Maajabu ya Quick share kwenye simu zetu

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
๐—จ๐—ป๐—ฎ๐—ถ๐—ท๐˜‚๐—ฎ ๐—š๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐˜…๐˜† ๐—ค๐˜‚๐—ถ๐—ฐ๐—ธ ๐˜€๐—ต๐—ฎ๐—ฟ๐—ฒ ??

Kuhamisha kitu toka kwenye simu yako ya Samsung kwenda kwenye kifaa chingine ambacho ni Simu au kompyuta unajua ni rahisi sana ? Najua ulikua hujui.

Watumiaji wa simu za Samsung wameletewa njia rahisi ya kuhamisha vitu toka Simu moja kwenda nyingine yani utaweza ku share picha, videos, files toka Simu nyingine ya Samsung ila lazima hiwe galaxy zingatia.

Inawezekana unakutana na watu au tukio fulani mukapiga picha za ukumbusho alafu ukataka kushare na wenzako sio lazima utumie xender, Bluetooth au Whatsapp aisee.

Kuna feature inaitwa Quick share kwenye Samsung ambayo inakusaidia kuweza kushare picha, videos, files na Samsung wenzako ambao ni Wana familia, ndugu na jamaa.

Ingia setting >> connected device >> Quick share hakikisha hii feature Iko On kwako kabla ujaanza kurusha kitu kwa rafiki yako. Hii quick share kwanza haipunguzi ubora wa picha , video unayotuma inaenda vile vile kama ilivyo.

Baada ya Ku enable hii feature fungua kitu unachotaka ku share na mwenzako gusa Kisha bonyeza share >> chagua Quick share>>jirani yako uliyekaribu naye ataweza kuona taarifa na kutakiwa ku allow ili haweze kutumia kitu anachotaka.

Kwaiyo muhusika pia ukimaliza kutumiwa ingia setting>> connected device>> quick share>> utaweza kuingia kwenye link shared history na kuona vitu vyako humo.

Pia unaweza tuma file lenye ukubwa kuanzia 1Gb mpaka 5Gb bila kupunguza ubora.

vipi umeshawahi kutumia hii feature au ndo umesikia Leo Tuachie maoni yako? View attachment 2653713View attachment 2653712View attachment 2653717View attachment 2653714View attachment 2653715
samsung-quick-share-file-transfer-details.jpg
View attachment 2653716
 
Hii Quick Share ni kwa ajili ya samsung devices tu. Kuna ile Nearby Share inayomilikiwa na google ambayo inafanya kazi kwenye simu yoyote ya android
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom