Maagizo ya Serikali ya awamu ya 5 yaanza kupotoshwa

Maagizo ya Serikali ya awamu ya 5 yaanza kupotoshwa

Bobuk

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Posts
5,870
Reaction score
3,275
Serikali ya awamu ya 5 ya Dr. JPM imetoa maagizo 10 kwa wafanyakazi wa serikali na Taasisi zake,

Aidha kwa makusudi au kwa kuhujumu au kwa wivu au kukomoa watendaji wakuu wa serikali wameanza kupotosha maagizo hayo ya Rais JPM.

Na hapa nitaongelea agizo namba 2 ambalo wafanyakazi wa serikali na Taasisi zake wamesambazia. Kulingana na waraka huo agizo hilo no 2 linasomeka hivi

2. SAFARI ZA NJE YA NCHI

a. Safari zote za nje ya Tanzania zimepingwa marufuku kuanzia sasa. Hii pia inahusisha safari zilizolipiwa na wahisani. (mwisho wa kunukuu)

Lengo la agizo hilo la Mh JPM ilikuwa na kuokoa pesa a zserikali ambazo zilikuwa zinatumiwa na viongozi wa serikali waandamizi kusafari nje kwasababu mbalimbali, ikiwemo safari za mhimu na sisizokuwa za mhimu. Mpaka hapo mimi sina tatizo.

Nilimsikia KMK balozi Ombeni Sefue akisema kwamba iwapo itabidi kiongozi/mtumishi wa umma kusafiri nje ya nchi basi ni lazima apate kibali cha Ikulu.

Lakini hao watendaji wakuu wa serikali ktk agizo hilo wameongeza hiyo statement kwamba hata zile safari zinazolipiwa na wafadhili. Je, kuna mantiki gani ya kumuzuia mfanyakazi wa serikali kwenda nje ya nchi kama safari yake 100% inalipiwa na wahisani? Kwanini apate kibali cha Ikulu?

Je, serikali kwa kumzuia huyo mfanyakazi kwenda safari nje ya nchi inayolipiwa 100% na wahisani inakuwa imeokoa kiasi gani cha pesa?

Madhara ya kongeza hiyo statement ya kwamba hata safari zinazolipiwa na wafadhali:

Nimeshuhudia lecturers ambao wanafanya kazi vyuo vya serikali wakishidwa kusafari kwenda nje ya nchi kufundisha vyuo vingine wanavyoshirikiana navyo, Wanaitwa Visting lecturers. Pamoja na kwamba gharama zote 100% zinalipiwa na host University.

Nimeshuhudia Watafiti wakishindwa kwenda kwenye makongamano ya kisayansi ambayo yanalipiwa na mashirika ya kimataifa. Mfano kongamano la shirika la Afya duniani, WHO, ambalo litaanza Jumatatu. Ambapo washiriki hao tayari wamelipiwa na WHO kwa 100%.

Nimeshuhudia watafiti wakishindwa kusafiri kwenda UK, kuhudhuria kuandika rasimu ya pamoja ya utafiti ya EDCTP, ambapo watafiti hao walikuwa wanalipiwa na EDCTP kwa 100%.

Nimeshuhudia wafanyakazi wa serikali ambao wamepata scholarship za kwenda kusoma nje (masomo ya muda mfupi na mrefu), wakishindwa kuondoka kwasababu hawana kibali cha Ikulu.

Je, nini mantiki ya kufuta safari za nje zinazogharimiwa na wafadhili kwa 100%. Mimi ninaona watendaji wakuu wa serikali wameamua kupotosha agizo hilo kwa lengo la kukomoana au tukose wote, kwasababu wao ndio walikuwa wanufaika wakubwa wa safari za nje zinazogharamiwa na serikali.

Ninaomba walio karibu na Dr. JPM, mumueleze kwamba maagizo yake yameanza kupotoshwa kwa lengo la kumhujumu. Hakuna sababu yeyote ya kupata kibali cha Ikulu kwa safari ya nje ya nchi kwa safari ambazo serikali haigharamii hata centi moja. Hivi hiyo Ikulu itakuwa inafanya kazi ngapi?

Sidhani kama Rais JPM anataka kuifanya nchi hii kama kisiwa wakati dunia imeshakuwa kama kijiji. Au Dr, JPM sidhani kama anataka kuifanya nchi hii kama North Korea.

Mimi naomba atengue hiyo statement inayosema hata safari zinazolipiwa na wafadhili. Ibaki safari zote za nje ya nchi ambazo serikali inagharamia 100% au partially ndiyo zipewe kibali cha Ikulu.
 
natumaini hao wanaohujumu agizo hilo ni wasopenda kasi ya jamaa,,na watashindwa tu
 
Hata kama ni wafadhili mtumishi wa umma anapoteza muda. Vile vile lazima tujue taifa li nanufaikaje wasije wakiwa wanafanya kazi bi nafasi. Kibali ni lazima
 
Hata kama ni wafadhili mtumishi wa umma anapoteza muda. Vile vile lazima tujue taifa li nanufaikaje wasije wakiwa wanafanya kazi bi nafasi. Kibali ni lazima

sidhani kama hizo safari ni za kustukiza hivo? Mbona wanapata muda wa kuprocess visa? Pia hao wahadhiri lazima tujiridhishe wanapokuwa huko nje nani anafundhisha vipindi vyao, wapo wahadhiri kama semboja na semakafu wao kiguu na njia kilasiku.
 
Wanapoteza mida wa kazi, ujue wanapokuwa huko nje mshahara unahesabu huku nya na mwisho wa mwezi anakinga kama kawaida.

Ni lazima hizo safari zinazolopowa 100% na wafadhili zidhibitiwe pia
 
sidhani kama hizo safari ni za kustukiza hivo? Mbona wanapata muda wa kuprocess visa? Pia hao wahadhiri lazima tujiridhishe wanapokuwa huko nje nani anafundhisha vipindi vyao, wapo wahadhiri kama semboja na semakafu wao kiguu na njia kilasiku.

Semekafu tena jamani
 
Neno kuhujumu maagizo ningelielewa kama wangeishia kuongeza hilo neno halafu yet watu wakaenda lakini kama hawaendi hujuma iko wapi? may be useme hawakulielewa vizuri agizo la Rais.

Hata hivyo mimi sionagi tija ya hizo tafiti, mfano mdogo ni kituo cha utafiti wa malaria Ifakara zaidi ya miaka ishirini sasa hata sijui wanatafiti nini maana hatuoni matunda ya hizo tafiti. afadhali wasiende tu maana wanatumia advantage hata kufanya mambo binafsi yasiyo na tija kwa nchi, hao wafadhili hiyo hela si afadhali wangeilete hapa tununue madawa ya kuangamiza mazalia ya mbu watu wengi wangenufaika?
 
Kitengo cha mawasiliano cha Rais Ikulu kiimarishwe. Hii ya kufafanua masuala yanayopotoshwa ama ambayo hayajaeleweka ni kazi ya kitengo hicho.Pia kitumie mbinu na njia za kisasa za mawasiliano, hivi wapo twitter, facebook au ndio wanatumia kule kwa Issa Michuzi bado? Rais anahitaji good, qualified, up-to-date and trendy PR team.
 
upoteze muda wa kuitumikia nchii kwa safari za nje? akiruhusu watu watatafuta safari lukuki za wahisani na hivyo hawatafanya kazi za ndani.naona tangazo la magufuli liko sawa kabisa kwamba hamna kwenda njee kivyovyote mpaka ikulu iridhie kwa wafanyakazi wa serikali
 
upoteze muda wa kuitumikia nchii kwa safari za nje? akiruhusu watu watatafuta safari lukuki za wahisani na hivyo hawatafanya kazi za ndani.naona tangazo la magufuli liko sawa kabisa kwamba hamna kwenda njee kivyovyote mpaka ikulu iridhie kwa wafanyakazi wa serikali

Sawa kabisa.
 
Ni mda kazi na hakuna safari, full stop. Tatizo watz wengi wanapenda short cut sana na michongo, wahisani watuvumilie tu, sahivi tuko kikazi zaidi Tz. Unataka safari nenda ukazunguke vijijini na rais kasema
 
Ndo hvo hakuna kusafiri kiholela, huku Ofsini kazi unamuachia nani? Au ndo ile kupiga kibunda afu unajifanya kusafiri Nje? Na huko Nje unafanya kwa Maslahi ya nani? Huoni kwamba huo mwanya waweza kutumika kumshawishi Mlipiwa na hatimaye kuingiza Taifa katika Mikataba mibovu inayowabeba Waliomdhamini kusafiri? Rejea kina Nyalandu siku za nyuma hapa kila Uchao yupo America na "Anti Ezkl" ndo matokeo yake tunashangaa Twiga wetu haoooooo wamepata soko Njeeeee!
 
