The Certified
JF-Expert Member
- Feb 10, 2016
- 910
- 773
Ukuaji wa teknolojia unazalisha stori mpya kila siku ila leo huenda ukashtuka; unajua simu yako inaweza kukwambia siku yako ya kufa?
‘Macabre iPhone App’ ni application ambayo unaweza kuiweka kwenye simu yako na jukumu ambalo utakuwa nalo ni kuweka ratiba zako zote za siku nzima, application hiyo inapiga hesabu halafu inakupa majibu siku zako ngapi zimesalia kuishi duniani.
Kali zaidi ni kwamba majibu utakayopewa ya idadi ya miaka, miezi, wiki, siku na saa itakuwa inaonekana kwenye screen lock, kwa hiyo kila unapotoa lock ya kwenye screen itakuwa inaonekana hapo juu.
Majukumu yako ya siku ndiyo yataakayoamua siku ngapi utaishi.
Application hiyo inapatikana kwa simu za Apple zinazotumia iOS na Windows 8.
Unadhani uko tayari kuitumia application hii?