Miaka 20 ilopita Daslam street haikua na lami. Leo stori ni ingine.
Miaka 20 ilopita ukiwa town ungeona barafu nyingi mlimani. Leo ukiwa town unaona vijibarafu tu.
Miaka 20 ilopita mto karanga ulikua na mimaji. Leo ni kama mfereji.
Miaka 20 ilopita hakukua na Supamaket hata moja. Leo zinaota kama uyoga.
Miaka 20 ilopita Panjwani tu ndo alikua anauza mavifaa ya maana ya umeme. Leo wakibosho nao na masabufa yao wametamalaki.
Miaka 20 ilopita Temba Watch ilikua ndo unapata saa na raba za ukwee. Matajiri tu. Leo Temba watch ni kijiduka.
Miaka 20 ilopita hoteli za Moshi mjini za ghorofa hazikuzidi 5. Kindoroko, Newcastle, Leopard, Buffalo na Zebra. Leo kuzihesabu hadi tume makini iundwe.
Miaka 20 ilopita stendi ya Moshi ilikua tu na baraza ya kusubiria abiria hotel ya Shangazi na maduka ma3 hapo kwa Shazily. Leo ni bonge la shopping mall. Na Morogoro wameiga Moshi.
Miaka 20 ilopita mji wa Moshi ulikua na kasehemu kanaitwa Shaonaro. Leo hakapo.
Miaka 20 ilopita alikua Chrisburger mwenyewe. Leo kuna Mekus, Red Stone, Story Lounge, Black Diamond, Hugos, n.k.
Yote kwa yote, Moshi inapnekana haibadiliki kwa sababu biashara nyingi za miaka hiyo ziko tu hadi leo japo na nyingine zimekuja. So kwa mtu wa zamani akirudi ataenda kulekule. Milans, Chrisburger, KNCU, Panjwaniz, Moshi Drapers, Temba Watch, etc. Labda ataimis Shaonaro na chapati zao.
Jipe Muda utaiona Moshi katika mwanga mpya man.