Kuna principle inasema ili kuzuia kenge wasiingie kwenye msafara wa mamba na mamba wasiingie kwenye msafara wa kenge unazuia misafara yote miwili hakuna namna😎
 
Mkuu kuniambia huoni tatizo kama safari inalipiwa na wafadhili kwa 100% ni ujinga uliopindukia. Hebu fikiria hivi:-

  • Ni maamuzi mangapi yatasimama kukusubiri wewe urudi kwenye safari uliyofadhiliwa na mfadhili wako?
  • Unapoteza muda kiasi gani kufanya kazi uliyotakiwa kufanya? Kwa mujibu wa sheria, kila mwajiriwa anatakiwa kufanya kazi sio chini ya saa 40 kwa wiki. Wewe haupo ofisini kwa wiki mbili mfululizo simply unahudhuria makongamano sijui wapi! Au labda ndio maana mmezibadilisha majina na kuziita "safari za kikazi" ili ku-justify ujinga.
  • Mshahara wako unakinga kama kawaida. Kwa taarifa yako kuna wengine wanamaliza hata mwaka hawajawahi kutoa fedha kwenye akaunti zao za mishahara; makongamano ya wafadhili yatatosheleza kila kitu.

Kwa hili naungana na JPM. Kama safari ni ya lazima woga au ugumu wa kuomba kibali Ikulu unatoka wapi? Mkuu, "the Tigers of the East" kwa wastani wananchi wao wanafanya kazi sio chini ya saa 70 kwa wiki wenye mamlaka wakiongoza kwa kukesha maofisini na ndio maana wanatisha kwa maendeleo duniani. Sisi kutwa kucha safari zisizo na maana na ma-secretary!
 
Hapa kazi tu...mwalalamika tena???? Mtafundisha hapa hapa,mtafanya makongamano hapa hapa.nakumbuka kale kawimbo kazuri "Mmeipenda mwenyewe,Chaguo letu milele,acha waisome namba" poleni kwa yaliowakuta ni jambo linalohuzinisha kwa mambo muhimu kama ulioyataja mleta mada kuzuiliwa eti kisa kupoteza pesa. Tukumbuke dunia ni kijiji tunahitaji exposure na tunahitaji kujifunza kwa wenzetu,ila kama Mkuu anataka tujifungie nchini mwetu as if hatuko duniani kama wenzetu.. Hali itakuwa mbaya.Nadhan kuna safari za kuzuia ila nyingine ni za muhimu kwa mtazamo wangu mm.
 
Mkuu umesema hayo ni "MAAGIZO YA SERIKALI" au "MAIGIZO YA SERIKALI YA AWAMU YA 5"
 
Inategemea. Mi nadhani kabla ya kuzuia safari za nje hasa zile zinazofadhiliwa wajiulize, serikali imewatimizia mahitaji wafanyakazi wake. Kwa mfano madaktari walidai nyongeza ya msahara hadi kipngozi wao akatekwa (Dr. Ulimboka) na hawakupngezwa.

Sasa hapo mtu ataacha kujitafutia riziki huko nje?

Wafanyakazi walidai nyongeza ya mshahara kima cha chini kifike sh315,000: hadi Rais Kikwete anamaliza miaka 10 hakupngeza. Sasa hapo akipata ka deal kake nje ya nchi napo umzuie?

Kuna mambo ya msingi serikali ya Magufuli inapaswa kuyafanya kabla ya kupiga marufuku tu.

Kwa mfano unapiga marufuku maduka ya dawa karibu na hospital wakati hospitali za serijali hazina dawa. Wizara ya Afya inadawa mabilioni na MSD imeshindwa kulipa. Sasa wagonjwa waende wapi? Tanzania hii unaweza ukawa tajiri na usitibiwe, utakufa na ugonjwa wako, labda uende private au nje ya nchi
 
Hizo tafiti za kisayansi zimelisaidia nini Taifa? Hizo tafiti zao wakafanyie vijijini sio Ulaya
 
Yaani mtu anajipinda kuandika thread inayomwonyesha kuwa kwakwe yeye muda si chochote, kwa hiyo kama mtu analipwa 100% na Donor ndio asiwe monitored?
 
Back
Top Bottom