wa Kiingereza na wachache wa kizalendo baada ya Mapinduzi ya 1964. Wakati ule siasa kali za utawala wa mkono wa chuma ulishuhudia serikali ikitaifisha vikataa vidogo vya mashamba na nyumba za makazi za watu walioonekana maadui wa Mapinduzi ziliipelekea Zanzibar kuelezwa na nchi za Magharibi kama Cuba ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo, alifanikiwa kuchukua shahada ya kwanza ya Elimu, Sayansi ya Kisiasa na Uhusiano wa Kimataifa´kutoka mwaka 1972 hadi 1975 na aliporudi Zanzibar alichaguliwa msaidizi maalum wa Rais wa Zanzibar mpaka mwaka 1977 alipochaguliwa Waziri wa Elimu.

Katika medani ya siasa Maalim Seif alichaguliwa mjumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa ya CCM ambayo aliitumikia kwa miaka 11. Katika mwaka 1984 kufuatia kile kilichojulikana kama kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Visiwani kulikoshuhudia kulazimishwa kustaafu kwa aliyekuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Sheikh Aboud Jumbe, Maalim Seif alichaguliwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Lakini kauli zake za uwazi za mara kwa mara za kuonyesha hafurahishwi na mwenendo mzima wa Muungano na kueleza Zanzibar haitendewi haki kwa baadhi ya mambo ndani ya Mungano kuliepelea kutimuliwa katika chama na pia kupoteza wadhifa wa Waziri Kiongozi kufuatia hatuahio ya chama.

Tokea wakati huo aliandamwa kwa kuonekana tishio la kisiasa na mwaka 1989 alifunguliwa mashitaka bandia ya kupatikana na nyaraka za siri za serikali. Alikaa miaka miwili gerezani, baadhi ya wakati katika chumba akiwa peke yake kwa muda unaoweza kufikia wiki mbili mpaka alipoachiwa na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwa kuwa hakuwa na kesi ya kujibu.

Tanzania ilipofungua milango yake na kuruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, Maalim Seif na baadhi ya wenzake aliofukuzwa nao Halmashauri Kuu ya CCM walikuwa miongoni ma walioanzisha Chama chaWananchi (CUF) na kuwa Makamo Mwenyekiti wake wa kwanza

Aligombea Urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, mwaka 2000, 2005, 2010,2015 na 2020, Alishindwa kwa kura chache, lakini mwenyewe amekuwa akiamini alishinda chaguzi zote hizo na aliporwa ushindi kwa sababu Tanzania na hasa Zanzibar haijakuwa tayari kupokea mfumo wa demokrasia kwa moyo safi.

Mnamo tarehe 18 machi 2019 maalim self alitangaza kujiunga na chanma cha ACT wazalendo baada ya kutokea kutokuelewana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba katika Mgogoro uliwafikisha Mahakani na Upande wa Seif Ukashindwa kesi.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi alimteua Dec 07, 2020 Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar. Uteuzi uliozingatia matakwa ya kifungu cha 9(3) cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinachosomeka kwamba, muundo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar utakuwa wa Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia.

Hadi mauti unamkuta, Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa.

Tarehe 31 Januari 2021 chama chake cha ACT Wazalendo kilisema kuwa wasaidizi kadhaa wa Bw Maalim Seif wamepatwa na maambukizi ya virusi vya corona. Pia kiliwafahamisha wanachama wake, Wazanzibari, pamoja na umma wa Watanzania kuwa mwenyekiti wake Maalim Seif Sharif Hamad na mkewe Bi Awena, wamethibitika kupata maambukizi ya Covid 19. Taarifa hiyo iliendelea kusema kwamba


''Katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi madaktari walimshauri Maalim Seif kuwa ni vyema awepo chini ya uangalizi maalum katika kipindi chote atakachokuwa anaendelea na matibabu'', ilisema taarifa ya ACT Wazalendo. Maalim Seif alipumzishwa katika Hospitali ya Mzazi Mmoja, Unguja.

Zaidi soma; Zanzibar: Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe Bi Awena waambukizwa virusi vya Corona

Apumzike kwa Amani

---
PICHA

Maalim 3.jpg

Maalim Seif na Mwalimu Nyerere nyumbani kwa Mwalimu (The Clinic) Msasani

Maalim 4.jpg

Vipande vya picha mbalimbali vikionesha harakati za Maalim Seif

Maalim5.jpg

Maalim Seif na Salmin Amour mwaka 1999 baada ya Mazungumzo ya Mwafaka

Tujikumbushe ahadi zake Uchaguzi 2020

 
Makamu wa kwanza wa Zanziba Maalimu seif Sharif Hamad amefariki dunia taarifa iliyotolewa muda huu na Rais wa zanzibar kuthibitisha kifo hicho, pia Rais ametangaza siku 7 za maombolezo na bendera kupepea nusu mlingoti

Kupitia ukurasa wa Twitter rais wa Jamhuri atoa pole

Mbona umeandika harakaharaka sana? Hebu tulia na uhariri bandiko lako!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom