Ni ujinga uliopitiliza na kujitoa fahamu kudhani kuwa wawekezaji kutoka nje ya nchi ndo wana umuhimu...
Kwamba wawekezaji kutoka nje ndo wanaweza kutusaidia kuwa kwenye uchumi wa kati.... Viongozi na wakubwa serikalini wamepigwa upofu. Kwa makusudi wanashindwa kujifunza kutoka kwenye uwekezaji wa madini, samaki, utalii, n.k.
Ninachofahamu ni kuwa kinachotetewa hapa ni rushwa ya 10%..... Shangaa uwekezaji mkubwa hivi unapigiwa chapuo ufanyike kwa misingi ile ile ya usiri baina ya mwekezaji na 'aliyemleta'!!
Uchumi imara; uchumi endelevu ni ule unaomilikiwa na wazawa... Nchi isiyowawezesha wananchi wake kutumia rasilimali zake kushikilia vyanzo vya uchumi na kuleta maendeleo itazidi kudumaa miaka nenda rudi!!
Kwa stahili hii ya kuwatetea wawekezaji wa kimataifa tena kwa jazba, kiburi, dharau dhidi ya matakwa ya wazawa... nchi haitapata manufaa ya maana...!!
Wajanja wachache watapiga hela ña kutajirika kutipitia rasilimali za wote kwa manufaa yao na ya ndugu zao!!