hapo nikweli wla hakuna ubishiNadhani mtaniunga mkono kuwa wakati Mwl J.K.Nyerere anapata Uhuru wa Nchi hii alitangaza kuwa tunakabiliwa na maadui WATATU ambao ni, NJAA, UJINGA na MARADHI ila kwa bahati mbaya sana kwa mtazamo wangu na kwa watanzania wenye mtazamo kama wa kwangu ni dhahili mtakubaliana na mimi kuwa kwa sasa maadui hao wameongezeka na adui aliyeongezeka anaitwa adui ''UCHAMA''
Nasema UCHAMA ni adui wa nne kwasababu ya kile kinachoendelea ''SERIKALINI'' hasa huko Bungeni Dodoma maarufu kama mjengoni, imekuwa ni nadra sana kwa wafanya maamuzi wetu (Wabunge) kuweka maslahi ya taifa hasa katika maamuzi ya msingi, Kama utakuwa makini jambo hili lazima likutie shaka
Ni mangapi yamekuwa yakifanyika kinyume na maslahi ya TAIFA badala yake yanafanyika kwa maslahi vyama?, hoja Binafsi ngapi zinazimwa bungeni ''ETI'' kulinda heshima ya chama?, Wabunge wangapi wanazomewa bungeni hasa wakisema juu ya maslahi ya wananchi?, Wabunge wangapi wakionyesha nia thabiti ya kutetea maslahi ya Wamanchi wanazimwa na Wakuu wa vyama vyao?
Ni rahisi sana kujibu maswali hayo hapo juu na jibu ni rahisi kuwa kwa mwendo huu hatuwezi kupiga hatua maana ''UCHAMA'' imekuwa ndiyo nongwa kwa maendeleo yetu
Nawasilisha kwa uchungu!!

Adui aliyeongezeka ni RUSHWA. Lakini mimi siamini kama UJINGA bado ni adui kwa jamii ya Watanzania wa leo; kuna watoto wadogo hivi leo kukwea pipa mpaka China na elimu yao ya Std VII ni kawaida bado utawaita hao ni wajinga?

Kwa maoni yangu maadui waliobaki ni

1) RUSHWA

2) UMASKINI (unaosababishwa na namba moja)

3) MARADHI (yanayosababishwa na namba 2)

Tukiangamiza RUSHWA tutakuwa na rasilimali za kutosha kukabili UMASKINI wa Watanzania na hivyo kuwajengea uwezo wa kuangamiza MARADHI

Vincent, ujinga bado ni adui! Mfano, mkubwa fulani akidanganya na wewe ukasema amedanganya, wewe ndio utakayeonekana una makosa na siyo aliyedanganya. Kama huu siyo ujinga ni nini? Kwenye daladala dreva akiendesha vibaya na ukatokea kulalamika kuwa anaweza kusababisha ajali, utasikia baadhi ya abiria wanasema: "ajali zimepangwa na Mungu. Kama Mungu hajapanga hata kama akiendesha vibaya hakuna ajali itakayotokea." Na huyo mlalamikaji akitaka kuchukua hatua mfano kwenda polisi anakosa ushirikiano kabisa kutoka kwa abiria wenzake ambao wanamgeukia na kuanza kusema "ana matatizo binafsi." Kama huu siyo ujinga ni nini? Kwa hiyo adui ujinga bado anaitesa jamii ya watanzania.