Maajabu ya ccm mtaa wa migombani

Maajabu ya ccm mtaa wa migombani

CCM walimpenyeza mtu wao ili agombee kupitia ukawa tukamshitukia na wananchi walilijua hilo wakamkataa pia.
Kuna wagombea wawili wa UKAWA. Wa CDM aliyepata kura 547 na nccr aliyepata kura 205, aliyepenyezwa ni huyo wa nccr? Kama ndivyo mbona alipata kura nyingi sana karibu sawa na yule wa ccm!

Hili lapaswa kuwa funzo kwa UKAWA kwa chaguzi zitakazofuata.
 
Kuna wagombea wawili wa UKAWA. Wa CDM aliyepata kura 547 na nccr aliyepata kura 205, aliyepenyezwa ni huyo wa nccr? Kama ndivyo mbona alipata kura nyingi sana karibu sawa na yule wa ccm!

Hili lapaswa kuwa funzo kwa UKAWA kwa chaguzi zitakazofuata.

Hapa wa kujifunza ni CCM walimpenyeza mtu wao mwisho wa siku zikagawanyika kura zao
 
Mtaa wangu huu kabisa;mwaka 2010 walichakachua kura za mgombea Ubunge wetu ni dhahiri kila kituo tulishindia na eneo hilo ni nyeti kimsingi ndio maana Magamba wanakomaa sana;aje John Mnyika atusaidie hapa vinginevyo CCM wahuni sana
 
Last edited by a moderator:
hao watoto wa mahanga na masaburi ni kama akina nani maana najua wote ni walevi mbwa.... kila kitu kiko wazi ushindi ni wa CDM....

Nisaidie kushangaa. Halafu hao kina Mahanga mbona Migombani hapawahusu?
 
CCM haikubariki sema wanalazimisha tu hapo Migombani
 
hivi huyu mtajwa ndo alisema watu wanafikiria kwa MAKALIO?
 
Kuto kusaini kwa mgombea wa NCCR si ajabu kwa sababu makubaliano yalikuwa UKAWA wamsimamishe mgombea mmoja, unapokuta kuna wagombea zaidi ya mmoja wanaowakilisha UKAWA ujue kuna mmoja aliamua kuwa hivyo bila kufuata kanuni na taratibu walizojiwekea. Kama mgombea wa CDM alipata zaidi ya kura 500 ili hali yule wa NCCR alipata kura 205 ni dhairi kwa taratibu walizojiwekea UKAWA ilibidi iwakilishwe na mgombea kutoka CDM. Watu wanaweza kuamua kukomaa tu kwa kushawishiwa na makundi yanayowaunga mkono au kudhani wana watu wa kutosha kuwaunga mkono. Katika siasa hayo ni mambo ya kuyategemea kwa sababu katika kundi la mamba na vijikenge vimo, kama huamini ngoja mwakani CCM watakapokuwa katika mchakato wa kumpata mgombea wao wa nafasi ya Urais watu watafika hadi Bagamoyo kwa babu
 
Mi niulize tu kuwa kwa nini chadema na nccr wote walisimamisha wagombea?

Najua muungano huu unekuja Ghafla na Uchaguzi ulishafika kwahiyo hakukuwa na muda wakutosha kwa Baadhi ya maeneo....kuwekana sawa....! Nadhani kwenye Uchaguzi MKUU hilo hatutalisikia Pamoja hayo ndio maana hatujackia Viongozi wakuu wa UKAWA wakililalamikia hilo Vinginevyo tuweke nguvu ya Pamoja cz Tanganyika bila CCM inawezekana na CCM bila kutegemea Vyombo vya DOLA ni karatasi nyeupe tu.....
 
