Maafisa na Askari wa Polisi Zanzibar washirikiana na Vyombo vya Usalama katika matembezi ya ukakamavu

Maafisa na Askari wa Polisi Zanzibar washirikiana na Vyombo vya Usalama katika matembezi ya ukakamavu

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Leo, tarehe 10 Oktoba 2025, maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kutoka Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na Mkoa wa Mjini Nagharibi Unguja wameungana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na Idara Maalum ya Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika matembezi ya pamoja. Matembezi haya yaliandaliwa kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya vyombo hivyo na pia kujenga afya ya mwili na akili kwa watendaji wake.
1760084392147.png

1760084412416.png

Picha mbalimbali kutoka matembezi hayo zinaonyesha maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba wakishiriki kwa bidii katika matembezi ya ukakamavu (route march) lililoshirikisha vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
1760084339231.png

Katika matembezi hayo, maafisa wa Polisi, wakaguzi pamoja na askari wa vyeo mbalimbali wa Mkoa Kaskazini Pemba walishirikiana na vyombo vingine vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Lengo la matembezi hayo lilikuwa kuendeleza ushirikiano kwa kuwakutanisha pamoja watendaji wa vyombo vya ulinzi ambao wana jukumu la kuhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi wa Zanzibar.

1760084357525.png

1760084437045.png

1760084451989.png
 
Back
Top Bottom