Maajabu na misimamo kuntu ya Rais Buhari wa Nigeria

Maajabu na misimamo kuntu ya Rais Buhari wa Nigeria

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,092
Reaction score
7,236
Miaka ile ya 1980 nilikuwa nasoma sana magazeti ya kimataifa kama ‘Africa,' ‘Africa Now,' ‘Africa Events' na mengineyo yaliyoruhusiwa kuingia nchini.

Haikuwepo mitandao ya kijamii kama ilivyo leo wala mawasiliano ya kompyuta, hivyo tulipata habari nyingi za kimataifa kupitia magazeti ya kimataifa.

Ni katika magazeti hayo, nilisoma habari za mwanajeshi mwenye cheo cha Meja Jenerali, Muhammadu Buhari aliyeingia madarakani nchini Nigeria kwa mapinduzi Desemba 31, 1983. Miaka miwili ya utawala wake ilikuwa michungu kwa wafanyakazi, madereva na wakorofi.

Siku chache baada ya kuweka mambo sawa yaani kuunda Baraza la Kijeshi, ‘mjeshi' huyo alifanya ziara kwenye kampuni moja ya umma (nadhani ya mafuta), ambapo yeye na msafara wake walifika mapema kabla ya baadhi ya wafanyakazi na wakurugenzi.

Hakuwaacha hivi hivi, aliamuru wanajeshi kuwachapa viboko wote waliochelewa kufika.

Buhari aliruhusu wanajeshi kwenda barabarani kufanya kazi ya Askari wa Usalama Barabarani. Tofauti yao ni kwamba wao, hawakuwa wanasimama kuruhusu magari kupita bali walikuwa wanawafuata madereva wanaokiuka sheria na kuwacharaza bakora sawasawa. Halafu aliwatawanya askari kwenye ofisi za umma ambako wafanyakazi waliojijengea utamaduni wa kuchelewa kazi walikula bakora.

Huyo ni Muhammadu Buhari wa wakati ule. Niliposikia ametangazwa mshindi wa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu wa kidemokrasia Nigeria hivi karibuni, haraka nilikumbuka bakora kwa madereva, kurushwa kichura kwa maofisa kama adhabu kwa kuchelewa kwao na kuamuru kunyongwa wauzaji ‘unga' na kulazimisha usafi kwa kuwatia jela vikojozi wa barabarani.

Ingawa kuna watu walifurahia alivyosimamia nidhamu, wanajeshi wenzake walimpindua mwaka 1985 na akazuiwa nyumbani kwake. Najiuliza, mjeshi huyu hatapenda kuchota mambo ya zamani na kuyatumia sasa akiwa rais wa kuchaguliwa?

Wampenda, wamgeuka


Siku za mwanzo za utawala wake, wananchi walimfurahia Buhari aliyetarajiwa kuondoa matatizo makubwa ya kiuchumi yaliyokithiri wakati wa utawala wa kiraia wa Shehu Shagari, lakini hatua kali alizochukua kukomesha uzembe, kufukuza wahamiaji, kucharaza viboko maofisa, alikasirisha wengi.

Ilionekana wananchi walihitaji mabadiliko makubwa ili kuondoa dhuluma, ufisadi, uzembe, utovu wa nidhamu uliokithiri enzi za Shehu Shagari, lakini alipoanzisha kampeni iliyoitwa "Vita Komesha Utovu wa Nidhamu" ambayo iliwagusa wanasiasa na wafanyabiashara wengi, wakashitakiwa kwa rushwa kwa lengo la kuipa heshima Nigeria, alichukiwa.

Utawala wake ulizuia uhuru wa habari, vyama vya siasa na vyama vya wafanyakazi. Hivyo, alipopinduliwa Agosti 27, 1985 na ‘mjeshi' mwingine Meja Jenerali Ibrahim Babangida, wengi walipokea habari hizo kwa shangwe. Baada ya kupinduliwa alizuiliwa nyumbani kwake katika mji wa Benin hadi mwaka 1988.

Buhari hakupotea kwenye siasa, alianza kufuata nyayo za mwanajeshi mwingine Olusegun Obasanjo, ambaye baada ya kutawala kijeshi kuanzia Februari 13, 1976 hadi Oktoba 1, 1979 alirejea kutawala kama raia kuanzia Mei 29, 1999 hadi Mei 2007. Hali hiyo ilimvutia Buhari, akawania urais kama raia mwaka 2003 lakini aliangushwa na Obasanjo wa chama cha People's Democratic Party (PDP).

Matokeo yalimpa hamasa ya kugombea tena mwaka 2007 na aliangushwa na mgombea wa PDP, Umaru Yar'Adua katika uchaguzi ambao mchakato wake ulishutumiwa na waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa kwamba ulitawaliwa na ukiukwaji wa taratibu. Hakukata tamaa, alijitosa kwa mara ya tatu, mwaka 2011 pia alipigwa mwereka na Goodluck Jonathan wa PDP.

