Maajabu ya watu wasioona (Vipofu)

Maajabu ya watu wasioona (Vipofu)

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
TAFSIRI ya neno ulemavu hutofautiana kutoka kwa mtaalam moja hadi mwingine, kutokana na mazingira ambamo tafsiri hiyo hutumika.

Upofu ni hali ya kukosa kuona kutokana sababu za kifisiolojia au zinazohusiana na neva.
viwango mbalimbali vimetengenezwa ili kuelezea kiwango cha kukosa kuona na kufasili upofu. Upofu kamili ni ukosefu kamili wa kuona maumbo na mwanga na hurekodi kikliniki kama NLP, kifupishi cha "no light perception"/kukosa kuona mwangaza.

Neno Upofu linalotumiwa mara nyingi kuelezea kuharibika sana kwa macho kuliko na kuona kwa masazo. Wale walio na uwezo wa kuona mwangaza pekee huwa hawawezi kuona kitu kingine ila kutofautisha mwangaza na giza na kuona upande ambao mwanga unatoka.

1. Mtu anaweza kuwa mlemavu wa macho kwa muonekano tu kwamba HUENDA HAONI CHOCHOTE, lakini ukweli ni kwamba ni asilimia 10-15 tu ya kundi hili ambao hawaoni kitu chochote kabisa.....walio wengi wanaweza kuona rangi tofauti, miali ya mwanga na maumbo mbalimbali ...............kifupi ni kwamba hawaoni kwa macho lakini wanaona kiakili
.......Ulemavu wa macho si upofu wa nafsi.....
2. Unaweza kutembea na mtu mwenye ulemavu wa macho bila kujua kwani ni chini ya asilimia mbili tu ya kundi hili hutumia mkongojo mweupe kuwaongoza..wapo wanaoutumia MBWA ama kutotumia kitu chochote cha kuwaongoza hata ikawa ngumu mtu kutofautisha anayeona na asiyeona kati yenu
3. Huu ni kweli wa kushangaza kwamba 80% YA WATU wasiiona duniani wangeweza kuepuka hali hiyo kwa TIBA MUAFAKA ama kuwa na ratiba ya uchunguzi wa macho yao mara kwa mara lakini kwa kuwa TUNADHANI tuko salama, wengi tunaishia kwenye ulemavu wa macho......Imegundulika kwamba kisababishi kikubwa cha ulemavu wa macho ni mtoto wa jicho ambaye ni RAHISI SANA KUMKABILI KWA UPASUAJI kungali mapema .....
Kulingana na makadirio ya WHO, visababishi vya upofu vya kawaida duniani kote katika 2002 vilikuwa:
mtoto wa jicho (47.9%),
glakoma (12.3%),
kuzorota kwa seli kunakohusiana na umri (8.7%)....Uhusiano kati ya umaskini na kuharibika kwa macho kunakoweza kutibu ni dhahiri
4. Watu wenye ulemavu wa macho huota NDOTO KAMA WATU WANAAONA (nadhani nimeeleweka) wawapo usingizini yaani anawexa kuota anacheza moira akiwa anauona na kupiga shuti ...tofauti ni kwamba ndoto zao hutawaliwa sana na sauti, RIHI na ladha mbalimbali.
5. Vipofu ambao macho yao bado hayajaharibika wanaweza kutambua kukiwa na mwangaza ingawa hawaoni kutokana na upakiaji wa kurekodi kwa mzunguko wa mwanga/giza wa masaa 24. Ishara za mwangaza za lengo hili husafiri kupitia njia ya retinohaipothalamia, kwa hivyo neva ya jicho iliyoharibika kupita mahali ambapo njia ya retinohaipothalamia hutokea kwenye jicho si kizuizi.
6. Mara nyingi watu walio na Ualbino huwa hawana uwezo mzuri wa kuona kiasi kwamba wengi wao ni vipofu kisheria, ingawa kwa hakika wachache wao hawawezi kuona. Ugonjwa wa Leber's congenital amaurosis unaweza kusababisha upofu kamili au kuharibu kabisa uwezo wa kuona kuanzia kuzaliwa au mapema utotoni.
7. Idadi ndogo ya watu hutumia mbwa wa kuongoza kuwasaidia kutembea. Mbwa hawa huwa wamefunzwa kuepuka vikwazo mbalimbali, na kuonyesha wakati inakuwa muhimu kwenda juu au chini kwenye ngazi.

8. Watu wenye ulemavu wa macho HUDUMU sana kwenye ndoa kuliko wanaoona..unajua ni kwa nini????..........
 
Kuna huyo mmoja tulisoma nae advance sasa hivi huwa namuona anapost fb, anakoment na kulike picha....
 
hapo kwenye kipofu kuona ndio nataka maelezo ya kina!
Ikiwa kipofu hajawahi kuona mfano umbile lolote lile la kitu mfano gari nzuri,wanyama, na i vitu vingine, sasa je picha zake za ndotoni kuhusu hivyo vitu anazipataje/anazijenga vipi???
 
hu
hapo kwenye kipofu kuona ndio nataka maelezo ya kina!
Ikiwa kipofu hajawahi kuona mfano umbile lolote lile la kitu mfano gari nzuri,wanyama, na i vitu vingine, sasa je picha zake za ndotoni kuhusu hivyo vitu anazipataje/anazijenga vipi???
enda ni wale waliowahi kuona yaani vision impaired
 
Back
Top Bottom