Maafa Kagera: Ugali wa sumu waua mama na watoto wanne

Maafa Kagera: Ugali wa sumu waua mama na watoto wanne

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,945
Reaction score
63,725
Maafa tena Kagera: ugali wa sumu waua mama na watoto wanne. Ni baada ya kununua unga wa muhogo, wanne hali zao bado mbaya
uploadfromtaptalk1475908012073.jpeg
uploadfromtaptalk1475908017718.jpeg

IMG-20161008-WA0004.jpg

MAMA na watoto wake wanne wamefariki dunia katika Kijiji cha Kyebitembe wilayani Muleba mkoani Kagera, baada ya kula ugali unaosadikiwa kuwa na sumu.
Waliofariki dunia ni Julitha Julius (35), Haujeni (14), Superius (12), Julius (4) na Paschazia mwenye umri wa miezi sita.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamilanda, Trasias Baltromeo, alidai kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa tisa mchana.
Baltromeo alidai familia hiyo baada ya kumaliza kula walianza kutapika na walifariki dunia wakati wakipelekwa katika Kituo cha Afya cha Kimaya kilichoko jirani na kijiji hicho.

Alisema baada ya kula walianza kutapika na kuhangaika, hata hivyo wananchi walifika ili kutoa msaada wa kuokoa maisha yao lakini haukuzaa matunda ambapo walifariki.

ìNilipofika nilikuta hali si nzuri, nilikuta wakiwa wanatapika, hivyo nilitoa taarifa Kituo cha Polisi Kyebitembe ambapo walifika wakati wakiwa wanakimbizwa hospitali ndogo ya Kimeya ambapo mama yao na watoto wawili walifariki,îalisema.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Augustino Ollomi, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na hakuna mtu aliyeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
Ollomi alisema miili ya marehemu inafanyiwa uchunguzi na wataalamu wa afya ili kujiridhisha na kutambua aina ya sumu iliyowaua.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango, alisema jopo la wataalamu wa afya na Jeshi la Polisi walikwenda katika Kituo cha Afya cha Kaigara na Hospitali ya Rubya kufanya uchunguzi.

Alisema baada ya kufanya uchunguzi watalaamu hao hawakuweza kubaini aina ya sumu iliyokuwepo katika chakula hicho, hivyo wamechukua sampuli kwa ajili ya kupelekwa Ofisi ya Mkemia Mkuu mkoani Dar es Salaam, kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mkuu huyo alikemea vitendo vya mauaji vinavyofanyika katika tarafa ya Kimwani kwani hilo ni tukio la tatu kwa mujibu wa vyombo vya dola la familia kuwekewa sumu kwenye vyakula na watu kupoteza maisha.

ìKitendo hiki kinasikitisha cha kuondoa uhai wa mwezio na si mafundisho ya Mungu licha ya waliofanya hivyo kuwa miongoni mwa waumini wa kiroho kwani wangetumia sheria kushitakiana kama hakuna usalama,îalisema.

Ruyango alisema Jeshi la Polisi na kamati za ulinzi na usalama za kijiji na kata, zimepewa jukumu la kufanya uchunguzi na kubaini waliohusika ili wachukuliwe hatua za kisheria.
 
Vyakula vya mizizi hasa mihogo ni vyakula vya hatar hatari pamoja na uyoga.
Mimi bwana hata uyoga ukipikwa home siuchangamkii naacha wale kwanza mpaka jioni nikiona siha zao zipo sawa hapo sasa ndo naweza nikala na dinner otherwise uyoga upo na thin demacation to poison na unachipuaga kiana aina hivi kama mihogo. Hata mbuzi au ng'ombe akijichanganya na na kisamvu a.k.a majani ya mihogo lazima aisome namba
 
Kumbe wachaga wapo sahihi kabisa kwa kukataa kuyala haya majitu yanayoitwa MUHOGO.In hatari sana
 
Vyakula vya mizizi hasa mihogo ni vyakula vya hatar hatari pamoja na uyoga.
Mimi bwana hata uyoga ukipikwa home siuchangamkii naacha wale kwanza mpaka jioni nikiona siha zao zipo sawa hapo sasa ndo naweza nikala na dinner otherwise uyoga upo na thin demacation to poison na unachipuaga kiana aina hivi kama mihogo. Hata mbuzi au ng'ombe akijichanganya na na kisamvu a.k.a majani ya mihogo lazima aisome namba
kwa hiyo unaacha ndugu zako kwanza wafe teh teh teh...
 
Uku ni kupatwa kwa kagera jamani,R.I.P mama na watoto wake
 
R.I.P ndugu zetu,kama kweli kuna watu wameweka hiyo sumu,mungu anawaona.
 
Mihogo usipoi-treat vizuri inaweza produce cyanide, hii ni sumu na inaua kabisa. Watu wanaweza mlaumu mama mkwe ila ukakuta hata alikua hana taarifa, tena hawa masikini hali yao inaweza changia kabisa maana masikini wengi misosi yao maandalizi yake ilimradi lisonge. Ni vizuri kufuatilia vyakula tunavyokula kila siku na sio kwenda kwa mazoea tu. Such a tragic loss, familia nzima kwa mpigo.
 
Hata kama ni kuaga sasa inatosha, ondoeni hizo picha kwa heshima ya marehem na ndugu zao.
 
Back
Top Bottom