Maajabu ya Rais Samia Suluhu

Maajabu ya Rais Samia Suluhu

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
Na Emmanuel J. Shilatu

1. Rais Samia ameimarisha mahusiano kidiplomasia ya Tanzania kwa nchi jirani na kimataifa. Mfano hai kuimarika kwa mahusiano baina ya Tanzania na Kenya kutokana na pande zote kuondoa vikwazo vidogo vidogo vilivyokuwepo.

2. Rais Samia ameendelea kuiheshimisha nchi ya Tanzania kimataifa kuwa ni Taifa huru linaloendelea na ukombozi wake wa kiuchumi kupitia miradi ya kimkakati inayoendelea kujengwa nchi nzima.

3. Rais Samia ameendelea kuwa mtetezi wa Bodaboda, Wajasiriamali wadogo kwa kuhakikisha Serikali yake inawaheshimu na kuendelea kulinda shughuli zao pasipo kusumbuliwa na mamlaka za mapato na vyombo vya ulinzi na usalama.

4. Rais Samia ameendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini na kufanya wawekezaji kukiri hadharani utofauti na maboresho ya kibiashara nchini. Mfano hai wa Mwekezaji ni Dangote ambaye ni Mwekezaji wa kiwanda kikubwa cha kutengeneza saruji nchini, ameridhishwa na mazingira ya sasa kuwa hayana urasimu na milango ya biashara yamefunguka sana na yupo tayari kuongeza uwekezaji wa kiwanda kingine kikubwa Tanzania.

5. Rais Samia ametoa maelekezo ya yameshatekelezwa ya kufungua akaunti za Wafanyabiashara zilizofungwa kwa sababu mbalimbali na TRA na wakae meza moja na Wafanyabiashara kuona namna bora kumaliza changamoto zilizopelekea akaunti zao kufungwa. Hii imepeleka furaha na vicheko kwa Wafanyabiashara kote nchini.

6. Rais Samia ameendeleza mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ambapo wanaotuhumiwa na vitendo hivyo amekuwa akiwaweka pembeni na kutoa maelekezo uchunguzi ufanyike. Tumejionea hayo kule bandari, hazina nk.

7. Rais Samia ameendeleza ujenzi wa miradi ya kimkakati kwa mwendo na kasi ile ile ya awali. Tunajionea miradi ya SGR, Bwawa la Nyerere nk ikiendelea kwa kasi ya ajabu. Huku ni kuenzi kwa vitendo na picha isiyo na shaka ya kuwa kitu kimoja.

8. Rais Samia ameongeza kasi ya ukuzaji ufanyaji biashara nje ya mipaka ya Tanzania. Mfano hai ni furaha na vicheko vya Wafanyabiashara wa Mahindi kwenda nchini Kenya kwa ulaini kabisa kufanya biashara.

9. Rais Samia ameendelea kuhakikisha anaimalisha ulinzi na usalama ndani na nje ya mipaka pamoja na kupambana vikali na madawa ya kulevya. Kukamatwa kwa zaidi ya tani ya Madawa ya kulevya kule mkoani Lindi; Mauaji ya Maalbino hayapo; Matukio ya wizi na ujambazi yamepungua kwani walianza kumbipu wakakutana na shoo kali ya Rais Samia. Pongezi za kipekee kwa vikosi vyote vya ulinzi na usalama nchini kwa kazi kubwa wanazoendelea kuzifanya kila siku.

10. Ilani ya uchaguzi 2020 - 2025 inaendelea kutekelezwa vyema kwa vitendo kwa kasi kubwa; Shughuli za Serikali zinaendelea kufanyika pasipo mkwamo wowote ule. Huu ni ushahidi wa kazi kubwa ya ukusanyaji imara wa kodi unaopelekea upatikanaji wa mapato ya ndani yanayowezesha nchi kujitegemea kiuchumi.

Shilatu, E.J
 
Nafikiri umeandika hivi kwa lengo la kutaka kuonesha kuwa raisi Samia she is doing better than hayati Magufuli, lkn ukweli ni kwamba unazidi kuipoteza Chadema na magenge yake ndan ya ulingo wa siasa, kwani mwaka 2025 watakosa hoja za kufanya watanzania wawaamini na kuwachagua kushika madaraka kwan mama atakuwa ameshafanya mengi ya faida kwa watanzania. Asante mleta mada kwa kuendelea kumtengenezea bimkubwa njia ya ushindi mnono.
 
1. TSH 1.6 billion kuibiwa hazina kwa miezi miwili
2. Mitandao ya luku na ya tra kuzima bila jufanya kaxi
3. Tangu mwezi march Hadi June haijawahi kutembelea kigoma Wala songwe
4. Ujambaxi na wizi kuongezea kwa kasi
5. Pesa kuendelea kukosekana mitaani
6. Wakuu wa WILAYA na DED ni wale wale na wanaendelea kuiba fedha za umma.
7. Barrick hajadaiwa mamilioni aliyekuwa ameanza kuyalipa.
 
Hizo propaganda zako hazifuti ukweli kuwa anaetawala Tanzania ni kivuli cha Kayafa!
4jHF.jpg
 
Nafikiri umeandika hivi kwa lengo la kutaka kuonesha kuwa raisi Samia she is doing better than hayati Magufuli, lkn ukweli ni kwamba unazidi kuipoteza Chadema na magenge yake ndan ya ulingo wa siasa, kwani mwaka 2025 watakosa hoja za kufanya watanzania wawaamini na kuwachagua kushika madaraka kwan mama atakuwa ameshafanya mengi ya faida kwa watanzania. Asante mleta mada kwa kuendelea kumtengenezea bimkubwa njia ya ushindi mnono.
Natanguliza samahani kwanza... lugha sio yetu hii

Samia she is doing [emoji777]
Samia is doing [emoji818]
She is doing [emoji818]
 
Hayati Magufuli kaacha legacy kubwa sana, naamini kila kiongozi ajaye atafuata nyayo zake na kuongezea zaidi ya yale aliyoyatenda ht Magufuli
 
Watekaji bado wapo jamani duuu haya tuone cinema hii....hawataki katiba mpya iongelewe
 
Nafikiri umeandika hivi kwa lengo la kutaka kuonesha kuwa raisi Samia she is doing better than hayati Magufuli, lkn ukweli ni kwamba unazidi kuipoteza Chadema na magenge yake ndan ya ulingo wa siasa, kwani mwaka 2025 watakosa hoja za kufanya watanzania wawaamini na kuwachagua kushika madaraka kwan mama atakuwa ameshafanya mengi ya faida kwa watanzania. Asante mleta mada kwa kuendelea kumtengenezea bimkubwa njia ya ushindi mnono.
Kwa hiyo sifa kwa SSH zinatolewa na CDM? Ama kweli mmenyujwa.galasa funza wako hatua za mwisho kutengeneza mboji murua msahau ah utakufa kwa sonona
 
Back
Top Bottom