Maajabu ya mdudu mende

Maajabu ya mdudu mende

Mpauko

R.I.P
Joined
Jan 19, 2019
Posts
2,323
Reaction score
3,451
1.Ni mdudu anayeweza kuishi zaidi ya mwezi bila ya kula chakula chochote. Wana uwezo wa kuishi katika mazingira magumu. Aina moja kwa jina Eublaberus posticus wanaweza kuishi mwaka mmoja kwa kunywa maji pekee

2.Ni mdudu anayeweza kuishi wiki mbili bila ya kunywa maji.

3.Wakati moyo wa mwanadamu ni mmoja wenye chemba nne mende ana moyo mmoja wenye chemba kumi na tatu.

4.Baadhi ya mende wa kike hawaitaji wanaume kuweza kuzalisha mayai hupandana wao kwa wao na kutaga mayai katika kipindi chote cha maisha yao.

5.Mende ana uwezo wa kukaa kwa zaidi ya dakika 40 bila ya kupumua.

6.Mende ana uwezo wa kuishi zaidi ya wiki mbili akiwa amekatwa kichwa.

7.Ana uwezo wa zaidi ya mara 15 ya binadamu wa kuzuia miale mikali ya nuklia isimdhuru na kubaki hai. 8.Mende ni mdudu asiye na mapafu.

9.Ana uwezo wa kuruka maili 3 kwa saa.

10. Badala ya kuwachukia, wanasayansi huwafurahia sana na kuwatumia kwa manufaa ya binadamu. Mwaka 1999, mende walitumiwa na Prof Robert Full katika Chuo Kikuu cha California, Berkley, kumpa wazo la kuunda roboti ya miguu sita iliyosonga upesi na kwa urahisi.

11. Mende wanatumiwa pia katika matibabu. Wanasayansi kwa miaka mingi wamekuwa wakishangazwa na uwezo wa mende kukaa muda mrefu maeneo yenye sumu na uchafu bila kudhurika. Wamegundua kwamba huwa wanatoa kemikali za kupigana na sumu. Leo katika hospitali Uchina, krimu inayotengenezwa kwa kutumia ungaunga wa mende waliosiagwa hutumiwa kutibu vidonda vya moto na pia humezwa kutibu vidonda vya tumbo

Halafu sijui mpuuzi gani alianzisha jina la staili ya kifo cha mende..
 
hapa umeniacha chaka
Noma sana mara ya kwanza kukutana na mende anaye paa ni mzumbe main campus,nilizani ni waluguru wantuchezea kumbe ni kawaida,niliona mende wakubwa weusi pia kipindi hicho,aise waluguru wanafuga Membe sorry Mende.
 
Pamoja na kuwa na sifa zote hizo lakini akigeuka chali tu na akashindwa kurudi kifudifudi ndo basi tena anakuwa hana ujanja wowote zaidi ya kuzidi kuhalalisha jina la style ya kifo chake kwa binadamu hahahaha nowmer na nusu
 
Haha daaah
Pamoja na kuwa na sifa zote hizo lakini akigeuka chali tu na akashindwa kurudi kifudifudi ndo basi tena anakuwa hana ujanja wowote zaidi ya kuzidi kuhalalisha jina la style ya kifo chake kwa binadamu hahahaha nowmer na nusu
 
Hizo zote 11, 12 ni kifo chake tu ndio kina umaarufu,
Yaani ile Mdembendembe, chalii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom