Maajabu: Twalaumiwa siye badala ya waliomfunga?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,186
103,702
Zile mamlaka zinazotathmini maaajabu ya dunia wanatakiwa kuchukua hili kama ni moja la ajabu duniani. Sio lazima liwe kati ya maajabu nane ila liwe tu hata ajabu la 98.

Scenario 1
Mtu anaamini Mh.Freeman Mbowe sio gaidi wala hana kosa. Anaamini anatakiwa kuwa huru kwa hali na mali. Anaamini waliomfunga wanamuonea kwa sababu za kisiasa.

Ajabu ni kwamba mtu huyu anatutaka siye tumbembeleze aliyemfunga Mbowe ili amuachie huru. Anatulaumu kwa nini tunachochea Mbowe akaze hakuna kuomba msamaha? 😥😥😥

Nasema anaamini Mbowe sio gaidi kwa sababu kama ni gaidi kweli kweli kwa nini anataka tumuombee Mbowe msamaha? Kama Mbowe ni gaidi si inabidi apigwe mvua za kutosha? Magaidi mfano wa Osama Bin Laden au Mullah Omar huwa wanatakiwa wawe Guantanamo Bay wasije wakalipua mabomu.

Kama unaamini Mbowe ni gaidi lakini unataka aombewe msahama, basi inabidi upimwe akili. Gaidi linaachiwa kwa kuombewa msahama? Yaani Gaidi la Alshaab likamatwe halafu Wasomali waanze kupaza sauti kuliombea msahama,wakati linataka kuwaua? Utakataa tukikupima akili?

Ajabu ni kwamba inashangaza mtu huyu badala ya kumlaumu yule aliyemfunga Mbowe kwa hila,analaumu wanaomlaumu aliyemfunga Mbowe.

Scenario 2
Lawama hizi kwetu zimechochewa na hukumu ndogo ya jana kwamba Mbowe ana kesi la kujibu. Wanasema makelele yetu yamemfanya jaji akaze.

Kwa hiyo mtu huyu anaamini kabisa ule ushahidi wa upande wa mashtaka hauna vigezo vya kumkuta mtu na kesi la kujibu.

Ajabu ni kwamba mtu huyu anatulaumu siye kwa nini hatuwi wapole yaishe ili Jaji alegeze?

Ajabu ni kwamba mtu huyu ameacha kumlaumu Jaji anayeaminisha watu juu ya ushahidi wa uongo anatulaumu siye tunayemlaumu Jaji,kama yeye.

Nasema mtu huyu anaamini hakuna ushahidi wa kumkuta Mbowe na kesi la kujibu kwa sababu kama Mbowe ana kesi kwa nini utulaumu siye? Kwa nini usione gaidi kakutwa na kesi ya kujibu?

Niwashauri waTz wenzangu lengeni mzizi wa tatizo sio kupaparika na watu wasiostahiki lawama. Hali hii inaonyesha unyonge wa kuzidi kipimo na tunaonekana taifa la hovyo kuliko mfano.

Kama sio taifa la watu wa hovyo, kwa nini umlaumu mtu anayekataa kulamba viatu au makalio?! Mtu huyu anatakiwa kupongezwa na kuungwa mkono
 
Serikali ya Tanzania ina utani sana na hizi siasa zake za ugaidi! Kama Mbowe angekuwa kweli ni Gaidi, wale Mabalozi wasingekuja mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi.

Hii kesi kama alivyosema ndugu Kaaya, ni kesi ya mchongo! Na huu ndiyo ukweli mchungu. Chief Hangaya naye akubali tu ukweli! Alilishwa matango pori.
 
Jela sio kuzuri ndugu zangu yawezekana mbowe anahitaji kutoka kule kwa namna yoyote afu uku nje chadema mnakaza oh ivi mala vile nw ww hujiulizi why lisu na rema wanaishi uhamishoni afu wanakomaa jamaa afungwe chadema lazima mulaumiwe kwa namna moja au nyingine .
 
Hakika jela sio kuzuri. Unatutaka tufanye nini ili kunusuru Mbowe asiende jela
 
Huwezi kujua kiatu wapi kinabana mpaka ukijaribu.
Take a walk in my shoes .I bet you will fall on your first step.Ni msemo wenye maana sana.
Hawa keyboard warriors wangekaa jela hata mwezi usingesikia hizi kauli za kumwambia Mwamba komaa hivyo hivyo.
We must come to our senses and end this saga.
Mwamba anahitajika kwenye familia yake .Tuache ushabiki na malumbano kwenye maisha ya mtu.
Guys cool down huu ushabiki na uharakati wa pande zote mbili haumsaidii Mwamba na wenzake.
Kesi hii imejaa sana ushabiki wa kisiasa.
 
Mkuu nyoosha maelezo badala ya risala na kingereza kingi. Tumia maneno machache tu;
1. Unataka mwamba afanye nini
2. Unataka wafuasi wafanye nini
 
Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa w South Africa wote wangekaa jela kama Mandela ili kuonesha uchungu wao. Lazima mmoja au wawili wawakilishe.
 
Msimamo wa Mbowe katika hili ni upi??

1. Je yupo tayari kuomba radhi??

2. Je yupo tayari kuendelea na kesi ili ajisafishe kupitia mahakama??

Je mawakili wake wametoa statement gani kuhusiana na mambo hayo??
1. Anaombaje radhi? Kwamba mnisamehe kweli nilitaka kulipua ila sirudii tena? Yaani haiji kichwani aisee. Aliyemshitaki ndo aombe radhi kuwa alidanganywa basi.
 
Hayo ni mawazo yako

Yeye mwenyewe anasemaje??
 
Mkuu nyoosha maelezo badala ya risala na kingereza kingi. Tumia maneno machache tu;
1. Unataka mwamba afanye nini
2. Unataka wafuasi wafanye nini
Mwamba hana la kufanya yupo jela.Wafuasi na washiriki watumie muda wao kwenye kumtafutia huduma anazozihitaji mahakamani. Kisheria.
Kupiga kelele na kuanzisha malumbano yasiyokuwa na tija haisaidii.
Nikupe mfano rhetoric kama za Katibu Mkuu tutaivua serikali nguo zinamsaidia nini Mwamba?
Huu ni wakati mgumu .Ni wakati wa viongozi waliobaki waonyeshe ukomavu.
Sisemi watu wa give up bali watumie akili zaidi.
 
Jela sio kuzuri ndugu zangu yawezekana mbowe anahitaji kutoka kule kwa namna yoyote afu uku nje chadema mnakaza oh ivi mala vile nw ww hujiulizi why lisu na rema wanaishi uhamishoni afu wanakomaa jamaa afungwe chadema lazima mulaumiwe kwa namna moja au nyingine .
Chadema wanakaza kwa sababu hawaoni ushahidi uliojitosheleza kumtia mwamba hatiani
 
Mwamba hana la kufanya yupo jela.Wafuasi na washiriki watumie muda wao kwenye kumtafutia huduma anazozihitaji mahakamani. Kisheria.
Kupiga kelele na kuanzisha malumbano yasiyokuwa na tija haisaidii.
Nikupe mfano rhetoric kama za Katibu Mkuu tutaivua serikali nguo zinamsaidia nini Mwamba?
Huu ni wakati mgumu .Ni wakati wa viongozi waliobaki waonyeshe ukomavu.
Sisemi watu wa give up bali watumie akili zaidi.
wewe na mimi tunaongea lugha moja
 
Back
Top Bottom