Bahati furaha
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 3,077
- 1,438
VATICAN ni nchi yaliko makao makuu ya Kanisa Katoliki.
Nchi hii ina mambo mengi ambayo yapo tofauti na nchi nyingine duniani. Baadhi ya mambo machache ni haya yafuatayo:
1. Ndio nchi ndogo kuliko zote duniani ikiwa na ukubwa wa 44 hectare(110 acres).
2. Ilikuwa nchi kamili Feb 11, 1929 baada ya Benitto Mussolini(kwa niaba ya Mfalme wa Italy) kutiliana saini na Pietro Gasparri(kwa niaba ya Pope) hivyo kuwa nchi huru ndani ya jiji la Roma.
3. Ni nchi pekee yenye raia ambao uraia wao sio wa kuzaliwa na uraia huo huweza kufikia kikomo.
4. Ni nchi yenye mabalozi nchi za nje lakini mabalozi wanaowakilisha nchi zao huko Vatikani wanaishi Roma.
5. Ni nchi ambayo zaidi ya nusu ya raia wake wanaishi nje ya nchi.
6. Ni nchi pekee yenye waumini wa dini moja.
7. Ni nchi pekee duniani isiyokuwa na mapato yatokanayo na kodi.
8. Ni nchi ambayo raia wake ambae uraia wake umefikia kikomo na akiwa hana uraia wa nchi nyingine, moja kwa moja mtu huyo anakuwa raia wa Italia.
9. Zaidi ya nusu ya eneo lote la nchi hii ni bustani.
10. Benki ya Vatikani ambayo pia hujulikana kwa jina la Institute for Works of Religion inafanya shughuli za kibenki duniani kote ambayo ATM zake zina maelekezo kwa Kilatini tu.
11. Kiongozi wa nchi hii (Pope) ndie kiongozi pekee anaeongoza nchi kifalme baada kuchaguliwa kwa kupigiwa kura.
Yeyote anaruhusiwa kuongeza mengine anayoyafahamu kuhusiana na nchi hii au kunisahihisha kiungwana pale ambapo nitakuwa nimekosea.