Wana MMU, salaam
Nilioa mwaka 1998,nikiwa huko mkoani kwetu. Wakati huo nilikuwa nafanyabiashara za mazao. Mwaka uliofuata Tar.30/08/1999tulipata mtoto wetu wa kwanza wa kiume. Baada ya kupata mtoto,tulikubaliana kupanga uzazi. Tulienda kupata ushauri wa njia bora ya kutumia kupanga uzazi, pamoja na kuelezwa aina zote, njia ya kutumia vidonge ndo ilionekana kuwa nzuri zaidi kulinganisha na zingine.Tangu hapo mke wangu akaanza kutumia hiyo njia tuliyoshauriwa.
Mwaka 2000,kuna shirika moja lisilo la kiserikali lilikuja hapo kijijini kwetu. Vijana wote wenye elimu za kuanzia kidato cha 4 na kuendelea tulipewa nafasi ya kwanza kuajiriwa. Mimi niliajiriwa pia,lilikuwa shirika kubwa na lilikuwa linasaidia jamii ya pale kuondoa umasikini kwa ibua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kushirikiana na jamii. Mimi nilipata nafasi nzuri ya juu kidogo,na mshahara ulikuwa si haba kwa kweli.
Perdiem nayo ilikuwa ya kuridhisha sana,na nilikuwa nasafiri mara kwa mara mikoani. Mambo yakawa yameninyookea sana, ilipofika mwaka 2003, tayari nilikuwa nimemaliza kujenga nyumba yangu nzuri tu kwa wakati huo,ni kipindi hicho tukashauriana kutafuta mtoto mwingine! Wife akaacha matumizi ya dawa zile mwaka 2004.
Mwaka 2005 Tar.08/08.Tulipata mtoto mwingine wa kiume. Maisha yakaendelea vizuri tu. Mwaka 2006,nilipata matatizo ya kikazi na nikasimamiswa kazi! Hapo ndo changamoto zilipoanzia.Kipato kikapungua na niliyumba sana kwakweli. Familia yangu pia haikuwa na utulivu kabisaa! Migogoro kila siku, mpaka nikawa napaogopa hapo nyumbani. Hapo hakukuwa na majadiliano tena ya kupanga uzazi kama awali, mke wangu alikuwa mgomvi kuliko kawaida.
Katika mazingira hayo hayo ya ukata na ugomvi,mke wangu akajikuta na ujauzito mwingine mwanzoni tu mwa mwaka 2007. Ugomvi uliotokea pale,sitasahau katika maisha yangu! Mke wangu alikerwa sana mimba ile na akataka nimpe pesa akatoe ile mimba! Kwanza hela kwangu ilikuwa issue, lakini kutoa mimba pia sikuafiki. Yeye akasema lazima anaitoa hiyo mimba,akaanza kutafuta namna ya kutoa ile mimba.
Alipewa dawa mbalimbali za kienyeji za kujaribu kuitoa ile mimba,kwa vile mke wangu alikuwa mbabe me sikuingilia kabisaa! Huwa sielewi nini kilichotokea, lakini mimba haikutoka. Lakini sisi hatukubaki salama,tukaachana kabisaa. Mimi nikaamua kutimkia hapa Dar. Maisha ni popote,nilipata changamoto za hapa na pale, lakini baadae nikasimama. Huko kwa mke wangu mimba iliendelea kukua na sikumsaidia chochote kwakweli kwa wakati huo. Hali yangu ilikuwa mbaya sana kiuchumi. Hatimae nikapata taarifa amejifungua mtoto mwingine wa kiume tar.11/12/2007.
Baadae mimi maisha yakaanza kuninyookea huku, kwa vile nilikuwa nawapenda watoto wangu,alipofikisha miezi 6 yule mdogo nikatuma nauli mke wangu awalete watoto. Kweli akafanya hivyo, nilikuwa na matumaini kuwa huenda amebadilika ili tuondoe zile tofauti zetu ili tulee watoto wetu,lakini haikuwa hivyo.
Ilikuwa ugomvi mtindo mmoja! Niliishi nae hivyo hivyo kwa kumpotezea. Mwaka 2009 nikiwa kwenye biashara zangu,yeye alikuja na gari pale home akabeba kila kitu, aliacha godoro moja tu,la watoto. Ingawa nilipigiwa simu,lkn sikutaka ugomvi,akaacha chumba cheupe kabisaa! Watoto wote pia aliwaacha.
Haikunisumbua sana,visenti vilikuwepo,nikanunua vitu vingine siku ile ile tu. Nikaanza maisha yangu mapya na wanangu. Nilikuwa tayari nna mtu wa kunifariji ambae nilikuja kumuoa baadae na nipo nae hadi sasa! Kilichonifanya niandike hapa,yule mtoto wetu aliyetaka kutupwa kwa kutolewa mimba,yupo darasa la pili.
Kwenye mitihani ya mwezi huu,amekuwa mtoto wa kwanza kati ya watoto 439. Cha kustaabisha zaidi,amepata alama 690 kati ya alama 700. Ni kiswahili tu alipata alama 90 mengine yote alipata alama 100. Mwalimu aliponipigia nilipata furaha mpaka nikawa natetemeka! Mpaka leo bado sijajua nimpe zawadi gani, nadhani hapa mtanisaidia pia kunishauri nimnunulie zawadi gani. Nataka nikamnunulie leo au kesho.
Nawasilishaa