MAAJABU mambo 6 ya kufahamu kuhusu sayari ya Venus iliyopo karibu na dunia

marcs

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
1,067
570
9ef378eecec3e610b899d3ecd26b8c41.jpg

5953ba28498aaa65827083404902a5e3.jpg
2b80e4f5af9db0883e1d02e1297e6d6b.jpg
563cace3c1a0e7e1f8ef7b955579066e.jpg
 
9af8209f9a62c564315b3691aca31d8e.jpg
najua utakua umesikia mara nyingi kuhusu wanasayansi na watafiti wa masuala ya anga wakitoa taarifa mbalimbali kuhusu kilichopo kwenye Sayari nyingine ukiacha Dunia. Leo Nakusogezea mambo 6 muhimu ya kufahamu kuhusu jinsi ilivyo Sayari ya Venus ambayo ipo jirani na dunia ukubwa wake unafanana na dunia ila tu ina mazingira tofauti na ni hatari.
92f7f662e751a596d647a060da74988f.jpg
sayari ya pili kutoka kushoto ndio Venus

Kwa mujibuwa shirika la utafiti wa masuala ya anga la nchini Marekani NASA, nimeyapata mambo 6 kuhusu Sayari ya Venus.

Sayari ya Venus ina unga sumaku mdogo kuliko dunia. Inaelezwa kuwa uchache wa ungasumaku husababisha mionzi ya anga ya jua kuingia kwenye angahewa, na mionzi hiyo huzalisha umeme kutokea kwenye mawingu.
Venus ina volkano nyingi zaidi kuliko sayari nyingine yoyote ya mfumo wa jua. Wanasayansi wamegundua aina za volkano 1600 kwenye sayari hiyo.
Venus ikizunguka yenyewe kwa mzunguko mmoja inahitaji siku 243 za dunia, na ikizunguka jua kwa mzunguko mmoja inahitaji siku 224.7 kwenye dunia. Unaona sentensi hii ni ngumu kuielewa? Hii inamaanisha kuwa kwenye sayari hiyo siku moja ni ndefu zaidi kuliko mwaka mmoja!
Asilimia kubwa ya hewa kwenye Venus ni Carbon Dioxide, ambayo inasababisha sayari hiyo kuwa na joto kali, ambalo kuna wakati hufikia nyuzijoto 470 sentigredi.
Mgandamizo wa hewa kwenye Venus ni mkubwa mara 90 ya ule wa dunia, na karibu sawa na mgandamizo wa maji kwenye kina cha kilomita 1 chini ya bahari.
Venus ni sayari yenye vimbunga vingi. Mwendokasi wa upepo wa sayari hiyo unaweza kufikia kilomita 724 kwa saa, ambao ni mkubwa zaidi kuliko mwendokasi wa kimbunga kikubwa zaidi duniani.

November 19,2016
Sijakuelewa mzunguko mmoja wa siku za Dunia ni 243 na Jua 224.7 ina maana gani naomba unifafanulie?
 
Safi sana kwa kutufahamisha vzr.
 
Asante sana mkuu..... Na pia wanasema kua pamoja na mercury kua iko karibu sana na jua ila venus ndo hottest planet cjuh n kwanini ila
 
Inamaana Venus huzunguka kwenye mhimili wake kwa muda tofauti lakini pia huzunguka jua kwa muda tofauti? Nifafanulie tafadhali.
 
tungekuwa tunaish huko yaan kumumba wangetawala karne na karne uzao wetu ungeendekea kuwa maskini..maana tangu mkolon aondoke mpk leo cjui ingekuwa miaka mingapi
 
Naongeza kidogo dunia inapouzunguka muhimili wake au nguzo yake mzunguko mmoja ikifika ilipoanzia itakuwa imechukua masaa 24 sawa na siku 1. Utakuwa umepata usiku na mchana
Kwa venus ikiizunguka muhimili au nguzo yake ikifika ilipoanzia itakuwa imechukua siku 243 za dunia,ikumbukwe hii ni mizunguko ya kuizunguka mihimili au nguzo zake c kulizunguka jua maana yake kuna mizunguko miwili
1. kuizunguka mihimili yake au nguzo zake
2. Kulizunguka jua usichanganye mizunguko
Kulizunguka jua dunia hutumia siku 365 sawa na mwaka 1 maana yake dunia ifike ilipoanzia

Venus ikilizunguka jua ikifika ilipoanzia itakuwa imetumia cku 224.7 za dunia
Maana yake mwaka wa venus ni mfupi kuliko wa dunia
Na kwamba venus ina speed kulizunguka jua kuliko dunia
Na kwa mahesabu ya kuizunguka mihimili dunia ina speed kuliko venus
Nafikiri mkuu umenielewa nimeeleza kwa kirefu kama kuna wanaofaham zaid waongeze elimu haina mwisho
 
Back
Top Bottom