Udhaifu alioonyesha Jonathan katika kupambana na rushwa na zaidi vita dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram, ulitumiwa na Buhari kama mtaji wa kisiasa. Mwaka 2014 aliteuliwa na Chama cha All Progressives Congress (APC) kuwa mgombea urais uliopangwa Machi 28, 2015. Vitu vilivyomwongezea mtaji na mvuto kwa wapigakura ni heshima aliyojijengea kwamba si fisadi, kwamba kati ya madikteta waliotawala Nigeria, yeye hakuwahi kufuja fedha za umma.

Aliwahi kuwa mkuu wa nchi akiwa na magwanda na kwa sasa wanaamini kuwa ataweza kupambana na Boko Haram.

Japokuwa kulikuwa na wagombea wengine 14 wa urais, ushindani ulikuwa kati ya Buhari na Jonathan wa PDP. Jonathan aliangushwa na Buhari kwa tofauti ya kura milioni 2.5. Kwa anguko hilo, Jonathan amekuwa rais wa kwanza kushindwa katika uchaguzi na kukabidhi madaraka kwa amani.

Changamoto


Buhari amerithi mikoba ya Jonathan huku nchi ikiwa inakabiliwa na changamoto kadhaa na kubwa zaidi ni usalama (kupambana na Boko Haram), kushuka bei ya mafuta (asilimian 70 ya mapato ya Serikali yanatokana na mafuta), na kushuka thamani ya naira (fedha za Nigeria).


General_Buhari_s_First_Speech_after_the_Military_Coup_of_31st_December_1983_The_Niger_Times.jpg


General-Muhammadu-Buhari.jpg
 
Akipatikana rais wa mtindo huu hapa Tanzania itasaidia sana kurudisha nchi njia kuu , maana imezid kuwa nchi ya michepuko kila sekta.
 
Last edited by a moderator:
Tunapaswa kupata rais wa namna hii mwenye msimamo,uwezo wa kufanya maamuzi na awajali wananchi wake na si marafiki zake.
 
Tunapaswa kupata rais wa namna hii mwenye msimamo,uwezo wa kufanya maamuzi na awajali wananchi wake na si marafiki zake.

kweli kabisa...mkuu umenena vema kwani kipindi hiki cha migomo hakika kina samwel sitta na makonda wangerambwa bakora bara bara kwa uzembe wa kushindwa kutatua kero
 
Akipatikana rais wa mtindo huu hapa Tanzania itasaidia sana kurudisha nchi njia kuu , maana imezid kuwa nchi ya michepuko kila sekta.

Tena ingekua vizuri zaidi mana kila sector mambo hayaendi inavotakiwa hakuna kujituma kila mahali. Angenyoosha wote waliopinda ili nchi inyooke vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Tayari Boko Haramu wameachia sehemu kubwa ya watu waliowateka ikiwemo wasichana.
 
Asitoke ccm wote wamechoka vichwa hawajui wafanye nini migomo inatatuliwa na wapinzani. Shame on CCM na Rais wao
 
Tena ingekua vizuri zaidi mana kila sector mambo hayaendi inavotakiwa hakuna kujituma kila mahali. Angenyoosha wote waliopinda ili nchi inyooke vizuri.

Kweli kabisa , yaani angenyoosha wahuni wahuni wote kama kina kabaka mpaka wangekoma nae.
 
Tayari Boko Haramu wameachia sehemu kubwa ya watu waliowateka ikiwemo wasichana.

kweli kabisa mkuu , mpaka mimi nikawa nina jiuliza hivi huyu Goodluck Jonathan alikuwa akiwagwaya hao Boko Haramu au alikuwa bado yupo yupo kwanza. Coz jamaa kaingia tu ndani ya muda mfupi jamaa wanapewa kipondo cha mbwa koko na kutokoma mbali,.
 
Kweli kabisa , yaani angenyoosha wahuni wahuni wote kama kina kabaka mpaka wangekoma nae.

Mana mazoea yamezidi mno kwa mambo muhimu kwa taifa, kila kitu utani Mara ufisadi hakuna uwajibikaji, uhuni uhuni mwingi, Nadhani tunahitaji mtu wa kutushtua na kutuamsha akili ichangamke na kuwa Sawa ndo itasaidia kuliokoa hili taifa.
 
Mana mazoea yamezidi mno kwa mambo muhimu kwa taifa, kila kitu utani Mara ufisadi hakuna uwajibikaji, uhuni uhuni mwingi, Nadhani tunahitaji mtu wa kutushtua na kutuamsha akili ichangamke na kuwa Sawa ndo itasaidia kuliokoa hili taifa.

Tujitahidi tuchague watu wa aina ya Buahari ili kuondoa makapi yote ya namna hii.
 
i wish you could be in tanzania!!! but anyway i see your copy is rising from north!!!!!
 
Back
Top Bottom