Maafande wa Kova wanasa majambazi 11

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watu 11 wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi hatari wanaojihusisha na makosa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutumia silaha.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema katika tukio la kwanza Kikosi Maalumu cha Kupambana na Kuzuia ujambazi cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kimefanikiwa kuwatia mbaroni majambazi 10 eneo ya Kidongo Chekundu kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha.

Aidha, alisema katika uchunguzi wa awali wamebaini kuwa watuhumiwa hao walihusika na mauaji ya aliyekuwa mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya Lehman’s Trader, aitwaye Petro Makubuli.

Watuhumiwa hao walipopekuliwa walikutwa na bastola aina ya Tourau yenye No. AXF 30336 ikiwa na risasi sita kwenye magazini.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Finias Hassan (65) dereva mkazi wa Manzese, Innocent Geitan (22) dereva ambaye ni mkazi wa Mbagala, Hillary Changa (28) mkazi wa Kurasini, John Joseph (32) mkazi wa Mbagala, Hamad Mwalimu (24) mkazi wa Temeke Mikoroshini na Deogratias Julius (22) mkazi wa Vingunguti.

Wengine ni Diktonis Mbowe (39) mkazi wa Temeke Mikoroshini, Babu Mohammed (32) mkazi wa Temeke Mikoroshini, Magase Timani (39) mkazi wa Kinyerezi na Boniface Kisako (33) mkazi wa Ulongoni.

Alisema katika tukio lingine mtuhumiwa Chacha Matinde ‘Mtoto wa Yesu’ (32) mkazi wa Tegeta Stendi amekamatwa kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha Januari 12, maeneo ya Tandika.

Mtuhumiwa baada ya kupekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola mbili, moja ikiwa imefutwa jina na namba na risasi sita, bastola ya pili aina ya Glock No; FHZ 358 iliyotengenezwa nchini Australia ikiwa na risasi nane kwenye magazini.

“Katika uchunguzi wetu wa awali pia mtuhumiwa amehusika na matukio mbalimbali ya
ujambazi wa kutumia silaha likiwemo tukio la Januari 8 mwaka huu la mauaji ya Mohammed Saidi ‘Eddy’ na kumpora silaha aina ya Glock No. FHZ 358 pamoja na fedha,” kamanda.

Katika tukio la tatu, askari wa doria walifanikiwa kukamata bastola tatu aina ya Chinese, baada ya kuwatilia mashaka watu watatu waliotembea kwa miguu, ambao mmoja alikuwa amebeba mfuko wa rambo.

Aliongeza kuwa baada ya askari kusimamisha gari ghafla watu hao walianza kukimbia na kutupa mfuko waliokuwa wameubeba.
 
Back
Top Bottom