#WANAWATINGISHA MKILAINIKA TU IMEKULA KWENU KOMAENI PIA KAZENI BUTI,makongoro na mgreada wake huwa anajitapa kila siku KUSHINDA KWAKE SEGEREA NI FEDHA ZAKE NA SI VINGINEVYO,na hiyo ndio ccm ya mashetani HAKI USAWA kwao ni jambo OVU KABISA bali wizi ubabe ni NJIA sahihi./NI WAKATI SASA WA VIONGOZI TAIFA CDM KUPITIA SEHEMU ZOTE KWA KUSHIRIKIANA NA WANASHERIA KUNYOOSHA UPUUZI NA DHULMA HIZI
 
Last edited by a moderator:
Katika uchaguzi uliopita wa serikali ya mtaa katika mtaa wa migombani kata ya segerea Matokeo ni kama ifuatavyo CHADEMA nafasi ya mwenyekiti ilipata kura 547 na CCM ilipata kura 215 na NCCR ilipata kura 205. Uchaguzi wa wajumbe haukufanyika kutokana na kasoro mbali mbali katika karatasi za wagombea ujumbe hivyo ukarudiwa tarehe 21 na Matokeo ni kwamba Wajumbe wa chadema walishinda kwa kura 410- hadi 390 huku wale wa ccm wakipata kura 20-60 mara zote za uchaguzi, ccm waligoma kusign karatasi za Matokeo . Mara baada ya kumaliza uchaguzi ameibuka mtoto wa makongoro Maanga na Masaburi wanatangaza kuwa uchaguzi utarudiwa bila sababu yoyote na mkuu wa mkoa katangaza kurudia uchaguzi siku ya hotoba ya jk na wazee wake. Wanaojua sheria tunaomba mtusaidie ni halali kurudia uchaguzi baada ya kutangazwa ushindi kwa muda wa wiki mbili? Ni nani anyeweza kutengua Matokeo kisheria baada kutangazwa kisheria? Nimeambatanisha karatasi za Matokeo yote
Uzoefu umeonyesha..,kadri uchaguzi unavyorudiwa ndio kura za CCM zinazidi kupungua..,wacha warudie alafu uone kama watapata hata kura 10.
 
Huyu jamaa wa NCCR alitoka CCM akataka kugombea kama ukawa tukamtosa, sasa hivi yuko pamoja na CCM kutaka uchaguzi urudiwe kienyeji.

Hongereni kwa kumstukia mamluki... Je ilikuwaje NCCR wanaendelea kumlea na kumpatia mpaka muhuri?
Siyo siri hapo kutakuwa na hujuma nzito.
 
Ukizoea Wizi/ujambazi Siku Ukikosa Cha Kuiba Utavizia Kama Kuna Mtu Ili Ujiibie Mwenyewe.Hiyo Ni Sifa Kubwa Ya CCM, WIZI!
 
Fomu za huyo mgombea ziliidhinishwa na ccm?

Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo, huyu jamaa huwezi amini ukweli ni kwamba fomu zake ziliidhinishwa na mkewe ambae alimpa cheo cha ukatibu wa chama.
 
Hawajasaini so wanahaki ya kwanza mahakamani lakini sio mkuu wa mkoa kutangaza marudio,ni mahakama pekee itakayoamua matokeo yakisha toka.
 
Hata mimi naweza kutengeneza hizo form nikajaza mwenyewe na ku sign.
 
Hongereni kwa kumstukia mamluki... Je ilikuwaje NCCR wanaendelea kumlea na kumpatia mpaka muhuri?
Siyo siri hapo kutakuwa na hujuma nzito.

Kwa kweli hilo ni swali la kujiuliza ilikuwaje nccr kumgongea mhuri wa chama kuidhinisha fomu yake ya ugombea huku wakijua yupo aliepitishwa na ukawa? Ilikuwaje msimamizi wa uchaguzi nae asigundue hii dosari? Upumbavu huu ndio uliowasababishia upinzani kwa maana ya ukawa mapingamizi hadi yanatia kichefu chefu. Endeleeni na ujinga wenu wa kujisikia muone 2015 kama hata wabunge wenu hawajaondolewa kwa mapingamizi.
 
Historia ya mtaa wetu ilikua inampa Japhet nafasi kubwa ya kushinda. Yani Chadema hata wangeweka jiwe lingepita. Mwenyekiti aliyetoka (Binagi ambaye pia ni ndugu wa kina Mahanga na Masaburi) aliharibu sana, Mahanga ni mbunge jina tu hakubaliki, yupo kitaifa zaidi bunge kaligaya kisa uchaguzi uliopita watu walimpa Mpendazoe.
 
Back
Top Bottom