Serikali ya awamu ya 5 ya Dr. JPM imetoa maagizo 10 kwa wafanyakazi wa serikali na Taasisi zake,
Aidha kwa makusudi au kwa kuhujumu au kwa wivu au kukomoa watendaji wakuu wa serikali wameanza kupotosha maagizo hayo ya Rais JPM.
Na hapa nitaongelea agizo namba 2 ambalo wafanyakazi wa serikali na Taasisi zake wamesambazia. Kulingana na waraka huo agizo hilo no 2 linasomeka hivi
2. SAFARI ZA NJE YA NCHI
a. Safari zote za nje ya Tanzania zimepingwa marufuku kuanzia sasa. Hii pia inahusisha safari za zilizolipiwa na wahisani. (mwisho wa kunukuu)
Lengo la agizo hilo la Mh JPM ilikuwa na kuokoa pesa serikali ambazo zilikuwa zinatumiwa na viongozi wa serikali waandamizi kusafari nje kwasababu mbalimbali, ikiwemo safari za mhimu na sisizokuwa za mhimu. Mpaka hapo mimi sina tatizo.
Nilimsikia KMK balozi Ombeni Sefue akisema kwamba iwapo itabidi kiongozi/mtumishi wa umma kusafiri nje ya nchi basi ni lazima apate kibali cha Ikulu.
Lakini hao watendaji wakuu wa serikali ktk agizo hilo wameongeza hiyo statement kwamba hata zile safari zinazolipiwa wa wafadhiri. Je, kuna mantiki gani ya kumuzuia mfanyakazi wa serikali kwenda nje ya nchi kama safari yake 100% inalipiwa na wahisani?
Je, serikali kwa kumzuia huyo mfanyakazi kwenda safari ya nje ya nchi inayolipiwa 100% na wahisani inakuwa imeokoa kiasi gani cha pesa?
Madhara ya kongeza hiyo statement ya kwamba hata safari zinazolipiwa na wafadhari. Nimeshuhudia lecturers ambao wanafanya kazi vyuo vya serikali wakishidwa kusafari kwenda nje ya nchi kufundisha vyuo vingine wanavyoshirikiana navyo, Wanaitwa Visting lecturers. Pamoja na kwamba gharama zote 100% zinalipiwa na host University.
Nimeshuhudia Watafiti wakishindwa kwenda kwenye makongamano ya kisayansi ambayo yanalipiwa na mashirika ya kimataifa. Mfano kongamano la shirika la Afya duniani WHO ambalo litaanza Jumatatu. Ambapo washiriki hayo tayari wamelipiwa na WHO kwa 100%
Nimeshuhudia watafiti wakishindwa kusafiri kwenda UK, kuhudhuria kuandika rasimu ya pamoja ya utafiti ya EDCTP, ambapo watafiti hao walikuwa wanalipiwa na EDCPT kwa 100%
Nimeshuhudia wafanyakazi wa serikali ambao wamepata scholarship za kwenda kusoma nje (mda mfupi na mrefu), wakishindwa kuondoka kwasababu hawana kibali cha Ikulu.
Je, nini mantiki ya kufuta safari za nje zinazoghalimiwa na wafadhiri kwa 100%. Mimi ninaona watendaji wakuu wa serikali wameamua kupotosha agizo hilo kwa lengo la kukomoana au tukose wote, kwasababu wao ndio walikuwa wanufaika wakubwa wa safari za nje zinazoghalamiwa na serikali.
Ninapenda walio karibu na Dr. JPM mumueleze kwamba maagizo yake yameanza kupotoshwa kwa lengo la kumhujumu. Hakuna sababu yeyote ya kupata kibali cha safari ya nje ya nchi kwa safari ambazo serikali haigharamii hata centi moja.
Sidhani kama Rais JPM anataka kuifanya nchi hii kama kisiwa wakati dunia imeshakuwa kama kijiji. Au Dr, JPM sidhani kama anataka kuifanya nchi hii kama North Korea.
Mimi naomba atengua hiyo statement inayosema hata safari zinazolipiwa na wafadhiri. Ibaki safari zote za nje ambazo serikali inagharamia 100% au partially.