Maajabu ya dunia, Mapacha Wapishana dakika 7 lakini wana Baba tofauti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maajabu ya dunia, Mapacha Wapishana dakika 7 lakini wana Baba tofauti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mike-Austin, May 19, 2009.

 1. Mike-Austin

  Mike-Austin Member

  #1
  May 19, 2009
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Mapacha Justin na Jordan wana baba tofauti, wataambiwa mkasa wao wa ajabu watakapokua Monday, May 18, 2009 6:03 PM
  Mama mmoja mkazi wa Texas nchini Marekani ambaye alitembea nje ya ndoa yake, amejifungua watoto mapacha waliopishana dakika saba lakini cha ajabu ni kwamba mapacha hao hawafanani kabisa baba zao ni tofauti yani mimba moja baba tofauti. Picha za mapacha hao shuka mwisho wa habari hii.
  Madaktari walioachwa midomo wazi na tukio hilo wamesema wana uhakika kwa asilimia 99.999 kwamba watoto mapacha wa mama huyo wenye umri wa miezi 11 sasa wamezaliwa kutokana na baba tofauti.

  Watoto mapacha wa kiume Justin na Jordan Washington walizaliwa wakipishana dakika saba tu lakini wametokana na baba tofauti kwakuwa mama yao alikuwa akitembea nje ya ndoa yake na mumewe James Harrison.

  Akiwa haamini macho yake mama huyo Mia Washington mwenye umri wa miaka 20 alisema "Katika watu wote Marekani na duniani, hali hii imenitokea mimi tu".

  Mama huyo mkazi wa Texas alikiri kutembea na wanaume wawili tofauti wakati aliposhika mimba na ilimbidi akatafute ukweli wa baba wa watoto hao kutokana na mapacha hao kuwa hawafanani hata kidogo.

  Mimba za namna hii hujulikana kitaalamu kama "heteropaternal superfecundation”.

  Genny Thibodeaux, wa maabara ya Clear Diagnostics DNA Lab ambayo iliwapima DNA watoto hao alisema " Ni kitu cha kushangaza, watu wengi hawaamini kama kinaweza kutokea, lakini ukweli ni kwamba inawezekana kuwa na mapacha wa baba tofauti".

  Majibu hayo ya DNA yanaamisha kuwa mapacha hao watakuwa ni ndugu wa baba tofauti.

  Pamoja na mkewe kutoka nje na kuzaa watoto wa baba tofauti, mumewe amesema atawalea watoto wote wawili ingawa mtoto wake halisi ni pacha wa kwanza Jordan
   
Loading...