Maajabu ya ziwa Natron

Aisee kama Ziwa Natron nalo lipo mnadani sijui tunaelekea wapi watz
 
Mshana Jr, huwa nahusudu maandiko yako lakini hili andiko lako naona kama umepigwa!
Nimepita mara nyingi pale Ziwa Natron kuelekea Waso (Loliondo) lakini hiki ulicholeta hapa si sahihi.
Ni kweli yapo magadi ya kutosha yanayotiririka toka Mlima wa Mungu (Oldonyo Lengai) ulio jirani na Ziwa Natron lakini haya uliyoleta hapa si sahihi kabisa.
 
Halina samaki?
Wapo pale samaki wachache wanoweza kustahimili viwango vikubwa vya maji chumvi.
Pia wapo Flamingo wa kutosha hasa kutegemea na msimu.
Pia kuja joto kali sana hadi kufikia 41 C. Mazingira ya eneo lile kwa kweli ni magumu sana lakini hata hivyo utawaona vijana wa Kimasaai wakichunga makundi ya mbuzi na pale waonapo gari likipita husimama katikati ya barabara na kuomba maji ya chupa.

Katikati na Mlima Odonyo Lengai na Ziwa Natron kuna kijiji kinaitwa Ngare Sero; Kutokana na joto kali sana la eneo lile, kama upo safarini ni lazima usimame pale kidogo angalau upate pause - utapata . maji baridi na nyama choma (mbuzi) kisha uendelee na safari kuelekea Mto wa Mbu kupitia Engaruka (historical Site) au Longido (kama unaelekea Arusha).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…