Maagano na mateso kwa Wanadamu

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,725
9,051
Kama unaishi hapa duniani sasa na huna ufunuo (revelation) wa chochote kitakacho kutokea baada ya lisaa 1 au mawili au masaa 24 unachokijua ni kiasi gani cha pesa ulizonazo bank au mfukoni au watoto wangapi ulionao au nyumba ngapi ulizonazo au magari mangapi uliyonayo au kwa mwezi unapokea kiasi gani cha pesa basi wewe bado uko gizani hata kama ni mkristo

Watu wengi wanaishi sasa kwa magereza waliojifungia wenyewe kutokusamehe ,kutokuachilia mahusiano yanaumiza hayani magereza ambayo watu wamejifungia wenyewe na hakuna mtu wakuwafungua mpaka wajifungue wenyewe

Wengi wameweka maagano na Mungu maagano
Eg: Kipaimara wakati tunapata kipaimara tunaweka agano nanukuu : Mimi Emmanuel namkataa shetani na mambo yake yote --------

Hili ni agano analoweka mtu kwa niaba ya Mtoto anayebatizwa kwahiyo anamsaidia kuweka agano hili kwake au mbele za Mungu
Au mtu anapobatizwa anaweka agano hili mbele za Mungu hivyo kinachotokea hapa ni mtu anaweka agano la kumkataa shetani na mambo yote ( dhambi zote) na agano hili linaweka kati ya Mtu na Mungu
Agano hili linapowekwa kuna Kuhani,mashahidi,madhabahu,sadaka,na Roho(Mungu)

Agano la ndoa :Mimi Emmanuel namkubali ----
Kuwa mke wangu nitqmpenda nitamtunza kipindi cha shida na raha mpaka kifo kitutenganishe

Agano hili linawekwa mbele ya Mungu ni agano kati ya Mungu na wanaoweka agano hili kumbuka maagano haya yanapoweka kuna madhabahu, kuhani , sadaka , mashahidi

Watu wa huku duniani wanajua umuhimu wa na wanapoweka maagano hayo wanafahamu kwa uhakika wakiyavunja wanakufa hakika, na wako tayari kuyatetea kwa jinsi yeyote iliwasiyavunje,

Mungu nae anaheshimu sana Maagano kama watu wa huku duniani wanaheshimu maagano
Mungu ni zaidi Jana nilizungumzia aina tofauti tofauti ya maagano nikasema kuna maagano ya ndoa , maagano , ya mahusiano, maagano ya kazi, biashara n.k

Nilisema pia watu wengi hawajui unapikutana na mtu kimwili( mahusiano) na labda mkaweka maagano kuwa nitakuoa , nitaolewa na wewe , nitakuwa na wewe hata kama ulikuwa humaanishi unachosema hili ni agano na linaweza kukutesa maisha yote,
Ndio maana unakuta mtu aliwahi kuwa na Rafiki wa kike/ au wa kiume na kwasababu wanazozijua wenyewe hawakuoana akaolewa au akaoa mwingine lakini bado ndani ya moyo wake au nafsi yake huyu wa kwanza ananafasi kubwa,

Hili ni kutokana na agano waliloweka au kwakutamkiana kwa kujua au kwakutokujua ndoa nyingi ziko kwenye matatizo siku hizi sio adui ameingia ni watu waliingia kwenye mahusiano huku wakiwa tayari wana maagano waliyokuwa wameyafanya pengine wanayakumbuka au hawayakumbuki,

Agano ni agano tu haijalishi ni dogo au kubwa,

Nilienda mbali zaidi nikasema wasichokijua watu wengi haswa wakristo ni kuwa kuna agano la (mahusiano) Relationship Covenant, agano hili lina nguvu sana na hili linatokea automatically pale unapokutana kimwili na mtu,
Hili ni njia rahisi sana ya kufanya family's spirts transmission ( kuhamisha roho za kifamilia kutoka mtu mmoja kwenda mwingine, pale unapokutana kimwili na mwanaume au mwanamke kama alikuwa ana roho ( pepo kumi au ishirini ) roho hizi zote zinaweza kukuingia kirahisi sana, sasa angalia kama kama umekutana na watu watano wa koo familia tofauti tofauti alafu wote walau walikuwa na roho 10x5=

Hii inamaana utakuwa unaroho 50 jumlisha za kwenu, kumbuka ninazungumzia roho zilizoingia kwa njia ya maagano tu na njia hii huitwa agano la dam,kumbuka agano lina nguvu,

Jumamosi wale waliofanikiwa kufika kwenye maombi ya mtu mmoja mmoja tulifanya zoezi la eneo hili na waliona kilichotokea Jana tulijifunza zaidi juu ya hili

Jumamosi hii nitaendelea na maombi ya mtu mmoja mmoja kwa eneo hili la maagano hivyo kama wewe unajua au unaona ni mwathirika eneo hili na upo Arusha fanya mawasiliano kwa msaada

Nitaendelea zaidi na maagano mengi na ni maombi gani unaweza kufanya na namna ya kufuta kila agano uliloingia

Barikiwa

Pastor/Mwlm :Emmanuel
 
Back
Top Bottom