Maajabu mengine Tanzania, sheria zimekaaje?

Maajabu mengine Tanzania, sheria zimekaaje?

Mjamaajr

Senior Member
Joined
Nov 13, 2013
Posts
110
Reaction score
82
Habari wanajf..

Leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kwenda Jela miaka Mitatu waliokuwa mawaziri wa nchi hii kwa kosa la kusamehe kodi ambayo ingesaidia wananchi kujikwamua kutoka kwenye umasikini.

Hilo sio ajabu nilichoshangaa mimi kitendo cha vijana wawili mkoani Kagera kuhukumiwa Miaka 30 Jela kwa kosa la wizi wa mali ya Tsh 16m .
Sasa sijui sheria zimekaaje hapo yaani hata sielewi labda mnisaidie.
 
Ni ngumu sana kupata haki ukingali duniani na zaidi sana ukiwa masikini.
 
Habari wanajf..

Leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kwenda Jela miaka Mitatu waliokuwa mawaziri wa nchi hii kwa kosa la kusamehe kodi ambayo ingesaidia wananchi kujikwamua kutoka kwenye umasikini.

Hilo sio ajabu nilichoshangaa mimi kitendo cha vijana wawili mkoani Kagera kuhukumiwa Miaka 30 Jela kwa kosa la wizi wa mali ya Tsh 16m .
Sasa sijui sheria zimekaaje hapo yaani hata sielewi labda mnisaidie.

Waliohukumiwa miaka 30jela, walihukumiwa kwa kosa gani? Na waliohukumiwa miaka 3jela walihukumiwa kwa kosagani?!
 
sheria zimetungwa kwa malengo ya kumkandamiza watu wenye vipato vya chini
 
Habari wanajf..

Leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kwenda Jela miaka Mitatu waliokuwa mawaziri wa nchi hii kwa kosa la kusamehe kodi ambayo ingesaidia wananchi kujikwamua kutoka kwenye umasikini.

Hilo sio ajabu nilichoshangaa mimi kitendo cha vijana wawili mkoani Kagera kuhukumiwa Miaka 30 Jela kwa kosa la wizi wa mali ya Tsh 16m .
Sasa sijui sheria zimekaaje hapo yaani hata sielewi labda mnisaidie.

katiba yetu inahtaji mabadiliko sana yani wezi na waliotia hasara isiyosahaulika taifa wanabembelezwa mwishoni unambiwa wamefungwa miaka 3...KWELI ALIYETULOGA KAFARIKI...
 
Ni kwamba hujasoma au macho yako yanachagua mahali pa kusoma?!

hujamwelewa G.25 inawezekana hao jamaa wakati wanaiba walitumia nguvu kwa kumkaba mtu au walitumia silaha kwenye wizi wao, halafu ukakuta hao mawaziri wakashitakiwa kwa kusamehe kodi na kuisababishia serikali hasara, lakini huwenda kwenye kodi aliyoisamehe kuna maeneo serikali ilipata faida ingawa faida iliyopatikana hailingani na hasara ambayo imepata pia usisahau suala la wao kusamehe kodi wameruhusiwa kisheria, halafu kuna suala la kuthibitisha pasipo kuwa na Shaka kuwa walisamehe kwa makusudi kwa manufaa yao wenyewe hapo ndipo Mara nyingi inakuwa ngumu kuthibitisha kisheria, halafu ujue fisadi ni mtu aliyesoma na huwa anasoma sheria inataka nini kabla hajaiba ili siku likibuma atakwepa vipi mkono wa sheria, nitakupa mfano mdogo kwenye kesi ya zombe ya mauaji ya wafanyabiashara zombe alijua sheria inasema ili yeye zombe akutwe na hatia ilibidi kwanza yule aliyeshika bunduki na kufyatua risasi na kuwauwa wale wafanyabiashara aithibitishie au ushahidi uthibitishe kuwa ye ye ndiyo aliyeua, halafu aliyeuwa atoe maelezo kuwa aliua kwa shinikizo au maelekezo ya zombe ndipo zombe angeingia hatiani na angekuwa na mashitaka ya kujibu, kwa maana hiyo wakaelewa Kama watafanikiwa kumkimbiza aliyeshika bunduki na kuua hakuna mtu atakaye thibitibitisha tena, jamaa alikimbia au alikufa na kuzikwa kwenye unmarked grave, baadae wakaona Yule dereva anaweza kuzingua siku ya kwenda mahakamani akaumwa baada ya muda akafa kukawa hakuna mtu yeyote atakaye thibitisha kuwa zombe alitoa amri ya kuuawa kwa wafanyabiashara wale, viongozi was nchi hii ukitaka uwaweze uwafanyie kama walivyomfanyia ditto anamalizana na mganga kimyakimya.
 
Back
Top Bottom