Maalim Seif Aanza kutekeleza Falsafa ya Lowassa;Wazanzibar watamwelewa?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
16,003
Amani iwe kwenu.

Falsafa za siasa za Lowasa zzimeanza kutekelezwa na Maalim Seif imedhihirika.

Katika hali ya kushitukiza jana baada ya swala lilijitokeza kundi kubwa linalosemekana kuandaliwa na kina Jussa na wenzake ili kutengeneza taswira ya kukubalika Maalim.Vijana waliima "raisi,raisi...!.

Nilikuwa na muuliza Maalim; Je tangu huu mwaka uanze hujawahi kwenda msikitini? Kwanini mara nyingine vijana hawakusanyiki?..Cuf wacheni michezo hii ya kuigiza.Huku Dar nako Lipumba ametengeneza makundi kuja kumshawishi arejee uenyekiti,Prof Lipumba hizi siasa za maigizo ulianza lini?Mbona kila wanapokuja hatupati mrejesho?

Ikumbukwe tu kuwa maigizo ya kutengeneza wachungaji,masheikh,wanafunzi yalifanywa CCM na kukatwa alikatwa.Sasa hili limewakamata na litawapoteza.

Propaganda za uongo zina ukomo...na ukomo ukifika mtaaibika.Sidhani kama Jussa na wenzake wanaweza kuandaa makundi haya kila ijumaa kwa miaka mitano bila ya kuchoka na madhara yake watawachoka nanyie.Kwa Prof.Lipumba sidhani kama makundi haya yatadumu kuja kufanya maigizo hapo kwako kwa muda mrefu bila kupata matokeo,usipopewa uenyekiti watakumwaga na utabaki na aibu.

Nimeandika haya machache ili kunyoosha wanaopotoka.Nawasilisha.
 
Na leo alikwenda Pemba akapokewa kwa kishindo sijui ni maigizo nayo? Na wale ccm wanaosusiwa misiba na misikitini sijui ni maigizo!!!!?
 
Na leo alikwenda Pemba akapokewa kwa kishindo sijui ni maigizo nayo? Na wale ccm wanaosusiwa misiba na misikitini sijui ni maigizo!!!!?
Mnaweza mkawa wachache mkasusa haimaanishi kuwa alishinda uchaguzi,hiyo ni misukule yake leo ni mahsusi wameandaliwa.....inamaana tokea tarehe 25 oct,2015 hajawahi kwenda msikitini?
 
Umsingi wa mada yako uko wapi ikiwa hoja yako kwanza umezungumzia habari kuonekanwa msikitini jana

Ndio tunakuuliza kwani ni mara kwanza kumuona akiwa msikitini jana????
 
Viherehere wa ccm uwa hawajifichi na kila wakati uwa hawana point yoyote ya msingi sawa tu na wabunge wao.
 
Naomba kuuliza kwani toka uchaguzi uishe leo ndio Mara ya Kwanza Sefu kutua Pemba?

Na kama ametua Mara nyingi kwanini iwe Jana ndio aimbwe Rais Rais,kama sio maigizo.!
 
Naomba kuuliza kwani toka uchaguzi uishe leo ndio Mara ya Kwanza Sefu kutua Pemba?

Na kama ametua Mara nyingi kwanini iwe Jana ndio aimbwe Rais Rais,kama sio maigizo.!
Tangu tar 25 mwezi octoba mwaka jana
 
Umsingi wa mada yako uko wapi ikiwa hoja yako kwanza umezungumzia habari kuonekanwa msikitini jana

Ndio tunakuuliza kwani ni mara kwanza kumuona akiwa msikitini jana????
Kwenda msikitini huenda ila tunashangaa mara hii watu waliondaliwa kumshangili,mbona siku nyingine hawafanyi?
 
Naomba kuuliza kwani toka uchaguzi uishe leo ndio Mara ya Kwanza Sefu kutua Pemba?

Na kama ametua Mara nyingi kwanini iwe Jana ndio aimbwe Rais Rais,kama sio maigizo.!
Haya maigizo yalianzia Unguja msikitini,je ndio mara yake ya kwanza kuswali?
 
kumbe mikusanyiko ya magu huwa inaandaliwa et watu wamemzuia hivi unaweza kuzuia msafara wa rais na ile spid ya yale magar? usanii kila kona!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom