Maajabu: Mbwa achaguliwa kuwa Mayor Marekani

Maajabu: Mbwa achaguliwa kuwa Mayor Marekani

Behaviourist

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2016
Posts
39,924
Reaction score
95,763
mayor_duke.jpg

Mbwa mmoja katika jimbo la Minnesota, Marekani amechaguliwa kuwa meya wa mji mmoja katika jimbo la Cormorant.

Mbwa huyo kwa jina Duke (pichani) ana umri wa miaka tisa na amechaguliwa mara ya kwanza kuwa meya wa mji wa Cormorant mwaka 2014, kwa mujibu wa kituo cha habari cha WDAY kituo ambacho kina ushirikiano na shirika la habari la ABC.

Mpinzani wake katika uchaguzi huo, Richard Sherbrook, alipata kura mbili au tatu kati ya kura zote 12.

Wadhifa wa Meya wa Cormorant huwa wa staha na watu huhitajika kulipa dola moja ili waruhusiwe kupiga kura.

Mmiliki wa mbwa huyo, David Rick aliwaambia wanahabari kwamba mara ya kwanza mbwa huyo kuchaguliwa ilikuwa kibahati lakini baadaye ameibukia kupendwa sana na wakazi.

"Kila mmoja alimpigia kura Duke, isipokuwa mtu mmoja aliyempigia kura mpenzi wake Duke, Lassie," Rick aliambia WDAY.

Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2014, watu 12 walishiriki.

Mji huo, ambao kwa mujibu wa ABC News ulianzishwa 1874, kwa sasa una wakazi takriban 1,000.

Kuchaguliwa kwa Duke kuwa meya wa Cormorant miaka miwili iliyopita kulitokea siku chache baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa meya wa mji jirani wa Dorset, Robert Tuff, mvulana wa miaka mitano, baada ya kuhudumu kwa miaka miwili.

"Hakuna mtu angeweza kunikamata, hata maafisa wa polisi," alisema Tuff wakati wa kuondoka kwake, akisema alifurahia sana kipindi chake madarakani.

Alimwachia majukumu Eric Mueller, 16.

Duke si mnyama wa kwanza kuchaguliwa kuongoza. Miaka karibu 20 iliyopita, paka kwa jina Stubbs alichaguliwa meya wa mji wa Talkeetna katika jimbo la Alaska.

Mji huo unapatikana kilomita 185 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Anchorage.

Chanzo: Mwananchi

 

Attachments

  • 1475670914125.jpg
    1475670914125.jpg
    72.8 KB · Views: 41
Some times idont believe that i am belong in to this
 
Nadhani tunahitaji ufafanuzi zaidi. Je sheria za huko zinaruhusu wanyama kuongoza watu!? Nini majukumu ya meya huko? Je mbwa anayetekelezaje majukumu yake ya umeya?
 
Aliejiuzuru alikuwa na.miaka5....

[emoji1] [emoji1] [emoji1]
Ila.jamaaa aliepambambanishwa.na.mbwa na.kushindwa nae anatia shaka
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] kama ni kweli bac mayor kwenye huo mji hana kazi zaid ya cheo tu
 
Back
Top Bottom