Maajabu: kwa miaka zaidi ya 20 jana maji yamekatika kijijini kwetu

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,967
6,464
Wakuu nawasalimu

Kijijini kwetu, mkoa wa kilimanjaro, ndani kabisa kijijini

Kwa miaka zaidi ya 20, tumekuwa tukipata maji safi ya bomba kabisaa, hayajawahi kukatika.
Safari hii kumetokea hitilafu kwasababu ya mvua kuwa nyingi mwaka huu.
Miaka 20 na zaidi

Ni maajabu haya!!!!
Wazee wangu watapitia wakati mgumu wa maji wiki hii ambapo wanafanya marekebisho.
 
Huku daslam toka aingie Mkumbo kitila maji hayajakatika aisee
Ule mgao wa maji umepotea kabisa
 
20 years bila maji kukatika kijijini wakati kwetu mkoani hakuna hata kipande cha bomba. Hongereni, halafu MTU anataka ulinganishe maendeleo na kwetu.
Tunaaka SAA tisa usiku kusaka maji tunarudi SAA NNE asubuhi.
Tutasoma SAA ngapi?
 
Kujiji gani mkuu huku kwetu Rombo mgao ni kama kawa
Upande wa machame mkuu
Kuna mradi mkubwa wa maji unaitwa
Losaa Kia water suplay ( LKWS) ambao husambaza maji boma Hai hadi kia, na kabla ya mradi huu wananchi walikuwa na mabomba yao wenyewe hivyo ni ndoto kukatika kwa maji
 
  • Thanks
Reactions: ADK
Kuna ile lyamungo water supply( km sikosei )INA ofisi zao zimepakana na shule ya sere!!! Ni ndoto maji kukatika maeneo Yale!
 
Wakuu nawasalimu

Kijijini kwetu, mkoa wa kilimanjaro, ndani kabisa kijijini

Kwa miaka zaidi ya 20, tumekuwa tukipata maji safi ya bomba kabisaa, hayajawahi kukatika.
Safari hii kumetokea hitilafu kwasababu ya mvua kuwa nyingi mwaka huu.
Miaka 20 na zaidi

Ni maajabu haya!!!!
Wazee wangu watapitia wakati mgumu wa maji wiki hii ambapo wanafanya marekebisho.
hongereni mwaya sisi kwetu kila siku hukatika na yakirudi ni machafu huwezi hata kuyatazama
 
Kuna ile lyamungo water supply( km sikosei )INA ofisi zao zimepakana na shule ya sere!!! Ni ndoto maji kukatika maeneo Yale!
Yaah maji nadhani yanaanziaga makeresho kuna mapotomoko kule mkuu ya siku zote 366 za mwaka
 
Yaah maji nadhani yanaanziaga makeresho kuna mapotomoko kule mkuu ya siku zote 366 za mwaka
Hata Yale ya mfrejini mkuu hayakauki ( kwa temba na Yale ya KNCU) pia Yale ya pale kijiweni utaelewa km utakuwa mwenyeji sana!
 
Back
Top Bottom