Kama tunaongelea utendaji kazi katika baraza hili la Mawaziri la Jakaya Mrisho Kikwete, no doubt, Prof. Muhongo ranks top. Nasema hivyo kwa dhamira hasa. Ni Waziri pekee ambaye hana unafiki wala kutafuta kujipendekeza kwa yeyote, huwa anasema kile kilichopo moyoni mwake na kile anachokiamini.
Ni bahati mbaya sana Watanzania tumezoea unafiki, tunapenda sana kusifiwa hata tusipostahili. Professor Muhongo, kwa kauli zake amewaumiza wengi, hasa wanaoamini kuwa huwa hawatakiwi kuambiwa ukweli katika udhaifu wao.
Ningetamani sana kama siku moja tutakuwa na baraza la Mawaziri lenye mawaziri wote wa namna ya Muhongo. Tukifikia hapo nidhamu ya utendaji kazi serikalini itarudi. Kwa sasa Muhongo ana maadui wengi, kuanzia wizarani pake kwa sababu ni mwepesi sana wa kuwaambia anayoamini ni mapungufu yao, na anapotamka hamung'unyi maneno.