Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Wasafirishaji abiria wanaotumia pikipiki maarufu Bodaboda na Bajaji Mkoani Katavi wametakiwa kuwa mstari mbele kudumisha amani na kamwe wasiruhusu kushawishiwa kujiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa amani.
Wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani wakati wa mkutano na wasafirishaji hao uliofanyika katika ukumbi wa Polisi Kantini Oktoba 21, 2025, ambapo amewataka kuhakikisha kuwa amani inadumishwa wakati wote wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Aidha, Kamanda Ngonyani amewahakikishia kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vimejipanga vyema kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika hali ya utulivu na amani, hivyo amewahimiza kujitokeza kwa wingi kushiriki haki yao ya kikatiba ya kupiga kura Octoba 29, 2025.